MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MISEMO,NAHAU NA METHALI ZA KISWAHILI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MISEMO,NAHAU NA METHALI ZA KISWAHILI
#1
Misemo ni kauli fupifupi ambazo hutumiwa na jamii kusisitiza ukweli wa jambo fulani. Kauli hizi huunganisha mawazo au dhana tofauti kuwa mwili mmoja na kupitisha ujumbe uliodhamiriwa na mnenaji au mwaandishi.
Pia, misemo ni fungu la maneno ambalo hutumiwa na jamii tofautitofauti kwa lengo la kusisitiza maadili fulani.
 
Kwa mfano tukisema mtu amegonga mwamba hatumaanishi kwamba amepiga jiwe kubwa kwa kifaa chochote au kwa mkono, bali tunamaanisha kwamba ameshindwa kuendelea katika jambo fulani.
Ifuatayo ni misemo ya kiswahili na maana yake.
Kupata jiko
Huu msemo haumaanishi kununua au kuazimz jiko la kupikia. Una maana ya kupata mke au kuoa. Kwa hivyo, mtu anaposema nimepata jiko anamaanisha kuwa ameoa.
Kuangusha uso
Maana ya huu msemo ni kuona aibu au soni mbele ya watu kwa jambo mbaya ulilolitenda. Mfano wa matumizi ni kama: ukitenda mema hapatatokea haja ya kujishusha hadhi kwa kuangusha uso kila wakati.
Kuenda mbwehu
Maana yake ni kutoa hewa mdomoni. Naneno lingine lililo na maana sawa na kuenda mbwehu ni kuteuka. Mfano wa matumizi ya msemo huu ni kama vile: Kwenda mbwehu ugenini ni dalili ya ulafi.
Enda msobemsobe
Maana kamili ya msemo huu ni kuenda pasipo na utaratibu wowote. Pia huweza kumaanisha kuenda pasipo na hiari. Mfano katika sentensi: alipougua malaria alikuwa akienda msobemsobe.
Enda mvange
Kabla ya kutoa maana ya msemo huu, ni vizuri uelewe kuwa maana ya neno ‘mvange’ ni ‘kombo’. Kwa hivyo mesomo huu unaweza kuwa ‘enda kombo,’ na maana yake mambo kufanyika kwa namna isiyotarajiwa. Kwa mfano, namshukuru Mola kwa sababu biashara yangu haikuenda mvange.
Chokoza nyuki mzingani
Mzinga ni nyumba ya nyuki. Musemo huu unamaanisha kuenda palipo na hatari na kujaribu kuichokoza au kuikabili kijiga hatari hiyo. Mfano katika sentensi: kung’oa simba usinga wake wa shingoni ni mfano wa kumchokoza nyuki mzingani.
Bwaga wimbo
Maana yake ni kuanzisha au kuongoza wimbo. Msemo huu huwezeka kutumika katika sentinsi kama ifuatayao; mahadhi ya aliyeubwaga wimbo yalikuwa mazuri.
Anua majamvi
Maana ya msemo huu ni kutamatisha jambo au shughuli fulani uliyoanzisha. Pia kukunja jamvi ina maana sawa na kuanua majamvi. Kwa mfano, baada ya wanariadha kuanua majamvi yao, walirejea nchini.
Choma mkuki
Maana ya msemo huu ni ‘kufuma’ au ‘shambulia’ kwa kutumia mkuki. Kwa mfano, siku hizi vituko ni vyingi, aghalabu watoto wanawachoma mikuku wenzao kwa utesi wa mashamba.
Fanya ndaro
Neno ndaro linamaanisha sifa au sifu. Msemo huu unamaashisha kujisifu kwa jinsi mtu anavyozumgumza. Kwa mfanfo, ni vizuri uyaeleze yote uliyoyapitia bila ya kujifanyia ndaro na kumbe hamna lolote.
Fanya speksheni
Speksheni ni neno ambalo lina maana sawa na ukaguzi. Hivyo basi, msemo huu unamaanisha fanya ukaguzi au kagua. Kwa mfano, mkubwa wa kituo cha polisi hufanya speksheni ya nyumba zote za polisi kila jumapili.
Fanya udhia
Msemo huu unamaanisha kufanya usumbufu. Kwa mfano, hakudhamiria kufanya udhia kwa matamshi yake kwani aliyoyasema ni ya kweli.
