MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
Miongozo ya Lugha na Fasihi

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Miongozo ya Lugha na Fasihi
#1
MIONGOZO ya Lugha na Fasihi ni mfululizo uliokusudiwa wanafunzi na wapenzi wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Mfululizo huu umebuniwa kutokana na lengo la kuwasaidia wanafunzi wa lugha na fasihi katika ngazi mbalimbali za taaluma zao, hasa wale wanaojiandaa kwa mitihani ya Taifa. Mfululizo huu utatoa vijitabu ambaVyo vitakuwa vinasaidia kuchambua vitabu vya lugha na fasihi ambavyo vimeteuliwa na Wizara ya Elimu vitumike kuwatahini wanafunzi katika vyuo na sekondari nchini. Kwa hali hiyo, mfululizo huu utajumuisha uchambuzi wa vitabu vilivyochapishwa na Dar es Salaam Umvereity Press (DUP) na vile ambavyo vitakuwa vimechapishwa na mashirika raengine.
Uchambuzi wa kila kitabu utazingatia fani na maudhui yanayojitokeza katika kazi hiyo, na mwishoni kuna maswali ambayo yanamwongoza mwanafunzi. Miongozo hii imeandaliwa kwa kuzingatia utaalamu wa hali ya juu ili kurahisisha usomaji wa kitabu kinachohusika. Wanafunzi na wapenzi wa lugha na fasihi watafaidika mno na mfululizo huu. Mhariri mwanzilishi wa mfululizo huu anawatakia usomaji mwema.
Namna ya Kuitumia
Miongozo ya Lugha na Fasihi inaweza kuwa ya manufaa kwa wanafunzi; lakini pia inaweza kuhatarisha juhudi za welewa kwa baadhi ya wanafunzi. Miongozo ya aina hii inapasa iwe kichocheo kwa wanafunzi katika kushiriki hisia na mihemko ya mwandishi iliyoko katika kazi ya fasihi inayohusika. Kutokana na hoja hii, msomaji anatakiwa aione miongozo hii kama kitu kinachosaidia kuimarisha stadi na welewa wake na sio kibadala cha kitabu kinaohohusika.
Wakati wa kusoma miongozo hii mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa nipamoja na haya yafuatayo:
Quote:
· Kabla ya kusoma mwongozo wowote ule, inampasa mwanafasihi asome kwanza kazi ya fasihi inayohusika.
· Kilichoandikwa katika mwongozo wowote kisichukuliwe kuwa ni sawa na maandiko matakatifu kama vile Quran Tukufu na Biblia Takatifu. Msomaji una nafasi ya kukubali au kukataa maoni yaliyomo katika mwongozo unaohusika.
· Msomaji una nafasi ya kutoa uchambuzi na uhakiki mpana zaidi kuhusu kitabu kilichohakikiwa.
· Msomaji ihusishe kazi ya fasihi na mazingira ambamo watu walioandikiwa wanayaishi. Jifanye kama yanakukuta utayatatuajie?
Mwishoni mwa mwongozo wowote kuna maswali ambayo yanasaidia kupanua welewa zaidi kwa mwanafunzi na msomaji wa kawaida. Msomaji aghalabu yuko huru kujadili kwa mapana zaidi kazi inayohusika.
I Mwandishi
Penina Muhando ni Profesa na Afisa Mkuu Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mchango wake katika fasihi na taaluma ya Kiswahili ni mkubwa – hasa kwa upande watamthiliya.
Katika tamthiliya, ‘mwandishi huyo amepata kutunga Hatia (EAPH), Tambueni Haki Zetu (EAPH), Pambo (F. Books), Nguzo Mama (DUP), Harakati za Ukombozi (na wenzake) (TPH) na huu wa Lina Ubani (DUP). Kazi zote hizo zinajishughulisha sana na maisha ya watanzania kwa ujumla; kuanzia enzi za ukoloni hadi kipindi tulichonacho. Aidha, Lina Vbani ni tamthiliya inayoangalia matatizo yanayomkabili mtanzania wa leo kama tutakavyoangalia katika uchambuzi/uhakiki ufuatao.
