MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MCHANGO WA WIZARA YA ELIMU KATIKA MAENDELEO YA LUGHA (KENYA)

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MCHANGO WA WIZARA YA ELIMU KATIKA MAENDELEO YA LUGHA (KENYA)
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Kwa Muhtasari
WIZARA ya elimu nchini Kenya ni mojawapo ya asasi mbalimbali zenye nafasi muhimu katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili.
Miongoni mwa majukumu yake ni pamoja na kuhakikisha kwamba kuna sera madhubuti katika viwango vyote vya elimu nchini. 
Pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa viwango vya utoshelevu vya walimu wa Kiswahili vimezingatiwa ili kuboresha ufaafu wa walimu. Ni majukumu haya pamoja na mengine, yanayoifanya Wizara ya elimu kuwa na nafasi muhimu katika kuendeleza na kukikuza Kiswahili nchini. 
Katika kufanya hivyo, bila shaka kuna changamoto ambazo ni lazima zishughulikiwe ikiwa asasi hii muhimu inaazimia kutimiza wajibu wake.
Miongoni mwa changamoto hizo ni sera za elimu, mielekeo ya wadau katika sekta ya elimu wakiwemo walimu, wanafunzi na wazazi pamoja na ukosefu wa fedha za kugharimia mipango yote ya wizara ya elimu. Wizara yenye jukumu la kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili ni ile ya elimu. 
Wizara hii hutoa mipango ya kisera ambayo hutafsiriwa kwenye sera ya lugha, mihutasari ya masomo na kwenye asasi zinazokuza Kiswahili. Kwa kuwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu viko chini ya Wizara hii, basi haiwezi kukwepa matatizo yanayoikumba sekta ya elimu humu nchini. 
Hata hivyo, makala haya yamezingatia hasa majukumu ya wizara ya elimu kwani ndiyo inayohusika kwa kiwango kikubwa na masuala ya kisera yanayoathiri taaluma ya Kiswahili. Hivyo basi, ni jukumu la Wizara ya elimu kupanga mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu kuyakabili matatizo hayo. 
Kwanza kabisa, Wizara ya elimu nchini Kenya ina jukumu la kuhakikisha kwamba walimu wanaofundisha somo la Kiswahili ni wale waliofuzu na kutosheleza masharti ya kitaaluma.
Isistoshe, ina jukumu la kuhakikisha kuwa walimu wa kutosha wanapatikana ili kuboresha ufundishaji wa Kiswahili shuleni na hata vyuoni.
Kimsingi, Wizara ya elimu inatakiwa kupanga mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu ya jinsi ya kupata walimu wa kutosha si tu walimu wa Kiswahili bali pia na walimu wa masomo mengine.
Jambo hili linapozingatiwa kwa njia inayofaa, taaluma ya Kiswahili itaendelezwa ipasavyo. 
Fauka ya hayo, Wizara ina jukumu la kuimarisha mieleko ya wanafunzi na wadau wote katika sekta ya elimu. Ukuzaji wa Kiswahili utawezekana ikiwa mielekeo ya wanafunzi katika kuitumia lugha hiyo itakuwa chanya.
Kuhusu mwelekeo wa kutaka au kutotaka kuzungumza lugha ya kigeni, Schooling (1990:71) anaeleza kwamba: Mtazamo chanya kuhusu lugha ya kigeni humchochea mtu kutaka kujifunza na kutumia lugha hiyo pindi nafasi ya kutumika inapopatikana (Msanjila 2005:215). 
Mtazamo
Kwa upande mwingine, mtazamo hasi kuhusu lugha ya kigeni humfanya mtu achukie kila jitihada zinazofanywa za kutaka kuongeza matumizi ya lugha hiyo.
Kinachojitokeza hapa ni ukweli kwamba katika mazingira ya Kenya, Wizara ya elimu, shule na vyuo kwa pamoja vinatakiwa kujenga mazingira chanya kwa wanafunzi ili wao wenyewe wahimizike kutaka kujifunza lugha nyingine kwa bidii kuliko kulazimishwa kutumia lugha ngeni kama Kiingereza bila wao kupenda. 
Isitoshe walimu na Wizara ya elimu wanaweza kushirikiana katika jitihada za kuimarisha mwelekeo chanya kwa wanafunzi katika matumizi yao ya Kiswahili.
Jambo hili lawezekana kupitia midahalo shuleni na hata nje ya mazingira ya shule. Ili kuipa mashiko midahalo hii, walimu wanaweza kuwashindanisha wanafunzi kividato yaani Kidato cha I na II, kidato cha II na III na kadhalika. Hatimaye washindi wa kila kikundi wapewe zawadi.
Kwa kufanya hivyo, Wizara ya elimu pamoja na walimu wa shule za msingi na sekondari watakuwa wanachangia kuendeleza mwelekeo chanya katika matumizi yao ya Kiswahili. 
Jukumu jingine la Wizara ya elimu ni kuhakikisha kuwa sera zinazoundwa na kutekelezwa zinachangia kuimarisha Kiswahili. Japo wizara ya elimu imetambua umuhimu wa Kiswahii, bado inaendeleza sera zinazoikandamiza lugha hii.