MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'SAFIHI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'SAFIHI'
#1
ETIMOLOJIA YA NENO 'SAFIHI'.
Safihi (wingi: masafihi), katika Lugha ya Kiswahili) ni neno (nomino) lenye maana: 1. mtu mwenye tabia ya kutoa matusi, mtu anayevunjia watu heshima, mtu mfyosi. 2. mtu mnyamavu, mtu asiyeongea akisemeshwa.
Katika Sarufi ya Kiswahili neno hili (safihi) hutumika likiwa kitenzi na pia kivumishi.
Neno hili (safihi) asili yake ni Kiarabu na huko ni 'safiihun/safiihan/safiihin سفيه'  neno litokanalo na kitenzi cha Kiarabu safuha سفه (amekuwa mjinga).
Katika Lugha ya Kiarabu neno (safihi) lina maana zifuatazo:
1. Mtu aliye mbadhirifu wa mali kutokana na ujinga wake.
2. (Kwa nguo) ~ iliyoshonwa vibaya (thawbun safiihun.)
3. (Kwa mnyama) ~ asiye mwendo (naaqatun safiihatun = ngamia asiyekwenda mbio.)
4. Mtu asiye na tabia njema katika jamii.
Neno hili 'safihi' lilipoingia katika Lugha ya Kiswahili limejifunga na ile maana ya mtu aliye mtovu wa adabu na ile ya mtu mnyamavu.
Shukran sana.

Na;
Khamis Mataka
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)