II Dhamira Kuu
Maudhui ya Lina Ubani yanaweza kuangaliwa katika nyanja mbali mbali za maisha ya jamii ya kitanzania. Maudhui hayo yanazungukia dhamira muhimu ya ujenzi wa jamii tnpya, artbamo ndani mwake kuna vidhamira vingine vidogo vidogo. Tutazichambua dhamira hizo hapo ehini.
III Maelezo ya Awali na Dhamira Zenyewe
Kwa kipindi cha ‘miaka kadhaa nchi ya Tanzania imekumbwa na msukosuko wa kiuchumi. Kuyumba huko kunatokana na hali halisi kwamba bidhaa zake zimekuwa zile ambazo hupangiwa bei kutoka kwa wanunuzi wake ambao ni mataifa makubwa ya dunia ya kwanza.
Pamoja na hali hiyo, nchi ya Tanzania yenyewe ilipopata uhuru ilidhamiria kujengajamii nlpya anlbayo itakuwa na uhuruwa kweli, haki kwa watu wake, usawa wa binadamu, uchumi kuwa mikononi mwa umma na mengineyo ya aina hiyo. Hali hiyo ilianza kutekelezwa, lakini haikufikia hali nzuri kabisa. Hii ilitokana na kutotekelezwa kwa misingi thabiti iliyotangazwa katika “Azimio la Arusha” ambalo lilikusudiwa lirekebishe hali mbaya iliyokuwepo nchini. Kama kwamba hili halikutosha, hali iliongezewa uduni baada ya nchi hii kushiriki katika vita vya kumng’oa Idi Amini aliyekuwa ameivamia. Tamthiliya ya Lina Ubani inaisimulia vita hiyo kwa kutumia mbinu za kifasihi simulizi na za kisasa, kwani mwandishi anatumia masimulizi ya ngano kuhuSu dude lililowavamia ndege na wanyama katika makazi yao msituni. Baada ya kuvamiwa na dude liitwalo Dyamini, ndege na wanyama hawa walikimbilia kijiji cha jirarii walikowakuta binadamu, nao wakawapokea vizuri. Baadaye binadamu na ndege na wanyama wanashirikiana kupambana na kumfukuza Dyamini, lakini kwa sadaka kubwa ya uchumi na niaisha ya watu. Tunaweza kuchambua mambo yanayojitokeza katika tainthiliya hiyo kania ifuatavyo:
(a) Dhana ya Ukale na Usasa
Tamthiliya hii inatumia mbinu za aina mbili katika usimulizi wake. Kwanza, mwandishi anamtumia mhusica Bibi, ambaye hutamba hadithi ya Dynamini kwa mtoto Mota – ambaye ni mjukuu wake. Kwa kutamba hadithi, mwandishi ameonyesha, mbinu za kifasihi simulizi (ukale), na hivyo kufanya kwa mara ya kwanza pawcpo na jaribio la matumizi ya mbinu za kifasihi simulizi naza kisasa katika tamthiliya moja. Mhusika Bibi anaonyesha dhana yake ya ukale katika masuala mbalimbali; yakiwemo:
(i) Suala la Ndoa
Quote:
Bibi anasema kwamba suala la kuoa bila kufuata ushauri wa wazazi na mababu ni kosa. Mashauri na maelekezo ya wakongwe ni kuwa wanamchagulia mchumba kijana wao, na mara zote wanakuwa wa kabila moja. Bibi analaumu kuwa mtoto wake Huila hakumsikiliza alipomchagulia mchumba na kujiamulia kuoa mwanamke wa Kichusa. Kwa maono ya Bibi, mwanatnke huyu hafai, na mkatili kwa kila hali. Jambo la mtu kujiamulia kuoa anavyopenda linakiuka matakwa ya wazazi katika kabila la Bibi.
(ii) Chakula na Neema Nyingine
Quote:
Bibi anaonyesha pia kuwa neema ya chakula ilikuwa hapo zamani; siyo sasa ambapo anaona mambo yamebadilika. Bibi anamwelezea mjukuu wake Mota kuhusu kijijini kwao Malolo; kabla ya kuhujumiwa na mwanamke Lijino.
