Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: HISIA ZANGU
#1
HISIA ZANGU
Nilijaribu kuficha, niwe Kama simpendi,
Moyo unanichokocha, kumpata yule fundi,
Naona huku kuficha, kunanifanya siwandi,
Natangaza nampenda,  mpeni habari hizi.

Hisia zanifumuka, moyoni kunikeketa,
Ni yule ninamtaka, mwambe aache matata,
Ninamtaka haraka, tafurahi kumpata,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Ninaomba samahani, kiwa nimevunja mwiko,
Kwa wetu utamaduni, niendako mie siko,
Sema nampenda Nani, inazua chokochoko,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Mkisema naigiza, eti tulivyo malenga,
Bure mtanipoteza, mniue mie Sanga,
Leo ninamtangaza, nimepagawa mkinga,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Kwanza nimependa ndevu, sharubu nazo sharafa,
Na macho yake makavu, yaniletea maafa,
Mwambieni Nina wivu, kumkosa nitakufa,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Si mweusi si mweupe, bwana yupo katikati,
Kijana Hana mapepe, Wala Hana hatihati,
Mwambieni hata lepe, siku hizi silipati,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Ni mrefu wa kadiri, si mnene si mwembamba,
Kumpata ni fahari, mtaani nitatamba,
Nimemuomba Kahari, ake kwangu huyu mwamba,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Siendelezi kutunga, nimeanza kumuwaza,
Machozi yananilenga, namlilia Hamza,
Amini akinitenga, binti mtanipoteza,
Natangaza nampenda, mpeni habari hizi.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama b
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply
#2
Hongera sana kwa utungo mzuri.

Hakika wewe ni mtaalam
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)