MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

LIPO LA KUFANYA KWA AJILI YAKE (ABDULRAZAK GURNAH)

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
LIPO LA KUFANYA KWA AJILI YAKE (ABDULRAZAK GURNAH)
#1
LIPO LA KUFANYA KWA AJILI YAKE (ABDULRAZAK GURNAH)

??Ni yeye Profesa Abdulrazak Gurnah. Jina kubwa kwenye ulimwengu wa Fasihi. Jina liliandikwa kwenye riwaya kumi za maisha yake. Ama kweli baada ya dhiki faraja. Mungu ametufariji kwa faraja hasa kupitia mkono wake. Itazame Dunia ilivyoimba Jina lake na letu ghafla tu  limekuwa kubwa mno. Ametukuka Subuhana
??Mcheza kwao hutunzwa.  Kwanini tusimtunze? Ametunyanyua waswahili. Hivi kumuenzi itakuwa dhambi?
??Hakika leo Tanzania  hasa Zanzibar imekuwa midomoni mwa walimwengu. Watu wanaitaja kwa wema. Tena kwa wema uliotukuka. Ulimwengu juzi ulipofungua mdomo na kutamka." Tuzo ya Nobel ya Fasihi imekwenda kwa mzaliwa wa Zanzibar Profesa Abdulrazak Gurnah." Wengi walitaka kujua huyu ni nani?
??Kwa hakika Dunia imepata kumuelewa mtu huyu mpole,mcheshi, mjuzi wa mambo na mzalendo hasa. Kwenye hili utambuzi wake upo baina ya pua na mdomo.
Mara nyingi amelidhihirisha kupitia ulimi wake. Kalamu ilaliweka wazi tu. Mara ngapi amejinasibu kwa uzawa wake? Hii haitoshi? Msikilize alipoulizwa kuhusu tuzo hii. " Tuzo hii ni kwa ajili ya Afrika, Waaafrika na Wasomaji wangu." Allah akubariki kwa hili.
?? Binafsi amenishajihisha sana. Mimi ni mwanafasihi chipukizi. Acha niweke ndoto yake kwenye kichwa changu. Msururu wa vitabu miaka 40 baada ya uzawa wake. Vitabu kumi baada ya kile cha awali. Hakika amefanya kazi kubwa mno. Jitihada zake zimemuweka pale alipotaraji kuwa.
??Nikiri kwamba Jina lake niliwahi  kulisikia kupitia kwa rafiki yangu mmoja. Ila kwa hakika hakuniambia wala kujiongeza kumtafuta kufahamu nasab yake. Ila  tokea tangazo lilipotoka kwamba yeye ndio yeye. Nikasema "Hakika dutu imepata mpigaji." Kwani hili haliwafanyi Wanafasihi chipukizi kuongeza jitihada? Lipo la kujifunza kwalo.
??Nadhani ipo namna pia ya kushangiria hili.Si lake peke yake. "Mvyelewe harusi ngia uwanjani mtu lake hatendewa." Lazima tumuenzi. Na arudi kusitiri kitovu chake. Profesa karibu nyumbani tena. Mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba.  Njoo tukuvishe joho na kukufuta machozi kwa safari tuliyokutima. Wewe ni askari uliyeipeperusha bendera yetu vyema. Umeshinda vita njoo tushangiriye. Wewe ni wetu itavyokuwa tena wetu hasa. Aliyemo yumo asiyekuwemo haingii.

Ali Ben Othman
Arusha
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)