MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - TATHMINI YA MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: TATHMINI YA MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Lugha ya Kiswahili baada ya uhuru imepata mafanikio kadhaa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:
  1. Uendelezwaji wa Kiswahili.
    Kiswahili kimeweza kuendelezwa kwa njia mbali mbali kama vile kufundisha kama somo moja wapo katika ngazi zote za elimu nchini, kufanyiwa utafiti, kusanifiwa na kutumika kama lugha kuu ya mawasiliano.
2. Kuongezeka kasi ya ueneaji wa lugha ya Kiswahili.
         Kiswahii kimeweza kuenea hadi nje ya Tanzania katika mataifa mbali mbali na hata kufikia moja wapo lugha ya kimataifa na pia kuongezeka msamiati.
3. Kuongezeka kwa uundwaji wa vyombo vya ukuzaji Kiswahili.
    Kuendelea kujitokeza vyombo mbali mbali vya ukuzaji wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania  ni mafanikio makubwa kwa upande wa lugha ya Kiswahili kwa sababu vyombo hivyo vimewea kuikuza lugha ya Kiswahili kwa njia mbali mbali.
4. Kutumika Kiswahili katika vyombo vya habari vya nje.
    Kuendelea kutumika lugha ya Kiswahili katika vyombo mbali mbali vya habari vya nje kama viel BBC. Deutchwelle,radio japani, sauti ya amerika na nyinginezo kumeifanya lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha mashuhuri duniani