MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO ' AFYA' 'AFUA' NA 'AFUWA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO ' AFYA' 'AFUA' NA 'AFUWA
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' AFYA' 'AFUA' NA 'AFUWA'

Neno afya katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: -i/-zi] ukamilifu na usahihi wa utendaji wa viungo vyote vya mwili na akili na ustahifu wa kijamii sawa.

Kuna methali: Afya ni bora kuliko mali.

Kuna msemo : Buheri wa afya: Afya nzuri.

2. Kihisishi: Neno linaloonesha utayari wa watu katika kufanya jambo aghalabu hutumiwa na watoto.
Mfano: Afya! Twendeni tukaangue mapera!

3. Neno linalotumiwa kumuombea uzima mtu aghalabu mtoto baada ya kupiga chafya.

Kuna msemo: Kua mwanangu kama mgomba, mnazi unachelewa (unakawia).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili afya (soma: aafiyatun/aafiyatan/aafiyatin عافية) ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Kinga; Tiba, Masdar (Tendo-Jina) kwa kitenzi cha Kiarabu aafaa عافى (amemkinga na shari/ubaya, amemtibia maradhi yake).

2. Siha/Swiha timilifu.

3. Wageni.

4. Watafutaji riziki (wanaadamu na wanyama).

5. Wafanyao wema, hisani.

Neno afuwa[ Ngeli: i-/i-] katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya: 'hali ya kumsamehe mtu au kumwia radhi kutokana na kosa alilolitenda.

Na neno afua katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino : [ Ngeli: i-/zi-] uamuzi unaoweza kufanywa; chaguo.

2. Kitenzi elekezi : Afu.a hali aghalabu ya Mwenyeezi Mungu kumwepusha mtu na madhara ambayo yangeweza kumpata.

Mfano: Usihofu, Mwenyeezi Mungu atakupa afua.

3. Nomino: [ Ngeli: i-/i-] hiari au kudra ya Mwenyeezi Mungu aliyonayo kwa mja wake anapokabiliwa na hatari.

Kuna msemo: Afua ni mbili, kufa au kupona.

Katika lugha ya Kiarabu maneno ' afua ' na ' afuwa ' yametokana na neno la Kiarabu afwu عفو ( soma: afwun/afwan/afwin عفو) lenye maana zifuatazo:

1. Nomino : Msamaha/Kusamehe, Masdar Tendo-Jina la kitenzi cha Kiarabu afaa عفا (amesamehe).

2. Nomino : Msamaha; kuacha kuadhibu.

3. Nomino : Wema, tendo jema.

4. Nomino : Ziada, kilichozidi.

5. Nomino/Kivumishi: -enye ubora.

6. Nomino: Ardhi ambayo haijakanyagwa na wayo wowote.

7. Mtoto wa punda.

Kinachodhihiri ni kuwa wakati maneno haya afya , afuwa na afua  yalipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  mbali ya kuchukua sehemu ya maana za lugha asili - Kiarabu, yalibeba dhana nyingine katika Kiswahili.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)