MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO ' ALFAJIRI' NA ASUBUHI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO ' ALFAJIRI' NA ASUBUHI
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ALFAJIRI' NA ASUBUHI

Neno Alfajiri katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mwanzo wa muda wa kupambazuka kwa anga katika siku, ambao hudumu kuanzia saa kumi na moja na kabla ya kuchomoza kwa Jua.

2. Muda mfupi kabla ya Jua kuchomoza.

3. Mwanzo wa kitu fulani.

4. Swala inayoswaliwa na Waislamu kati ya saa kumi na moja  na kabla ya kuchomoza kwa jua.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili alfajiri ( **fajrun Al-fajr* *فجر/الفجر* ) lina maana zifuatazo:

1. Mwanga wa asubuhi au mawio.

2. Ukarimu au kipawa.

3. Umaarufu.

4. Mali au ukwasi.

5. Hali ya kuondoka kwa kiza cha usiku na kutawala weupe wa asubuhi yaani kupambazuka.

Na neno Asubuhi katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Muda uliopo baada ya alfajiri na kabla ya mchana.

2. Wakati,kati ya kuchomoza kwa jua na kabla ya kuanza adhuhuri.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *asubuhi* ( **subhun/Al-Subhu (soma: As-Subhu* *صبح/ الصبح* ) lina maana zifuatazo:

1. Pambazuko la asubuhi; mawio.

2. Moja kati ya Swala Tano za faradhi kwa Waislamu ambayo huswaliwa kati ya kuchomoza kwa Alfajiri na kuchomoza kwa jua.

Ni dhahiri kuwa, maneno haya yalipoingia katika Kiswahili yalijikita na yale yaliyo mashuhuri katika maisha ya Waswahili nayo ni: wakati na Swala na kuacha maana nyingine katika lugha ya asili - Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)