MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: ANA TABU ASKARI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: ANA TABU ASKARI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
ANA TABU ASKARI
Maisha ya Askari, ya kufa ama kupona,
Yeye huona fahari, nchi yake ikipona,
Tena anajawa ari,halali anakazana,
Ana tabu Askari!

Hujavalia kombati, zake risasi begani,
Miguuni ana buti, na mkanda kiunoni,
Na siye tuvae suti, hujiona furahani,
Ana tabu askari!

Usiku huyu halali, nchi ibaki salama,
Hufika kila mahali, wima ama kachutama,
Na mtu huyu hajali, afe yeye hata kama,
Ana tabu askari!

Huiacha familia, hali mkewe mpweke,
Yake nchi kulilia, salama isalimike,
Ajabu nawaambia, yu radhi ahatarike,
Ana tabu askari!

Mshairi nimeona, nimtie utungoni,
Naye nimpange vina, na hadhira mbaini,
Mtu wa yake aina, nimeona duniani,
Ana tabu Askari!

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Shairi zuri sana
(08-29-2021, 12:47 PM)MwlMlela Wrote: [ -> ]Shairi zuri sana

Mtunzi anastahili pongezi