MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
Nitawapeleka Mtoni, Nitawalazimisha kunywa maji

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Nitawapeleka Mtoni, Nitawalazimisha kunywa maji
#1
Nitawapeleka Mtoni, Nitawalazimisha kunywa maji
Siku moja baba alimuamsha kijana wake apeleke ng'ombe machungani.
Mtoto akatoka na kundi la ng'ombe hadi porini. Ilipofika majira ya alasiri akawapitisha mtoni kisha akawarejesha zizini.
Alipofika baba yake akamuuliza;
Baba: Ng'ombe wamekunywa maji?!
Kijana: Niliwapeleka mtoni.
Katika Elimu na mchakato wa kujifunza kuna mambo matatu muhimu:-
1. Kufundisha; Bila shaka mtakubaliana nami kwamba, kuna matendo ya kufundisha (teaching activities) ambayo mwalimu anatakiwa ayafanye.
2. Kujifunza; pia yapo matendo ya kujifunza (learning activities) ambayo mwanafunzi anatakiwa ayafanye.
3. Upimaji na Udhibiti; lengo lake kwa kiasi kikubwa ni kupima ufanisi wa 1 na 2 hapo juu. Anapimwa mwalimu kama amefundisha, na mwanafunzi kama amesoma.
Mwalimu ambaye ameandaa skimu, ameandaa nukuu za somo, amesaini mahudhurio ofisini, ameandaa lesoni plani, amesaini klasi juno, amefundisha, ametoa mazoezi na kazi mbali mbalimbali, anakuwa anatekeleza majukumu ya ufundishaji, sawa na kusema ng'ombe wamepelekwa mtoni.
Ikitokea wanafunzi hawajisomei, hawaadhibiwi, wanafeli mitihani, hawaukizi maswali kwa mwalimu; hii ni sawa na kusema ng'ombe wamefika mtoni hawataki kunywa maji
Baada ya matokeo kutoka;
Stakeholders: Mwalimu kwanini wanafunzi wamefeli. kwanini hawakunywa maji?!
Mwalimu: *_Niliwafundisha_* niliwapeleka mtoni.
Pamoja na ukweli kwamba kujifunza ni jukumu la mwanafunzi, lakini je, tunahakikisha wanafunzi wanafanya matendo ya kujifunza? Wanafunzi wanawajibishwa vipi ikiwa hawatekelezi jukumu lao au wanazembea?!
Siku moja nikiwa darasani, katika mazungumzo na wanafunzi;
Wanafunzi: Naipenda nchi yangu, sitakubali ihujumiwe...(salamu ya sasa kuhimiza uzalendo)
Mimi: Hujuma mwaifahamu!?
Tukapiga hesabu ya pesa ambazo serikali inalipa katika huu mpango wa elimu bure, kama ada na gharama nyingine.
Nikauliza kuna mwalimu wa somo lolote hayupo?!
Walimu wa kila somo wapo, na wanafundisha, walimu wanalipwa, chaki zinanunuliwa, vitabu vipo shuleni, madarasa yanajengwa na Ada hamlipi.
Nikawaambia 'hapo ukifeli basi umehujumu nchi yako ambayo unasema hutakubali ihujumiwe.'
Mimi ni mwalimu. Madarasa ninayofundisha pamoja na kutokosa kipindi changu hata kimoja na kuomba vya ziada, nimekuwa nikiwasisitiza waniletee maswali yanayowatatiza muda wowote. Kwa mwaka sasa hawazidi watatu wanaokuja lakini hasa ni mmoja..
Nakubali wapo baadhi yetu walimu wanaotia doa sehemu ya ufundishaji lakini kama mtaalamu katika nafasi yangu nasema kwa kinywa kipana kwamba upande wa mwanafunzi (kujifunza) kuna mapungufu makubwa.
Andiko hili si lawama kwa yoyote, bali ni kuhamasisha kila mdau atimize yanayomhusu.
Elimu yetu imeingiliwa na siasa, wataalamu wengi wa tasnia yetu wamekuwa wanafanya kazi kisiasa. Wakuu wa shule na maafisa elimu wanaelemea kwenye siasa kuliko utaalamu wao katika utendaji. Huenda miongoni mwa vigezo vya kuhudumu katika nafasi hizo ni kustawisha maslahi ya kisiasa ya mamlaka za uteuzi, badala taaluma na elimu.
Niwakumbushe wote waliopewa dhamana katika nafasi mbalimbali tuwe wazalendo kwa nchi na taifa letu, elimu yetu ni nyenzo muhimu katika ustawi wa taifa hili.
Uzalendo ni kupenda nchi yako kwa mapenzi na wivu mkubwa, na kuweka mbele masilahi ya taifa, na si kupenda serikali.
Tuelewane:
Uzalendo ni kupenda nchi, taifa.
Uzalendo si kupenda chama, serikali.
Ndio maana hata ukiwa mtumishi wa serikali kuna mambo inatakiwa ujifinze kuyakataa kwa maslahi ya taifa lako sababu uzalendo wako sio kwa serikali bali ni kwa taifa na nchi yako.
Ningeweza kugusia sehemu nyingi katika mfumo wetu wa elimu, lakini kwa vile kuna mchakato wa maboresho ya mitaala, tutatoa maoni yetu huko.
Lakini walau niseme kwa ufupi kuhusu somo la hesabu;
Somo hili liwe la lazima hadi kidato cha pili, kisha liwe hiari (optional) kuanzia kidato cha tatu.
Mada kama Statistics, Linear programming na Accounts ziitwe junior O-level mathematics, mahususi kwa kidato I na II ambazo zitakuwa ni lazima kwa wanafunzi wote.
Mada kama logarithms, exponent radical,  zipelekwe kidato cha tatu ili wasome wanaotaka (watakaochagua) kusoma Maths.
Siku moja katika wasaa wa kunasihi wanafunzi, (sisi walimu huwa tunatenga muda wa _kupiga stori_ na wanafunzi kuhusu mambo mbali mbali nje ya mada)..
We spare three to five minutes talking contemporary issues
...nikawasimulia hiki kisa cha mzazi aliyemtuma mwanawe porini kuchunga ng'ombe.
Mwisho nikawaambia professionally ilitakiwa niwapeleke mtoni lakini wakuu wangu wananitaka nihakikishe mnakunywa maji.
Buchu, Hamza O.
+255 715 345 789
10/07/2021
Mwanza
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)