MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - Wazungumzaji wa Kiswahili ni zaidi ya milioni 200- Prof. Mutembei

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: Wazungumzaji wa Kiswahili ni zaidi ya milioni 200- Prof. Mutembei
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
[Image: image1170x530cropped.jpg]
Vuta nikuvute imeibuka kuhusu idadi ya watu wanaozungumza lugha ya kiswahili duniani. Je ni milioni 98 kweli kama inavyojadiliwa sasa au la?
Lugha za asili barani Afrika zinaangaziwa tarehe 25 mwezi huu wa Mei, ambayo ni siku ya Afrika.
Kuelekea siku hiyo, kumekuwepo na taarifa ya kwamba lugha ya Kiswahili ambayo asili yake ni barani Afrika, ni ya kwanza kwa kuzungumzwa na watu wengi zaidi ikifuatiwa na Hausa halafu Yoruba.
Jambo lililoibua hoja na mjadala mzito kwenye mtandao wa Twitter, si kuongoza kwa lugha hiyo bali ni idadi iliyowekwa ambayo ni milioni 98.
Ili kusaka ukweli wa hoja hiyo nimezungumza na Profesa Aldin Mutembei, kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, TATAKI, na kumuuliza je takwimu ni sahihi?
Ukweli ni kwamba Kiswahili kinazungumzwa na watu zaidi ya milioni 200. Hii ni kutokana na taarifa ya kiutafiti ya Profesa Mutembei kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyoitoa 7 Mei, 2018.