MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO ' USTADHI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO ' USTADHI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' USTADHI'

Neno Ustadhi katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mtu mwenye kiwango kikubwa cha elimu.

2. Mtu mwenye maarifa au ujuzi wa kufundisha.

3. Ubingwa au uhodari wa hali ya juu.

4. Jina la heshima la mahiri, mtungaji wa nyimbo, mwimbaji, mpigaji muziki (ala/vyombo) za/vya muziki na kadhalika.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ustadhi ( ustaadhun/ustaadhan/ustaadhin استاذ) lina maana zifuatazo:

1. Mwalimu (yeyote yule).

2. Rais/Kiongozi.

3. Mwanachuoni/Mwanazuoni; Mtu mwenye kiwango kikubwa cha elimu.

4. Mtu mahiri katika elimu au ujuzi fulani anayewafundisha wengine.

5. Hadhi ya kiakademia katika ndaki/vyuo vikuu; Profesa.

Ingawa Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21 zimesajili kuwa etimolojia ya neno hili *(ustadhi)*  ni *Kiarabu*, ukweli ni kwamba hili *si neno la asili la Kiarabu* bali ni neno la kiajemi *(kifursi)* limeingia katika lugha ya Kiarabu karne ya 13 wakati wa Utawala/ Ufalme wa Uthmaaniyyah (Ottoman Empire).
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *ustadhi* *أستاذ*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)