MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - UMUHIMU WA NADHARIA KATIKA UHAKIKI WA FASIHI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: UMUHIMU WA NADHARIA KATIKA UHAKIKI WA FASIHI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Swali (Jadili umuhimu wa nadharia katika uhakiki wa fasihi) nadharia ni jambo la kweli (factual theory) husaidia kutafuta ukweli wa kazi, ni msingi wa kupimia ukweli unaowakilishwa.
  • Ni nyenzo ya kufikia maana halisi ya kazi ya fasihi.

  • Kumtahadharisha mhakiki kuwa makini

  • Humsaidia Mhakiki kulinganisha na kulinganua vipengele katika jamii kamavile, utamaduni, uchumi, siasa.

  • Nadharia huchochea akili za Mhakiki. Inampa shauku/hamu ya kusoma kazi mbalimbali za fasihi kwa madhumuni ya kulinganisha.

  • Humpa mhakiki tajriba ya tanzu mbalimbali za fasihi.

  • Ni Msingi wa kisayansi.

  • Huonesha upeo wa kuhakiki. Hutambulisha mambo ya kuzingatiwa ili kuondoa utata.

  • Humsaidia Mhakiki kuwa yakinifu.

  • Hutoa ulinganifu kati ya fasihi na dunia ya kawaida.

  • Ni msingi wa kupima hali ya kawaida na hali inayowasilishwa katika fasihi. Huonesha kuwa fasihi ni hai na inahusiana moja kwa moja na dunia ya kawaida. Kwa hivyo, nadharia husaidia kutoa kazi ya fasihi katika udhahania na kuiweka katika hali ya ukweli.

  • Ni hazina ya lugha ya kisanaa.