Arusi ya mzofafa
Neno ‘mzofafa’ lina maana sawa na maringo au madaha. Arusi ya mzofafa ina maana sawa na arusi iliyonoga kwa mbwembwe na hoihoi. Kwa mfano, Bwana alituandalia arusi ya mzofafa hatutaisahau.
Kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa
Msemo huu una maana kuwa unapewa sifa usizostahili. Msemo mwingine ulio na maana sawa ni kuvalishwa kilemba cha ukoka.
Chezea unyango wa kima
Msemo huu huweza kutumika kuonya mtu dhidi ya jambo fulani. Kwa mfano, ” wewe, utakiona leo, nitakuchezesha unyago wa kima”. Inaaminika kuwa kima huacheza ngoma (Unyago) ili kuwatoa vigori (Wali). Tendo hili  hufantika kwa siri na endapo watagundua umewaona, lazma nawe uchezeshwe. Kwa hivyo, kuwa makini na mambo ya watu, usije ukachezeshwa unyago wa kima!
Bura yangu sibadili na rehani
Huu ni msemo ambao una maana lukuki, baadhi ya watu hutafsiri neno “bura’ kama kitu cha tunu kichakavu. Kwa hivyo msemaji wa msemo huu hunamaanisha kuwa hawezi badili kitu chake cha tunu kwa kipya.
Usiache “mbachao” kwa msala upitao
Katika msemo huu, wahenga wametumia neno “mbachao” linatamkwa “m-bachao,” yaani ni kifaa duni kinachotumiwa kufanyia ibada, Kwa mfano, mkeka au jamvi kuukuu (Kidukwa)..sasa wamesisitiza usije ukauacha kwa “Msala” upitao..msala nao ni sehemu ya kusalia lakini si duni kama ilivyo m-bachao. Pia, msemo huu un maana sawa na Usiyadharau madafu, maembe ni ya msimu.
Mwanya ni kilema pendwa
 Wengi hawafahamu kuwa hata kama mwanya ni kilema, lakini ni kilema kinachopendwa na wengi. Vilema vya aina hii hutambulika kama ‘vilema pendwa’, vipo vingi kwa uchache ni baadhi ya matege ya miguu, makalio makubwa, vifua, na misuli mikubwa.
Mungu hakupi kilema akakunyima mwendo
Msemu huu una maana kuwa mtu anapaswa kuridhika na alicho nacho. Funzo kuu ni kuwa haina haja kutamani vitu ambavyo vimepiku uwezo wetu.
Mlevi haukubali ulevi
Msemo huu una maana kuwa hata anywe vipi hakubali kuitwa mlevi. Msemo hu umewalenga mahasidi na mafisadi ambao hukataa chungu ya ukweli.
Chongo kwa mnyamwezi kwa mswahili amri ya mungu
Wengne hutumia neno ‘chogo’ badala ya ‘chongo’, yote kheri alimradi haipotosha maana ya usemi huu.
Ushikwapo shikamana, si wengi wa kupendana
Maana ya msemo huu ni, endapo atatokea mtu akakupenda na akaomba muwe marafiki usikatae, kwani hapa ulimwenguni watu wachache sana wanaopendana.
Maji! Ni kumbwe na kinyweo, matupu yasonga moyo
 Maana ya msemo huu ni kuwa, kunywa maji pekee bila ya kula chakula yaweza kusumbua tumbo. Ni vema upatapo mgeni umpe chakula kwanza halafu ndo umpe maji. Ni vizuri uelewe kuwa msemo huu unaweza kuwa na maana tofauti tofauti kulingana na muktadha uliotumika.
Akomelepo mwenyeji na mgeni koma papo
Msemo huu wa kiswahili una maana kwamba mgeni anapaswa fuatisha mipaka ya mwenyeji wake. Endapo atakushawish jambo fulani,usipinge.
Pema usijapo pema, ukipema si pema tena
Kaana ya msemo huu ni kuwa, mahala popote huwa pazuri endapo hujawahi kwenda. Ukishaenda mara kwa mara uzuri wake huisha. Hutumika kuonya mtu dhidi ya kuzoea jambo fulani kwa uzuri wake kwa sababu anaweza kuzoea ule uziri na pindi ukipotea hatakuwa na sababu ya kulipenda jambo hilo.
