Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHADI'

Neno ahadi katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: i-/-zi] mwisho wa uhai wa kiumbe aghalabu mwanadamu; mauti.

2 - Nomino: [Ngeli: i-/-zi] makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande mbili au zaidi.

3 - Nomino: [Ngeli: i-/-zi] hakikisho la utekelezaji wa jambo ambalo mtu au watu hujipa jukumu la kutimiza.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ahadi( soma: ahdun/ahdan/ahdin عهد ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Ahadi : tendo-jina kutokana na kitenzi cha Kiarabu ahida عهد ameahidi.

2. Utekelezaji wa jambo fulani.

3. Dhamana.

4. Amani.

5. Mapenzi.

6. Dhima.

7. Azimio; makubaliano.

8. Wasia/wosia, usia.

9. Kiapo.

10. Andiko la uhawilishaji wa madaraka.

11. Zama/wakati, ahdush shabaabi عهد الشباب wakati wa ujana.

12. Mrithi wa ufalme, ikitanguliwa na neno waliyuu, waliyyul Ahdi ولي العهد.

13 -  Agano la Kale, likiambatana na neno Al-Qadiim, Al-Ahdul Qadiim العهد القديم، maandiko matakatifu kabla ya ujio wa Masihi Issa Mwana wa Maryam (Yesu Kristo).

14 -  Agano la Jipya, likiambatana na neno Al-Jadiid, Al-Ahdul Jadiid العهد الجديد، maandiko matakatifu yanayohusu wakati wa Masihi Issa Mwana wa Maryam (Yesu).

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahadi ( soma: ahdun/ahdan/ahdin عهد ) lilipoingia katika  Kiswahili lilichukua baadhi ya maana zake katika lugha ya asili- Kiarabu na kuacha maana zingine.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)