MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO ' MRABAHA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO ' MRABAHA
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MRABAHA'

Neno Mrabaha (wingi: Mirabaha) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Kiasi kinacholipwa na mchapishaji kwa mtunzi wa kitabu kwa kipindi fulani kutokana na mauzo ya kitabu husika.

2. Faida inayopatikana kutokana na biashara fulani.

3. Ushuru anaotozwa  mfanyabishara au mwekezaji na mtu aliyemkodisha eneo au mtaji.

4. Malipo yanayotolewa na mfanyabiashara kwa mtu aliyempa mali au mtaji wa biashara.   

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili mrabaha ( muraabahatun مرابحة) lina maana zifuatazo:

1. Jumla ya rasilimali na ziada maalumu (faida).

2. Kumpa mtu mtaji ili aufanyie biashara kwa makubaliano ya kugawa faida kwa namna mliyokubaliana.

3. Biashara inayolenga kupata faida fulani.

Katika Sarufi ya Kiarabu neno (nomino) muraabahat مرابحة linatokana na kitenzi cha Kiarabu raabaha رابح (amefanya la kumletea faida) na jengo la kitenzi hiki linaashiria kitendo kilichofanywa kwa ushirikiano wa watu wawili au zaidi (mushaarakah).

Utaona kwamba neno hili lilipoingia katika lugha ya Kiswahili halikuiacha ile maana ya lugha yake ya asili nayo ni kufanya muamala kwa lengo la kupata faida.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)