MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' STAHILI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' STAHILI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' STAHILI'.

Stahili katika lugha ya Kiswahili ni kitenzi na nomino.
Katika kategoria ya kitenzi, neno hili (stahili) lina maana zifuatazo:

1. Kuwa na sifa ya kupata jambo fulani aghalabu kutokana na hicho ulichokifanya; faa.

2. Wajibika kutokana na jambo ulilolifanya au kulisababisha.

Ima katika kategoria ya nomino, neno hili (stahili) lina maana ya "hali inayomfanya mtu afikwe na jambo jema au baya".

Lakini katika lugha ya Kiarabu, neno hili (stahili) linakuwa  na maana mbili tofauti kutokana na utamkaji wa herufi 'h'; pale herufi 'h'  inapotamkwa kama 'h' kavu (dry 'h') kama ile iliyopo katika neno 'Alhamdu' na pale inapotamkwa kama herufi 'h' ya kawaida ile iliyopo katika neno 'hujambo'.

Kama ikiwa ni herufi 'h' kavu, basi neno (stahili) linakuwa linatokana na kitenzi cha Kiarabu istahaala (-mekuwa muhali/ugumu,uzito), na ikiwa ni 'h' ya kawaida neno hili linatokana na kitenzi 'ista-a-hala' (amestahiki).

Aidha,neno hili 'stahili' lilipoingia katika lugha ya Kiswahili, limejifunga na ile maana ya kustahiki tu wakati ikiitupa ile maana ya kuwa "muhali".

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)