MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MASWALI NA MAJIBU YA SARUFI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MASWALI NA MAJIBU YA SARUFI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.

  1. Eleza maana ya ‘kiimbo’
    Kiimbo ni sauti maalum inayojitokeza unapotamka maneno fulani. (kupanda na kushuka kwa sauti)
  2. Tunga sentensi mbili zinazodhihirisha uamilifu wa aina mbalimbali wa kiimbo.
    Mama ameenda sokoni? -swali
    Mama ameenda sokoni. -kauli
  3. Tunga sentensi ya hali timilifu ukitumia kiunganishi cha kibantu
    Mwalimu na mwanafunzi wameenda nyumbani.
    na- kiunganishi cha kibantu
    wameenda – hali timilifu
  4. Kazi hii imekuwa ngumu kwangu. (maliza kwa ….ngumu)
    Kwangu, kazi hii imekuwa ngumu.
  5. Andika sentensi hii kwa hali ya ukubwa, wakati uliopita
    Ningepelekewa huyu ndama nyumbani ningefurahi.
    Nilipelekewa hilo dama jumbani nikafurahi.
  6. Tunga sentensi kutumia kirejeshi cha tamati.
    Kiti wakitumiacho kimevunjika.
    Kirejeshi tamati ni ‘cho’
  7. Taja yambwa za sentensi ifuatayo :
    Mjomba hakupikiwa mlo wa leo kwa bidii.
    Mjomba – Yambwa tendewa:
    Mlo- Yambwa tendwa
  8. Tunga sentensi kanushi kutumia kiambishi ‘a’
    Mtoto asipolishwa vizuri, hawezi kulala.
  9. Andika miundo yoyote miwili ya nomino katika ngeli ya U-ZI huku ukitoa mifano
    U-ny uzi-nyuzi
    u-nd ulimi-ndimi
    w-ny wembe-nyembe
    u- ukuta -kuta
  10. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kinyume
    Mwafrika anapenda kutii maagizo.
    Mzungu anachukia kuasi amri.
  11. Bainisha vitate vifuatavyo kwa kutunga sentensi moja. (alama 2)
    kaza, kasa.
    Mvuvi alikaza kamba alipomuona kasa akiwa ndani ya wavu.
  12. Taja ala za kutamkia vitamkwa vifuatavyo.
    /v/g/j/t/
    v- Midomo + Meno
    g – Kaakaa Laini
    j- kaa kaa ngumu
    t- Ufizi
  13. Bainisha shamirisho katika sentensi: (alama 3)
    Mwalimu atawasimulia wanafunzi hadithi kwa kipaza sauti
    Mwalimu-shamrisho kitondo,
    Hadithi- shamrisho kipozi,
    kwa kipaza sauti- shamrisho ala
  14. Toa mifano miwili ya matumizi ya ritifaa(’)
    Kuonesha king’ong’o kwa mfano ng’ombe
    Kuonyesha nambari iliyoachwa kwa mfano ’99
  15. Walipokuwa wanasoma mgeni wa heshima alifika (andika kwa wakati ujao)
    Watakapokuwa wakisoma mgeni wa heshima atafika.
  16. Tunga sentensi yenye ni uundo ufuatao:
    S KN(N+U+N+V)+KT(T+E+E)
    Mama na mtoto wake wanatembea haraka sana.
  17. Tunga sentensi mbili kutofautisha vitate hivi kimaana. (alama 2)
    (i) Hawara
    (ii) Hawala
    Hawara alifukuzwa nyumbani kwa kuwa mzembe.
    Alipomaliza kazi, alilipwa kwa hawala.
  18. Kanusha bila kutumia ‘amba’
    Nitavaa nguo ambayo ni safi.
    Sitafaa nguo iliyo safi.