12-23-2021, 11:29 AM
MAZAWA YA KILA MWAKA
Mazawa ya kila mwaka, leo azaliwa tena
Tarehe imeshafika, Rais mumemuona
Khatamu ameishika, na nchi inapambana
Tena imesalimika, ipo tuli sasa mbona.
Ya Rabbi Mola Karimu, mtoa na kuondoa
Nanyanyua kwa Nidhamu, mikono kuomba dua
Kwani imenilazimu, leo kwako kukujia,
Mpe wetu Muadhamu, kila jema la dunia.
Mpe anachokitaka, wepesi umfanyiye
Mpe tena kwa haraka, moyoni asiumiye
Mpe pasi na mashaka, na siye tufurahiye
Mpe mema kwa hakika, nchi aisimamiye.
Kheri pasi na mipaka, baraka mmiminiye
Neema zipate fika, na maisha yatuliye
Na watuwe kuridhika, daima washukuriye
Lije hilo kila mwaka, Ya Rabbi muhurumiye.
Furaha apate cheka, afya usimnyime
Imara kuimarika, mahiri na asimame
Na bila kutikatika, mambo yetu yasikwame
Naomba kwako Rabbuka, mtu wetu mtazame.
Ben Othman
Zanzibar
Happy birthday Mr president.
Mazawa ya kila mwaka, leo azaliwa tena
Tarehe imeshafika, Rais mumemuona
Khatamu ameishika, na nchi inapambana
Tena imesalimika, ipo tuli sasa mbona.
Ya Rabbi Mola Karimu, mtoa na kuondoa
Nanyanyua kwa Nidhamu, mikono kuomba dua
Kwani imenilazimu, leo kwako kukujia,
Mpe wetu Muadhamu, kila jema la dunia.
Mpe anachokitaka, wepesi umfanyiye
Mpe tena kwa haraka, moyoni asiumiye
Mpe pasi na mashaka, na siye tufurahiye
Mpe mema kwa hakika, nchi aisimamiye.
Kheri pasi na mipaka, baraka mmiminiye
Neema zipate fika, na maisha yatuliye
Na watuwe kuridhika, daima washukuriye
Lije hilo kila mwaka, Ya Rabbi muhurumiye.
Furaha apate cheka, afya usimnyime
Imara kuimarika, mahiri na asimame
Na bila kutikatika, mambo yetu yasikwame
Naomba kwako Rabbuka, mtu wetu mtazame.
Ben Othman
Zanzibar
Happy birthday Mr president.
Mwl Maeda