MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MASWALI NA MAJIBU -6: DARASA LA 3 & 4

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MASWALI NA MAJIBU -6: DARASA LA 3 & 4
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MASWALI NA MAJIBU -6: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Jibu maswali kwa kuchagua jibu na kuandika katika sehemu iliyowazi.
  1. Piga yowe maana yake ni………………
(a) piga kelele (b) imba kwa sauti ya juu © furahi sana
  1. Wanyama pori ni wale…………………
(a) wanaofugwa (b) waishio porini © tembo na simba
  1. Neno keti maana yake ni……………………
(a) kaa chini (b) simama © andika
  1. Huyu kijana ni mwerevu. Neno huyu limetumika kuonesha…………….
(a) umbali (b) karibu © sifa
  1. Mama yake aliaga dunia Aga dunia maana yake ni………………
(a) fariki (b) aga watu © fanya sherehe
  1. Mtoto mwenye adabu…………………
(a) hupendwa (b) hupigwa na watu wengi © hulia hovyo
  1. Lipi kati ya mazao yafuatayo ni nafaka…………………..
(a) nazi (b) mbaazi © mahindi
  1. Mtu anayefanya kazi ya kufua na kupiga nguo pasi huitwa………………
(a) mpiga pasi (b) dobi © maridadi
  1. Wakatafakari maana yake ni…………….
(a) wakasahau (b) wakakariri © wakafikiri
  1. Shangazi aliweka fedha na funguo………..ndani ya pochi.
(a) yake (b) zake © wake
SEHEMU C: Jibu kwa kuchagua maneno katika kisanduku ulichopewa.
Quote:Usingizi ulipaa, fedha lukuki, walikaa chonjo, waliangua kicheko, walipigwa butwaa, walitega sikio, kufuja mali.

  1. Watu wote……..waliposikia Juma ameuawa na majambazi.
  2. Wanafunzi wote…………walipomwona mwalimu wao anacheza dansi.
  3. Alikuwa na……………lakini hakuwa na mipango mizuri ya matumizi.
  4. Baada ya kuota ndoto ya kutisha……….usiku wote.
  5. Wanakijiji………….kumsikiliza mgombea wa ubunge alipofanya kampeni yake.
SEHEMU D: Jibu swali 16-20 kwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Andika kinyume cha sentensi hizi.
  1. Sitalala usingizi leo………………………..
  2. Chausiku hatarudi leo……………………
Kamilisha methali zifuatazo
  1. Mchagua jemba……………………..
  2. Jungu kuu……………………………
  3. Kila mtu humwabudu apitapo………………………
SEHEMU E: Vitendawili, Methali na Nahau
  1. Nyumba yangu ina mlango juu………………
  2. Haba na haba……………………
  3. Chapa mguu……………………..
  4. Kila niendapo hunifuata…………….
  5. Kula chumvi nyingi…………………
MAJIBU
  1. A
  2. B
  3. A
  4. B
  5. A
  6. A
  7. C
  8. B
  9. C
  10. B
  11. Walipigwa butwaa
  12. Waliangua kicheko
  13. Fedha lukuki
  14. Usingizi ulipaa
  15. Walitega sikio
  16. Nitalala usingizi leo
  17. Chausiku atarudi leo
  18. Si mkulima
  19. Halikosi ukoko
  20. Mlango
  21. Chupa
  22. Hujaza kibaba
  23. Tembea
  24. Kivuli
  25. Ishi niaka mingi