MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO ' JAALA', 'JALIA' 'JALI.A/JAALI.A' na 'MAJALIWA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO ' JAALA', 'JALIA' 'JALI.A/JAALI.A' na 'MAJALIWA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' JAALA', 'JALIA' 'JALI.A/JAALI.A' na 'MAJALIWA'

Neno jaala[ Ngeli: i-/i-] katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya' mambo yafanyikayo kwa mapenzi/uwezo wa Mwenyezi Mungu'.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili jaala (soma: ja-a-la جعل) ni kitenzi cha Kiarabu chenye maana zifuatazo:

1. Amefanya kitu fulani kiwepo.

2. Ametoa kitu kumpa mtu mwengine.

3. Ameanza jambo fulani.

4. (Kwa Mwenyeezi Mungu tu) Ameumba.

5. Ametengeneza.

Neno jalia[ Ngeli: a-] katika lugha ya Kiswahili ni kisawe cha neno jalali [ Ngeli: a-]  lenye maana ya 'jina la kumtaja Mwenyeezi  Mungu kwa sifa yake ya kuwa utukufu mwingi'.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili jalali (soma: jalaalun/jalaalan/jalaalin جلال) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Utukufu. Mwenyeezi Mungu hutajwa kuwa Dhul Jalaali  ذو الجلال mwenye utukufu.

2. -enye cheo/hadhi kubwa.

3. Kilicho kikubwa zaidi.

Maneno jali.a/jaali.a[ Vitenzi Elekezi ] katika lugha ya Kiswahili vina maana ya 'fanya uwezekano, saidia, wezesha: Mwenyeezi Mungu akitujalia/akitujaalia uhai tutaonana.

Neno hili linaponyambuliwa tunapata vitenzi: jaalika, jaalisha na jaaliwa.

Neno majaliwa[ Ngeli: ya-/ya-] katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya' mambo yafanyikayo kwa uwezo/mapenzi ya Mwenyezi Mungu'.

Maneno ' jaala ' na ' majaliwa ' ni visawe.

Neno ' majaliwa ' halina mfano wake kimatamshi katika lugha ya Kiarabu bali yumkini limebuniwa kutokana na nomino ' jaala ' au kitenzi ' jaalia/jaaliwa'.

Kitenzi ' jali.a/jaali.a' kinamhusu Mwenyeezi  Mungu tu kwa maana ya kumpa mtu uwezo wa kupata au kuweza kufanya jambo fulani.

Kinachodhihiri ni kuwa neno jaala ( soma: ja-a-la  جعل) ambalo ni kitenzi katika lugha ya Kiarabu lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno jaala limekuwa nomino kwa maana ya 'mambo yafanyikayo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu'.
Kiujumla, maneno yote haya hayakuepukana na maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)