…mwanamke yule katufanya kitendo. Wenyewe tulistarehe kule kwetu Malolo. Chakula kila aina. Wewe ulikuwa mdogo sana mlipokuja na mama yako, Malolo, Ndizi! Viazi!! Miwa! mmoja humalizi (uk. 17).
Yawezekana lawama nyingine za Bibi kuhusu chakula kwa Huila na Sara zinatokana na imani ya hali ya maisha aliyoizoea ya kijijini na siyo ile ya mjini.
(iii) Elimu ya Zamani
Quote:
Bibi anaona pia hapo zamani mambo yalikuwa mazuri kwa upande wa elimu. Watoto wake, akiwa Daudi na Huila, walipokuwa wakisoma zamani walikuwa wanaimba na kufurahi sana, siyo kama hawa wa sasa, akina Mota. Nyimbo za sasa, Bibi anazionani kelele tu zisizo na msingi. Anaziona shule za siku hizi kuwa duni, kwani zimejaa kelele za ujamaa! ujamaa! tu.
(iv) Mabadiliko ya Kihistoria
Quote:
Katika hali isiyo ya kawaida tunamwona Bibi akiulizia mabadiliko ya jamii; jambo ambalo katika hali ya kawaida ya ukale wa Bibi tusingelitegemea, Katikatamko hilitunamsikia akisema:
Quote:
…niambiebasi. Zamani sanaulikuwepo utumwa – nasikia walikuwa wanapita kijijini kwetu wanapelekwa pwani. Utumwaukaisha. Ukaja ukoloni, wazungu wakaja kukaa pale kwetu. Halafu ukoloni ukaisha wazungu wakahama. Halafu ukaja uhuru, wakaondoka machifu. Babu Wa baba yako, huyo Daudi akaambiwa yeye si chifu tena. Halafu Uhuru ukaisha. Halafu ndiyo tukasikia Ujamaa! Ujamaa! Huuujamaa Mwalimu anasema utakwisha lini (uk. 27).
Mawazo ya Bibi katika dondoo hili yanaonyesha anatambua nguvu za mabadiliko katika jamii. Lakini pamoja na kutambua mabadiliko hayo, inaelekea Bibi huyo amechanganyikiwa, kwani kuna mawazo ya kukubali mabadiliko na kuna mawazo yanayopinga mabadiliko ya jamii kama tulivyokwishadokeza.
(v) Fasihi Simulizi
Quote:
Jambo jingine linalojitokeza ni lile linalohusu Fasihi Simulizi na imani za utambaji wake. Kuna imani miongoni mwa jamii mbalimbali kuwa utambaji wa hadithi unafanywa usiku na siyo mchana. Jamii hizo zilisisitiza jambo hili kufanyika usiku badala ya mchana kwa sababu muda wa mchana watu walilazimika kujishughulisha na kazi kama vile kilimo na usiku wakati wa mapumziko watambe hadithi. Dhana hii inajitokeza pia katika tamthiliya hiyo.
(b) Ukombozi wa Jamii
Dhamira hii muhimu inajadiliwa pia na mwandishi katika tamthiliya hii. Ukombozi huo tunaweza kuujadili kwa kuzingatia hatua mbili; kwanza, kwa kutumia ngano ya Dynamini aliyeivamia Tanzania, kuna mapambano ya kumwondoa adui huyo. Pili, kuna ukombozi wa Watanzania wenyewe na sualala kuijenga jamii mpya.
(i) Mapambano ya Kumwondoa Mvamizi
Ingawa katika ngano inayojadiliwa, Dyamini ndiye dude vamizi, lakini katika hali halisi, Idi Amini ndiye aliyeivamia Tanzania mwaka 1978. Uvamizi huo wa Amini ulifanywa kwa madai kwamba alikuwa akiwasaka wapinzani “Guerrillas” ambao ilidaiwa walitokea Tanzania. Baada ya uvamizi huo wa Amini, kulifuatiwa na mapambano makali yaliyofanywa kwa hatua.
– Hatua ya Kwanza
Hii ilihusu kupambana ili kupata nafasi ya kujenga daraja ya Kyaka katika mto Nile upya. Baada ya ujenzi huo wa daraja, kulikuwa na kuvuka kwa majeshi na vifaa vya kivita.
