Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
BAINA YA "KUA" na "KUWA
#1
BAINA YA "KUA" na "KUWA"

Assalaamu alaykum tena, Prof. Abdulaziz Lodhi.  Katika maoni yako uliyoniandikia kuhusu "wimbo" na "nyimbo" ulinieleza kwamba "...baadhi ya wasemaji wa jadi wa Kiswahili hawatafautishi baina ya vitenzi vya 'ku-kua' na 'ku-wa'. Badala ya kuandika k.m. 'Alikuwa amelala wanaandika 'Alikua amelala' ".

Kama tujuavyo, katika kanuni za uandishi za Kiswahili Sanifu, maneno haya mawili huendelezwa kwa namna mbili tafauti ili kutafautisha maana zake. Kwa hivyo, "kua" likawa na maana ya _grow_ na "kuwa" likawa na maana ya _to be_. Lakini wasanifishaji hao walioyawekea kanuni hiyo maneno hayo hapo mwaka 1930, hawakuifuata kanuni yao hiyo katika maneno mengine ili kutafautisha maana zake. Kwa mfano, katika Kiswahili Sanifu  kwaandikwa "ua" kwa maana ya _kill_, _flower_ na _fence_; au "jua" kwa maana ya _know_ na _sun_; au "pua" kwa maana ya _nose_ na aina ya madini ya chuma.

Lakini tukitizama jinsi maneno hayo (kwa maana zake zote) yalivyokuwa yakiandikwa na Waswahili wenyewe kwa harufu za Kiarabu, kabla ya Kiswahili kuandikwa kwa hizi harufu za Kilatini, tutaona yalikuwa yakiandikwa hivi: "kuwa" (كُوَ), "uwa" (اُوَ), "juwa" (جُوَ), na "puwa" (پُوَ). Kwa ufupi, maneno yote kama hayo yalikuwa yakimalizika kwa -*wa* (وَ) na hayakuwa yakimalizika kwa -*a* (اَ) pekee. Mtu aweza kuyaona haya akizitizama nyaraka za kale, au hata  za hivi karibuni, zilizoandikwa kwa harufu hizo.

Kuhusu hayo maneno mengine uliyoyataja yanavyoandikwa leo katika Kiswahili Sanifu, nakuletea haya maoni yangu hapa chini?niliyoyaandika zaidi ya mwaka mmoja unusu uliopita kulijibu swali nililoulizwa kwenye kikundi kimojawapo cha Kiswahili cha WhatsApp.

Wassalaamu alaykum.

-Abdilatif Abdalla,
2.1.2022,
London
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)