Mwanaharamu hata umtie kwenye chupa atatoa japo kidole ili ajulikane kama yupo
Msemo huu unamlenga mtu aliye na tabia mbaya. Maana yake ni kuwa, popote aendapo lazma atataka mtambue uwepo wake.
Afugae ng’ombe tume, mwenye ziwa la kujaza
Usemi huu una maana kuwa, fanya kazi kwa bidii na utafaidi matunda ya kazi ya mikono yako. Msemo mwinigine ulio na maana sawa ni ‘mwenye kisu kikali ndiye ataekula nyama.’
Usione ukadhani
Huu ni msemo ambao nafahamika na wengi. Una maana kuwa, usije liona jambo na ukaridhika na tafsiri ya awali. unapaswa ulichunguze kwa makini ili upate uthibitisho wake pengine lina maana tofauti. Msemo huu unatufunza umuhimu wa kuhakiki jambo fulani ili kuhepuka tafsiri hasi.
Punda afe mzigo wa bwana ufike
Msemo huu hautushawishi kuua punda ili kufikisha mzingo. Una maanana kuwa, weka lengo la kutimiza wajibu wako. Labda kutakuwa na vizuizi katika kutimiza wajibu, lakini ili kulinda hadhi na cheo chako iwe kazini au popote pale ulipopewa wadhifa,jitahidi utimize wajibu wako kwa gharama yoyote.
Usimlaumu mungu kwa kumuumba chui, mshukuru hakumpa mbawa
Maana kuu ya msemo huu ni kwamba, unapaswa kumshukuru mungu kwa hicho mungu alichokujaalia, wala usikosoe uumbaji wake. Funzo kuu kutokana na msemo huu ni kuwa mungu huumba au hutoa kwa makadirio maalum, hazidishi wala hapunguzi. Hebu fikiria kama chui andegukuwa na mabawa tungekuwa wapi.
Maji ya kifuu bahari ya chungu
Msemo huu una maana kuwa jambo dogo unalolidharau wewe, wenzako linawatoa jasho. (maji ya nazi mdudu chungu/sisimizi kwake sawa na bahari).
Mgala mwue na haki yake umpe
Maana  ya musemo huu ni kuwa, Hata kama umeamua kumkandamiza mtu kwa kumfanyisha kazi ngumu ama malipo duni, mtimizie ulichomwahidi ama iliyo haki yake.
Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
Msemo huu unatufunza kwamba kuwasaidia wengine si kuonyesha utajiri mtu alionao bali ni ishara ya upendo na kujali maslahi ya wengine.
Bure huchosha
Msemo huu unadhamiria kutufunza kuwa si vizuri kuzoea kupenda kupokea vitu bila kufanya kazi. Tabia hii ya kupokea tu hukwaza wanaotupa, ama labda wao wakatusema vibaya na kutukera.
Ampaye shetani maana,hujipatisha ghadhabu za Rahamani
Msemo huu unamaanisha kuwa anayemsifu shetani au mtu mwovu humchukiza Muumba na kujiletea adhabu. Msemo huu unatuonya kama wanajimii dhidi ya kuwapa watu waovu sifa nzuri.
Bahati yenda kwa wawi wema wakalia ngoa
Maana ya msemo huu ni kuwa bahati ikiwaendea watu waovu, wema huwewaonea wivu iweje wamebahatika? Husistaajabishwe na hayo kwani bahati haibagui.
Akuchukiaye hakosi hila ya kukutia
Maana ya msemo huu ni kuwa, mtu asiyekupenda anaweza kukuzushia mabaya ilimradi tu, akuchafue, akuharibie sifa zako, au mambo yako.
Waja kufa na laiti na vyanda kinywani
Msemo huu unatufunza kuwa tusipozingatia ushauri ama makanyo tutaishia tukifikwa na mabaya na tujutie kutoyazingatia.
Afichaye ugonjwa hufichuliwa na kilio
Funzo kuu katika msemo huu ni kuwa anayefanya siri matatizo yake huumbuka pale yanapomzidi ama kumgharimu hadi kuonekana.
Utatumiaje mchuzi nyama usile
Msemo huu unawalenga watu ambao wnapenda kujinufaisha na mali ya watu wengine ilhali hawataki kuhusishwa na wao. Maana ya msemo huu ni iweje wamkataa mtu ilhali unajinufaisha na vilivyo vyake?
Hutendwaje ikafana shubiri ikawa tamu?