– Hatua ya Pili
Kupambana ili kumwondoa kabisa Idi Amini kutoka ardhi ya Tanzania. Hii ilifanyika kwa muda usiopungua majuma mawili.
– Hatua ya Tatu
Mapigano kuhamia Uganda. Haya yalidumu hadi kukombolewa kwa Uganda na Amini kukimbia kabisa.
Pamoja na kuikimbia Uganda, na pamoja na kuwa Tanzania ilikuwa imeshinda vita, kulikuwa na madhara ambayo yalitokana na vita hiyo.
– Upotevu wa Maisha ya Watu
Kulikuwa na vifo vya watu wengi, askari nawananchi. Kulikuwanawengi waliopata vilema vya maisha.’Katika tamthiliya hii tunaambiwa kuwa Daudi, mtoto wa Bibi alikufa vitani, kitendo ambacho yaelekea kiliwehusha akili yake.
– Kutetereka kwa Uchumi
Uchumi wa Tanzania ulitetereka kwa kiasi kikubwa. Inasemekana vita hiyo ilikuwa inatumia T.Shs.7,000,000.00 kwa siku moja na hivyo kudhoofisha kabisa uchumi wa Tanzania ambao ulikuwa tayari umeanza kuimarika kwa wakati huo. Aidha, tatizo la uchumi nchini linatokana pia na hali ya uchumi duniani.
– Wizi wa Fedha za Umma
Kuna methali inayosema “Kufa Kufaana!” Vita hivyo vimeleta tabia ya wizi kwa baadhi ya maofisa wajeshi na hata wa kawaida.
Kwaupandewa maofisawajeshi, baadhi yaowalikuwaamawanaiba fedha, au wanazitumia vibaya fedha walizokuwa wamepewa kwa ajili ya vita.
Pensheni ya wanajeshi waliofia vitani kama vile Daudi wa tamthiliya haikuwafikia, wamekula “wakubwa”. Waliopoteza viungo vyao wakati wa mapigano pia hawakulipwa.
Maofisini, watu mbalimbali walikuwa wameiba fedha kwa kisingizio cha vita.
Kuliibuka matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi na kila tatizo ilisemwa ni kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwa imetokana na vita vya kumwondoa Amini. Kimsingi, hivyo vilikuwa visingizio tu. Kutokana na hali ilivyokuwa, kuna baadhi ya watu wanaona ni afadhali kama Tanzania isingeingia vitani – kwani imeleta hasara zaidi kuliko faida. Lakini Amini angekaa hapa hadi lini?
(ii) Ujemi wa Jamii Mpya
Dhamira hii imekuwa ikijitokeza katika kazi nyingi za kifasihi toka kutangazwa kwa “Azimio la Arusha” ambalo ndilo lilikuwa nguzo ya ujenzi wa jarnii mpya iliyokusudiwa. Jamii mpya kimsingi ilipasa kuzingatia mambo kama vile usawa wa binadamu, haki miongoni mwa watu wajamii, uongozi safi, niakazi bora na chakula cha kutosha. Mwandishi wa tamthiliya ya Lina Ubani amechambua matendo ya wanajumuia na kuyatafiti kwa undani.
– Suala la Haki
Mwandishi anaiona jamii kukosa kuWatendea haki watu kama wanavyostahili. Katika kuilalamikia jamii, mwandishi anatumia mifano mbalimbali, lakini ya msingi hii inayotajwa hapa chini:
I. Kuhamia Vijijini
Miaka ya 1970…; Tanzania iliamua kuwahamishia watu katika vijiji vya maefndeleo. Mipango ya kuwahamishia watu katika vijiji haikutekelezwa vyema. Watu walihamishwa kutoka sehemu nzuri na kuwekwa nyikani kama mhusika Bibi anavyosema; na kulalamikia uamuzi wa Lijino hivi:
Quote:
Basi kaja huyo Lijino huyo! Mfflh! Mwanamke yule! Nasikia ana watoto lakini utafikiri hakuzaa. Mtahama! Amri moja! Kwa hiyari mmekataa. Sasa amri moja. Mmh! Basi kwenda kutuweka nyikani….
Huu ni mfano mmoja wa kunyimwa haki kwa bitiadamu.
