MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO ' SHEHE'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO ' SHEHE'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' SHEHE'.

Neno Shehe katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mtu mwenye kiwango cha juu cha mafunzo ya Dini ya Kiislamu ambaye pia huwa na jukumu la kuwafundisha wengine.

2. Mtu mzima aghalabu mzee ambaye jamii inampa heshima kubwa kutokana na hekima na busara zake. 

3. Ubingwa au uhodari wa hali ya juu.

Neno hili shehe ndilo lililisanifiwa na kusajiliwa rasmi katika Kamusi Kuu ya Kiswahili na ile Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21 ingawa wazungumzaji wa Kiswahili hususan Pwani hutumia maneno Shekhe, Sheikh na Shaykh.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili shehe ( soma: shaykhun/shaykhan/shaykhin شيخ ) lina maana zifuatazo:

1. Mtu aliyefikia umri wa miaka 50 na kuendelea.

2. Mwanachuoni/Mwanazuoni; Mtu mwenye kiwango kikubwa cha elimu.

3. Mwalimu yeyote yule.

4. Mkuu wa familia/ukoo/kabila/kundi la watu.

5. Mtu mwenye hadhi katika kundi au jamii fulani.

6. Mkuu wa kiroho kwa Dini ya Druze (Wadruzi (kwa Kiarabu: درزي) ni watu wenye asili ya Mashariki ya Kati wanaofuata dini yao maalumu inayohusiana na Uislamu, Uyahudi na Ukristo lakini inategemea zaidi falsafa, ikimuheshimu Plato, Aristotle, Socrates na Akhenaten.) na huitwa Shaykhul Aqli .

7. Mume wa mtu na huitwa shaykhul Mar-a/ Shaykhu ...... (Mume wa mwanamke/ mume wa .....)

8.Ibilisi na huitwa shaykhun Naari (Mzee wa Motoni).

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( shaykh شيخ  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa shehe maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - zinazohusu ujuzi wa Taaluma za Dini ya Kiislamu na umri  mkubwa wa miaka 50 na zaidi hazikubadilika.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)