MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: KONGONI NGULI KONGONI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: KONGONI NGULI KONGONI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
BOFYA HAPA CHINI KUFUNGUA >>>>>
[attachment=614]
Siku hizi neno ” kongole” latumiwa kwa maana ya pongezi. Lakini kwa Kiswahili cha kale lilikuwa na maana ya ukaribishaji pia.
Na maana ya “kongoni” ni karibuni (uwakaribishapo zaidi ya mtu mmoja). Kwa kumkaribisha mtu mmoja husemwa: kongo; kwa mfano, Mgeni kongo! Na kitenzi chake ni kukongowea, yaani kukaribisha: Namkongowea mgeni. Hili ndilo neno la asili la Kiswahili kabla ya kutumiwa “kukaribisha”, ambalo asili yake ni lugha ya Kiarabu.
MAANA ZA BAADHI YA MANENO YALIYOTUMIWA KATIKA SHAIRI “KONGONI NGULI KONGONI”:
– kongoni = karibuni
– nguli= mashujaa (pia shujaa)
– nde = nje
– tuwakongowee = tuwakaribishe; tuwalaki
– ‘siselee (asiselee) = asibaki
– pamwe na = pamoja na
– ndume = madume; wanaume
– ghamidha = ushupavu
– kondo = vita
– watezi wa bangu (wachezaji wa bangu) = wapiganaji vita. (Katika Kimvita cha kale kulikuwa na usemi (siku hizi zaitwa “nahau”) “kuteza bangu” , kwa maana ya kupigana vita).
– jasara = wingi wa ujasiri
– sera = tabia au vitendo atendavyo mtu maishani mwake
– kuterema = kufurahi (nderemo = furaha)
– ndima = kazi ngumu
– tujifunge masombo (masombo ni nguo inayotatiwa na wanaume kwa kuzungushwa tumboni na nyuma yake wakati wa kupigana vita au kufanya kazi ngumu. Wanawake hufunga vibobwe (vibwebwe) lakini wanaume hujifunga masombo.) Kwa mfano, katika ubeti wa pili wa shairi, “Mgogoto wa Zamani”, lililotungwa na mshairi wa kale wa Mvita, Muyaka bin Haji (1776-1840), alipokuwa akiwahamasisha Wamvita wenziwe kupigana vita dhidi ya utawala wa Oman (ambao wakati huo makao yake makuu yalikuwa Zanzibar), unasema:
Jifungetoni masombo, mushike msu na ngao
Zile ndizo zao sambo, zijile zatoka kwao
Natuwakaliye kombo, tuwapigiye hario
Wakija tuteze nao, wayawiapo ngomani.
– wafileo = waliokufa
– waukile = wameondoka; wamekufa
– mauko = kifo
– akudare = akuguse
– huj’epui = hujiepushi; hukimbii
– kuyacha = kuyaogopa
– mare = marefu; makubwa
– watezaji shere = wachezaji shere; wanaowafanyia watu mizaha ili waonekane ni wajinga. (Hivi karibuni nilimsikia Waziri mmoja wa Tanzania akihutubia mkutano wa hadhara Nairobi akilitumia neno “shere” kwa makosa. Alilitumia kwa namna iliyoonesha kuwa kumcheza mtu shere ni kuzuri, na ilhali ni kinyume chake).