II. Kunyimwa Vitu/Vyeo Wasomi
Jambo jingine muhitnu linaloonyesha kukosekana kwa haki kwa watu m kule kuwapa vyeo wasiosoma, na wasomi kuwatUmikia wasiosoma. Imeelezwa kuwa wale waliosoma wanakosa hata gari la kutembelea wakati wale wasibsoma ndio wenye kustarehe. Tazama Bibi anavyosema kuhusu suala hilo:
Quote:
…. Kumbe vyeo wanakuja kupata wasiosoma. Baba yako kasoma, kasoma miaka na miaka. Sasa mie namuuliza, ‘hivyo mwanangu kusoma kote kule hata gari unashindwa kununua?’ Akaniambia eti magari hayaruhusiwi. Mbona barabarani yamejaa?. Eti hayo ni ya wakubwa. Hao wasiosoma hao! Ningejua wanangu wasingesoma. Wamesoma nimepata faida gani? (uk. 33 – 34).
Mwandishi anaichambua jamii ya Tanzania katika uhalisi wakc. Kwa muda mrefu sasa watu ambao elimu yao si ya juu sana, au hata wale wasiosoma kabisa, wamekuwa ndio wanaoteuliwa kuwa viongozi. Wamekuwa wakitembelea magari, na wameruhusiwa kununua magari. Hali hii imekuwa ikikatisha tamaa watu wengi, na hivyo wakati mwinginp kuathiri utendaji kazi wa wasomi mbalimbali.
Katika utendaji kazi, tumeona kuwa wakati mwingine kumekuwa na chuki kati ya wasomi na wasiosoma, na kwa sababu hii; wasiosoma wamekataa kushauriwa nawasomi. Mfano mzuri hapa niwa Zoersi na Huila.
Huila ni mtaalamu na ni msomi wa kiwango chajuu. Kila mara amekuwa akijitahidi kutoa ushauri kwa mwanasiasa mashuhuri, lakini aliyekosa busara na welewa Bwana Zoeni. Zoeni, kama zilivyo tabia za baadhi ya wanasiasa, amekuwa akidharau kabisa mawazo ya mtaalamu Huila. Kisingizio kikubwa cha Zoeni ni kuwa SERA ya CHAMA haiwezi kujadiliwa na wataalamu. Matokeo ya dharau ya watu wa aina hii ni kuanguka kwa uchumi wa nchi na kufanya mikataba ya kuifilisi nchi. Iko mifano kadhaa katika tamthiliya hiyo.
– Zoeni anagongana kimawazo na Huila wakati anapotoa ushauri wa kitaalamu. Zoeni anaona Huila anamfundisha kazi, na hivyc anamfokea:
Quote:
…sihitaji ushauri wako. Kazi yako ni kutekeleza. Sera siyo kazi yako. Ondoka ofisini kwangu… (uk. 25).
– Zoeni anafanya mikataba kwa niaba ya nchi ambayo inahatarisha kabisa uchumi wa nchi. Kwa mfano kuna mikataba inayohusu nishati katika nchi nzima. Kwa sababu ya kutokuwa na upeo mkubwa vva kitaalamu, tunaambiwa Zoeni aliwekeana mikataba na nchi zilizoendei ‘a ili kupata mitambo ya nuklia ambayo haikutakiwa kwa wakati huo nchini. Zoeni anamkebehi mtaalamu na kumdharau, kwa mfano anasema;
Quote:
…. Tujadili sera? Unazungumza nini bwana mtaalamu? Sera inajadiliwa?
…. Ulipokuwa unasomea huo utaalamu hawakukufundisha kuva sera ikishapitishwa haijadiliwi?
…. Ninyiwataalamukwaninimnapendakuchezeaakilizawatu. Pesa zote tunapoteza kusomesha watu, utaalamu wenyewe ndiyo huu… (uk. 24 – 25).
Iko pia miradi mbalimbali inayotekelezwa bila mpango maalumu kama vile kuanzishwa kwa “windmills” katika kila kijiji (jambo ambalo haliwezekani), kushughulikia mti wa ‘Hanga’ unaotoa mafuta ambao Zoeni amepata habari kuwa Philippines kuna mti huo ambao yawezekana upo pia nchini. Bila kufanya tathmini, inaamriwa rnradi uanze mara moja! Hili ni jambo la hatari na linaonyesha hali halisi ambayo imekuwa ikitokea nchini. Miradi mingi imeanzishwa na kufa bila mafanikio kutokana na kutosikiliza maoni na ushauri wa wataalamu wetu. Muda umefika wa kubadilisha hali hii.
