MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' FADHAA' na 'FAZAA'

Neno *fadhaa* katika lugha ya Kiswahili (kwa mujibu wa Kamusi Kuu ya Kiswahili Sanifu na Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21) lina maana zifuatazo:

1. *Nomino* : Kosa utulivu wa moyo kutokana na jambo fulani ambalo ama umefanyiwa wewe au umemfanyia mtu mwengine ambalo aghalabu huwa si jema.

2. *Nomino:* Hali ya wasiwasi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *fadhaa* (soma: *fadhaun/fadha-an/fadhain فذع* ) ni nomino yenye maana ya ' *jeuri* '.

Ama neno *fazaa* ambalo ni mashuhuri uswahilini na ambalo linachukuliwa kuwa kisawe cha neno *fadhaa* , katika lugha ya Kiarabu ni nomino inayotokana na kitenzi *faza.a/fazi.a* *فزع* ambacho kina maana zifuatazo:

1. *Faza.a فزع* amefazaika/amefadhaika.

2. *Faza.a ilayhi فزع إليه* ameomba hifadhi/amemba msaada.

3. *Faza.aahu  فزعه*  amemnusuru/amemsaidia.

4. *Faza.a min nawmihi فزع من نومه* ameamka kutoka usingizini.

Hiyo nomino *fazaa فزع* katika lugha ya Kiarabu ina maana zifuatazo:

1. Khofu/hofu na wasiwasi.

2. Kuomba hifadhi/ukimbizi.

3. Kuomba msaada.

Kinachodhihiri ni kuwa wataalamu wetu wamelichukua kutoka Kiarabu neno *fadhaa فذع* lenye maana ya ' *ujeuri* ' wakalipa maana ya neno la Kiarabu *fazaa فزع* lenye maana ya khofu/hofu na wasiwasi.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)