MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
Fasihi ya Kiafrika wakati wa ukoloni & baada ya ukoloni

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Fasihi ya Kiafrika wakati wa ukoloni & baada ya ukoloni
#1
Kazi nzuri za Kiafrika zinazojulikana Ulaya kutoka kipindi cha ukoloni na kile cha biashara ya utumwa ni za masimulizi ya utumwa, kama vile The Interesting Narrative of the Life of Olaudah Equiano (1789) cha Olaudah Equiano.
Katika kipindi cha ukoloni, Waafrika walioathiriwa na lugha za Ulaya walianza kuandika katika lugha hizo. Mwaka 1911, Yusufu Efraimu Casely-Hayford (ajulikanaye pia kama Ekra-Agiman) kutoka Pwani ya Dhahabu (sasa Ghana) alichapisha ile ambayo pengine ni riwaya ya kwanza ya Kiafrika kuandikwa kwa Kimombo, Ethiopia Unbound: Studies in Race Emancipation[9] Ingawa kazi hii iligusia hadithi na utetezi wa kisiasa, uchapishaji na kupitiwa upya na wanahabari wa Ulaya kulimaanisha wakati muhimu katika fasihi ya Kiafrika.
Katika kipindi hiki, tamthilia za Kiafrika zilianza kuibuka. Herbert Isaka Ernest Dhlomo wa Afrika ya Kusini alichapisha tamthilia ya kwanza ya Kiafrika kwa Kiingereza katika mwaka wa 1935. Mwaka 1962, Ngugi wa Thiong’o kutoka Kenya aliandika mchezo wa kuigiza wa kwanza wa Afrika ya Mashariki, The Black Hermit, hadithi iliyohadhari “ukabila” (ubaguzi kati ya makabila ya Afrika).
Fasihi ya Afrika mwishoni mwa kipindi cha ukoloni (kati ya mwisho wa Vita Vikuu vya Kwanza Vya Dunia na uhuru) iliendelea kuonesha mandhari ya ukombozi, uhuru, na (walau kati ya Waafrika kwenye maeneo yaliyotawaliwa na Ufaransa) kutambua weusi wa Waafrika. Mmoja wa viongozi wa harakati za kutambua weusi, mshairi na hatimaye Rais wa Senegal, Sédar Léopold Senghor, alichapisha mkusanyo wa kwanza wa mashairi ya lugha ya Kifaransa yaliyoandikwa na Waafrika mwaka 1948, Anthologie de la Nouvelle poésie nègre et malgache de langue Française, akishirikisha utangulizi kutoka kwa mwandishi wa Kifaransa Jean-Paul Sartre. [10]
Si kwamba waandishi wa fasihi ya Afrika wakati huo walikuwa mbali na masuala waliyoyakabili. Wengi, kwa hakika, waliteswa kwa undani na pia kwa kuelekezwa: akilaaniwa kwa kuyaweka kando majukumu yake ya kisanaa ili kushiriki kikamilifu katika mapambano, Christopher Okigbo aliuawa katika vita vya Biafra dhidi ya wanaharakati wa Nigeria katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1960; Mongane Wally Serote aliwekwa kizuizini kati ya miaka 1969 na 1970 chini ya sheria ya Afrika Kusini juu ya Ugaidi ya mwaka 1967, na hatimaye kutolewa bila hata kujibu mashtaka; mwananchi mwenzake Arthur Norje alijiuamjini London mwaka 1970; Jack Mapanje wa Malawi aliwekwa kizuizini bila kesi au tuhuma kwa sababu ya matamko aliyotoa katika baa ya chuo kikuu; na, mwaka 1995, Ken saro-Wiwa alikufa kwa kutiwa kitanzi na serikali ya wanajeshi ya Nigeria.
Fasihi ya Afrika baada ya ukoloni
Kwa ukombozi na kuongezeka kwa kusoma na kuandika kwani mataifa mengi ya Afrika yalipata uhuru wao katika miaka ya 1950 na hasa miaka ya 1960, fasihi ya Afrika imekua kwa kasi kwa wingi na kwa umaarufu, kwa kazi nyingi za Afrika kuonekana katika mitaala ya elimu ya Ulaya na katika orodha ya “vitabu bora” vilivyoandikwa mwishoni mwa karne ya 20. Waandishi wa Afrika katika kipindi hiki waliandika katika lugha za Ulaya (hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno) na pia lugha za jadi za Afrika.
Ali A. Mazrui na wengine hutaja migogoro saba kama mandhari: Farakano kati ya Afrika iliyopita na iliyopo, kati ya Utamaduni na Usasa, kati ya wazawa na wageni, kati ya kujijali na kujali jamii, kati ya Ujamaa na Ubepari, kati ya maendeleo na kujitegemea na kati ya Uafrika na ubinadamu. [11]
Mandhari mengine katika kipindi hiki ni pamoja na matatizo ya kijamii kama vile ufisadi, tofauti za kiuchumi kati ya nchi ambazo zimepata uhuru majuzi, na haki na majukumu ya wanawake. Waandishi wa kike wamewakilishwa vyema katika fasihi ya Afrika iliyochapishwa kuliko walivyokuwa kabla ya uhuru.
Mwaka 1986, Wole Soyinka alikuwa mwandishi wa Afrika wa kwanza baada ya uhuru kushinda Tuzo la Nobel katika fasihi, ingawa Camus Albert, mzaliwa wa Algeria, alipokea tuzo hilo katika mwaka 1957
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)