MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU D : MAENDELEO YA KISWAHILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU D : MAENDELEO YA KISWAHILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU D : MAENDELEO YA KISWAHILI

1. Lugha ya Kiswahili ni lulu ya Taifa la Tanzania, barani Afrika na duniani kote. Toa sababu tano zenye mifano kuthibitisha dai hilo.
 
MAJIBU
UTANGULIZI
Lulu ni kitu cha thamani, Kiswahili kinafananishwa na kito cha thamani kutokana na umuhimu wa lugha yenyewe na historia yake kwa jamii.
 
KIINI (Sababu tano)
  • Kiswahili hutumika kama lugha rasmi bungeni, mahakamani, serikalini
  • Kiswahili hutumika kufundishia shule za msingi na kama somo kwa shule za sekondari na elimu ya juu (Tanzania)
  • Nchi za nje nyingi zimeanzisha mifumo ya elimu inayohusisha somo la Kiswahili. Baadhi ya nchi hizo ni Marekani, Canada, China, Sudani na Botswana
  • Matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania mfano: Televisheni (Channel Ten,TBC, ITV, Clouds)
Redio (TBC, Radio One, Efm, Magic Fm)
Magazeti (Mwananchi, TanzaniaDaima, Uhuru)
Nchi za nje – mfano BBC, Sauti ya Amerika, Redio Vatican, Redio France International, Deutsche Welle
  • Kiswahili hutumika kwenye mitandao ya kijamii kama ‘Facebook, Twitter, WhatsApp, n.k
  • Matumizi ya Kiswahili katika mfumo wa kibiashara kimataifa na kitaifa mfano mikataba ya kibiashara, vituo vya kibiashara kama Beijing China, New York Marekani, Moscow Urusi, Dubai Uarabuni, London Uingereza. Hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana.
  • Kiswahili kimepewa hadhi ya kimataifa kufikia kuwa lugha ya tano katika umoja wan chi huru za Afrika. Kiliteuliwa kuwa moja ya lugha za kiafrika itakayotumika pamoja na lugha za kigeni kama Kiingereza, Kireno, Kifaransa na Kiarabu.
  • Kiswahili hutumika kama lugha ya Taifa nchini Tanzania, vilevile nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.
  • Kiswahili hutumika katika shughuli za maisha ya kawaida ya kila siku kama vile majumbani, sehemu zenye mikusanyiko kama kanisani, misikitini, n.k
 
HITIMISHO
Toa hitimisho zuri linaloendana na swali.

2. Dini inasaidiaje katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania? Toa hoja tano (5)
 
MAJIBU
UTANGULIZI
Dini ni miongoni mwa taasisi za kijamii zenye mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili hapa nchini Tanzania. Mchango wa dini katika kukuza na kueneza Kiswahili unajipambanua kama ifuatavyo:
 
KIINI
  • Mahubiri na mawaidha ya kidini hutolewa kwa lugha ya Kiswahili
  • Madrasa na shule za dini za watoto (Sunday schools) hufundisha kwa kutumia lugha ya Kiswahili
  • Uanzishwaji wa vyombo vya habari vya kidini kama redio, magazeti na televisheni ambavyo hurusha na kutoa habari kwa lugha ya Kiswahili mfano: Redio Maria, Redio Imaan, Agape Televisheni, Magazeti kama Al-Noor, Mwangaza, n.k
  • Uanzishwaji wa shule pamoja na vyuo vya taasisi za kidini ambavyo hufundisha kwa lugha ya Kiswahili. Vilevile hufundisha walimu wa somo la Kiswahili mfano wa vyuo ni kama St. Augustine, Tumaini, TEKU, Mum, n.k
  • Pia taasisi za kidini zinamiliki shule nyingi za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu
  • Nyimbo za kidini kama kwaya na hata tenzi za rohoni, huimbwa kwa lugha ya Kiswahili mfano wasanii wa injili kama Rose Muhando, Christina Shusho, n.k huimba nyimbo zao kwa lugha ya Kiswahili na husikilizwa na watu wengi
  • Vilevile kanda na santuri za Kaswida nazo huuzwa na kusikilizwa na watu wengi ndani na nje ya nchi.
 
HITIMISHO
Toa hitimisho zuri lenye kuafiki mchango chanya wa dini katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili.