MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

UCHAMBUZI - WAKATABAHU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
UCHAMBUZI - WAKATABAHU
#1
UCHAMBUZI - WAKATABAHU
Wakatabahu (Wa-kataba-hu) وكتبه ni kitenzi cha Lugha ya Kiarabu chenye maana (Ameuandika (waraka huu) fulani bin fulani.
Neno hili jumuishi huandikwa mwishoni mwa waraka/barua kumtaja mwandishi wa waraka huo/barua hiyo.
Neno hili kwa Kiingereza ni sawa na kusema: 'written by.../It is written by....'.
Ni desturi ya Waarabu kuandika hivyo mwisho mwa waraka/barua na kwa kuwa Waswahili walianza kukiandika Kiswahili kwa herufi za Kiarabu na hili nalo wakalibeba na kuwa mtindo wa uandishi wa barua zao.
Kiuchambuzi neno hili jumuishi linaundwa na maneno manne: matatu yanadhihiri na moja linajificha kama ifuatavyo:
1. WA ni Kiunganishi maana yake 'na'.
2. KATABA ni kitenzi kinachoihusu nafsi ya tatu ya kiume (kwa Kiingereza 'He') na Kiswahili (Yeye). Maana ya KATABA kwa Kiswahili: Ameandika.
3. HU ni Kiwakilishi nafsi ya tatu kikiwakilisha Shamirisho (Kilichoandikwa).
Tanbihi: Maneno ya Kiarabu kama ilivyo kwa Kifaransa yanahusika na mgawanyo wa kijinsia. Hivyo kama Shamirisho ni kitu cha jinsia ya kiume utatumia 'HUU' na kama ni jinsia ya kike utatumia 'HAA', yaani utasema: KATABAHAA كتبها.
4. Neno lisilodhihiri ni Kiwakilishi cha Nafsi ya Tatu ya Kiume na ndiye Mtendaji wa kitenzi. Ukisema KATABA (ameandika) kitenzi tayari kimeashiria aliyeandika ni mwanamume. Na kama ni mwanamke kitenzi kitakuwa: KATABAT كتبت. (Ameandika mwanamke).

Na.
Khamis Mataka
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)