MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
TAMTHILIYA YA BIBI TITI MOHAMED NA PROF. EMMANUEL MBOGO

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
TAMTHILIYA YA BIBI TITI MOHAMED NA PROF. EMMANUEL MBOGO
#1
Tamthiliya hii inahusu Bibi Titi Mohamed. Titi alikuwa kiongozi shupavu aliyeupipgania uhuru wa Tanganyika kwa ujasiri mkubwa akiwa mwanachama wa TANU na kiongozi wa Umoja wa Wanawake. Wakati wanaume wengi walipokuwa wakiogopa kukata kadi za TANU, wakhofia kufukuzwa kazi na mkoloni, Titi aliwahamasisha wanawake kote nchini kuupigania uhuru wa Tanganyika
Kitabu kinaanza mwaka wa 1970 kwa kumuonesha Bi. Titi akiwa Gereza la Isanga Dodoma, moja ya magereza magumu Tanzania. Kabla yake mwaka wa 1953 mwanasiasa mkubwa sana Tanganyika sehemu za Maziwa Makuu, Ali Migeyo alifungwa gereza hilo na Waingereza kwa kosa la kufanya mkutano wa siasa Kamachumu bila idhini ya serikali. Miaka 17 baadae mpigania uhuru Bi. Titi yuko kifungoni kwa kuhusika na kesi ya uhaini kutaka kuiangusha serikali aliyoipigania wakati wa kudai uhuru.
Akiwa hapo gerezani Bi. Titi anaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na anaeleza ushirikiano wake na Nyerere wakati wakiwa katika ofisi ya TANU New Street. Bi. Titi anaeleza katika mswada wake, anaoandika jela vipi yeye na wenzake walipita mtaa kwa mtaa kueneza TANU.
Kitu cha ajabu Gereza la Isanga wanamuomba Bi. Titi watumie historia yeke ile kufanya onyesho la historia ya uhuru wa Tanganyika.
[Image: UaCj2HX7kWcRvzy3Az5CTtgufV1I1FtGPvbT8Xwd...46-h659-no]
Bi. Titi akiwa katika moja ya matawi ya TANU Dar es Salaam tawi hili lilikuwa Magomeni Mapipa nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu 1955
[Image: tTRTeOOZOOEnRd4Z5Se7kCkFQvldNUen4fJjA6Ja...77-h659-no]
[Image: 1SoH8DK4E3Rp_beqWUyYroAl-85hb9m-PN4bznGL...70-h526-no]
Picha ya Mwandishi aliyopiga Viwanja Vya Mnazi Mmoja mwaka wa 1966 nyuma yake ni barabara iliyokuja kujulikana baadae kama Titi Street kwa kumuenzi Bi, Titi Mohamed na ukivuka barabara hiyo linaloonekana ni Soko la Kisutu maarufu kama ”Soko Mjinga.”
Tamthilia hii ya Bi. Titi Mohamed ni kazi ya kupigiwa mfano kwani naamini hii ni tamthilia ya kwanza ambayo imejaribu kuhadithia historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwataja wale ambao waliupigania uhuru wa Tanganyika. Kurasa za mwanzo Mwandishi anamleta Schneider Plantan akizungumza na Boi Selemani kuhusu TANU.
Bwana Boi akimlalamikia Schneider kuwa mkewe Bi. Titi hatulii nyumbani kwa ajili ya shughuli za TANU kiasi imekuwa yeye ndiyo mfuaji wa nguo zake na mpishi wa chakula chake.
Boi Selemani alikuwa dereva wa taxi.
Schneider yeye ana historia ndefu katika siasa za Tanganyika. Yeye ndiye aliyesimama kidete kuwaleta vijana wasomi katika TAA ili kuwaondoa wazee waliokuwa wamechoka na kuifanya TAA isifanye siasa za maana kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika.
Hii ilikuwa mwaka wa 1950.
Sasa TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka wa 1954 Schneider ndiye aliyemleta Bi. Titi katika TANU pamoja na wenzake akina Tatu Bint Mzee na wanawake wengine kuja kukipa nguvu chama.
Tamthilia inaanza mwaka wa 1955 wakati Bi. Titi na wenzake wako katika hekaheka ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU na wakati huo ndiyo safari ya Julius Nyerere kwenda UNO inatayarishwa.
Boi katika mazungumzao yake na Schneider anatabiri kuvunjika kwa ndoa yake na mkewe Bi. Titi kwa ajili ya TANU na anamtupia lawama zote rafiki yake Schneider Plantan kwa kumpeleka mkewe TANU.
Boi analalamika hadi kufikia kusema, ”Titi mwanamke wa Kiislam. Kasoma madrasa….Bibi Titi kapanda jukwaani…hana baibui…”
[Image: Z6-fQpBJ-lRfA2xmvcOGq9RAPspFuBFrJ_17576x...79-h659-no]
Bi Titi Mohamed na Julius Nyerere wakihutubia wananchi Uwanja wa Jangwani 1955
[Image: Jk3j6Mf4o1KdhJppiFYzyOyBfPfECav6eFwMT5Ib...91-h659-no]
Kulia ni Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere na nyuma ya Nyerere ni Maria
Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia
Kitabu hiki, ”Malkia Bibi Titi Mohamed,” ukikianza hukiweki chini hadi umekimaliza.
Mwl Maeda
Reply
#2
kwakeli nimefarijika nayo, inanikumbusha nadharia ya UFEMINISTI
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)