Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'SINTOFAHAMU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SINTOFAHAMU'.

Neno sintofahamu katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] hali ya kutatanisha impatayo mtu ya kushindwa kuelewa afuate lipi au aache lipi; mtanziko.

2. Nomino: [Ngeli: i-/zi-] hali ya kutofahamiana, hali ya kutoelewana

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili sintofahamu halina mfano wake.
Kisemantiki, neno hili sintofahamu katika lugha ya Kiarabu ni maneno mawili yaliyowekwa pamoja  suui na tafaahamu na kupata suui-tafaahamu  سوء تفاهم (kutoelewana, kufahamiana ndivyo sivyo kwa kila mmoja kufahamu kinyume na ilivyokusudiwa).

Katika lugha ya Kiarabu neno suui maana yake ni ubaya/-baya na neno tafaahamu lina maana zifuatazo:

1. Maelewano, mwafaka.

2. (Likianza neno suui) na kuwa  Suui Tafaahamu maana yake ni kulifasiri jambo au kitendo au kauli kinyume na uhalisi wake hivyo kuleta kutoelewana.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno haya mawili suui tafaahamu  yaliipoingia katika Kiswahili na kutoholewa,  neno jipya la Kiswahili sintofahamu lilipatikana.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)