Msemo huu unatufunza kuwa haiwezekani mtu kubadili jambo hata likawa kinyume na lillivyoumbwa au linavyofahamika.
Midundo ikibadilika ngoma huchezwa vingine
Maana kuu ya msemo huu ni kuwa, mabadiliko yanapotokea katika mazingira yako, huna budi kubadili mbinu ili kukabiliana na mabadiliko hayo. Funzo kuu ni kuwa wanajamii wanapaswa kukubali mabadiliko badala ya kulalamika.
Bata mtaga mayai usichinje kwa tamaa ya wingi
Msemo huu una funzo nzuri sana kwa wanajamii. Maana yake ni kuwa tamaa za haraka za kukifaidi kitu zisituponze tukaharibu manufaa makubwa zaidi ya kitu hicho hapo baadae.
Samaki mkunje angali mbichi
Msemo huu ni muhimu sana katika jamii yetu. Unatufunza kwamba ni vinzuri kuwaonya watoto wetu tangu utotoni mwao ili kwafanya waelewe mambo na kujirekebisha kwa urahisi.
Bahati ikibisha hodi sharti ufungue mlango mwenyewe
Msemo huu unamaanisha kuwa unapopata fursa ama nafasi ya kutenda jambo yakupasa uitumie vema na si kuipuuzia au kukata usaidiwe kuipokea. Kwa hivyo, ni vyema wanajamii wajifunze kutumia fursa tofauti tofauti kama inavyohitajika.
Kipenda roho hula nyama mbichi
Msemo huu una maana kuwa, mtu hujitosa hata kuyatenda mambo yasiyo ya kawaida au magumu bora apate anachokipenda.
Dunia tambara bovu ukivuta utachana
Msemo huu untuonya dhidi ya kuwaamini sana wanadamu. Maana yake ni kuwa, usiwaamini sana walimwengu au  kuwategemea sana kwani wanaweza kukutenda.
Cha mchama huchama cha mgura hugura
Msemo huu una maana kuwa asiyekuwepo kulinda mali yake au kutunza mali yake huishia kutumiwa vibaya ama kumalizwa na wengine ambao labda hawana.
Akopaye akilipa huondokana na lawama
Huu ni msemo ambao una funzo nzuri sana kwa wanajamii. Una maana kuwa anyekopa akilipa hujiondolea lawama. Kwa hivyo, ni wajibu wate kuhakikisha tumeiondolea lawama kwa kulipa madeni yote yanayotukabili.
Achezaye na tope humrukia
Msemo huu una maana kuwa unaposhiriki kutenda uovu si ajabu mabaya hayo yakakudhuru mwenyewe. Kwa hivyo, msemo huu unatuonya dhidi ya kushiki katika kutenda uovu.
Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba
Pemba ni mji fulani wa pwani na waswahili wanoishi huko huvalia vilemba. Msemo huu una maana kuwa watu a tabia moja hujuana kwa mambo wanyofanya.
Lenye mwanzo lina mwisho
Msemo huu unamaanisha kuwa jambo lolote lililo na mwanzo lina mwiso. Msemo huu una maana sawa na hakuna ndefu lisilokuwa na mwiaso.
Zunguo la mtukutu ni ufito
Msemo huu unatufunza kuwa njia ya kumfunza mtoto mkaidi ama asiyesikiliza ni kumpa adhabu.
Maji usiyoyafika hujui kina chake
Msemo huu unamaanisha kwamba jambo ambalo hujalifanya hujui ugumu wake. Pia, msemo huu una maaana sawa na kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
Ukiwaona ni watu moyoni hawana utu
Msemo huu unamaanisha kuwa usifikiri kwamba kila uliyekuwa karibu naye anakupenda kwa dhati wengine ndio maadui zako namba moja na ni vigumu kuwatambua.
Afadhali jirani mbuge kuliko jirani mwenye mdomo mrefu
Msemo huu una maana kuwa mtu anayefitini wengine ni hatari kuliko hata mlafi.
Misemo ni muhimu sana katika jamii. Kwanza, ni njia ya kupitisha mafunzo kutoka kazazi kimaja hadi kingine. Pia, misemo huwafunza wanajamii kuhusu utamanduni wao, ni njia ya kujiburudisha na pia hutumika kuonya au kushauri.
Kwa hivyo, ni vyema wanajamii kuitumia misemo kila siku kwani itawajenga kielimu na pia kimaadili.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 2 Guest(s)