– Suala la Makazi Bora
Jamii ya Tanzania ilikusudia kujenga makazi bora kwa wananchi wake, hasa baada ya kutangazwa kwa “Azimio la Arusha”. Ingawa wazo lilikuwa zuri, utekelezaji wake haukuridhisha kwa kiwango kikubwa. Yaelekea vyombo vya dola vilitumia vibaya madaraka yake na hivyo kuwatesa wananchi bila sababu za msingi. Kuna watu waliobomolewa nyumba zao eti kwa sababu zilikuwa nje ya kiwanja kilichopimwa, lakini ilikuwa katika eneo lililotakiwa; kama Bibi anavyolalamika:
Quote:
…Mh! Tuna taabu. Huyo Kibwana Kata! Mmh! Shoga yangu Mama Senga nyumba yake maskini: ‘Bomoa! Haiko kwenye kiwanja’. Tumetutika maji sie! Tukasema: hela Senga kaleta, maji tutashindwa kuteka nyumba ijengwe? Hata! Basi kila kukicha ndoo kichwani. Halafu Kibwana Kata anakuja: ‘Bomoa!’ Tukadhani anatania. Wakabomoa… (uk.12)
Hali hii inaonyesha kwamba watu wengi waliathiriwa na “Operesheni Vijiji” ya miaka ya mapema ya sabini. Wananchi wengi waliteseka. Kuonyesha kwamba kulikuwa na utekelezaji mbaya wa Operesheni hiyo hivi sasa baadhi ya watu waliohamishwa wakati huo wameruhusiwa kurudi kwenye vijiji vyao vya zamani.
– Mipango Mibaya ya Maendeleo
Tumeidokeza dhamira hii pale awali. Lakini pengine hapa tungezungumzia tatizo la mipango mibaya ya maendeleo na utekelezaji wake. Mfano wa maelezo ya jambo hili nl ule wa Talafa aliyegeuzwa shingo “uso ukawa nyuma”. Inasemekana aliwalazimisha wananchi walime pamba ambayo haikuchukuliwa/kununuliwa na serikali kwa vile hapakuwa na daraja la mto uliokitenga kijiji hicho. Mwaka uliofuata inasemekana wananchi waliamua kulima fiwi badala ya pamba. Jambo hili linaonyesha pia mpango mbaya wa utekelezaji wa sera za kiuchumi nchini na kusema kweli matukio ya aina hii nimengimno.
Kuna Ubani
Huo wote ni mvundo ambao si sawa na ule wa “La kuvunda halina ubani”, bali “La kuvunda lina ubani!” Hakuna tatizo hata moja kati ya yaliyosemwa ambayo hayawezi kutatuliwa. Kuna ubani…. Matatizo haya yana dawa. Ni suala la kuamua tu. Mifano michache imeanza kuonekana katika baadhi ya taasisi zetu: Kwa mfano, hivi sasa Waziri wa Mambo ya Ndani anajitahidi kuisafisha jamii. Rais na Waziri Mkuu wamemwunga mkono. Ili kufanikisha jambo hili, ni lazima watanzania wote tumwunge au tuunge mkono juhudi hizo za kuleta “ubani” utakaoondoa “mvundo” kama vile uzembe, wizi, uvivu na ufujaji wa mali ya umma na pia unyimaji wa haki kwa watu.
© Dhamira Nyingine
Pamoja na dhamira hizo tulizoziona, kuna dhamira kadhaa ambazo ingefaa zijadiliwe hapa. Tuziangalie dhamira hizo.
(i) Imani ya Ushirikina na Uchawi
Jamii nyingi zina imani hizo za uchawi na ushirikina. Nchini Tanzania imani hizo pia zipo; na kimsingi zilipata kujitokeza wakati wa “Operesheni Vijiji” ambapo inasemekana baadhi ya watendaji wake walikumbana na matatizo mengi. Uchawi na ushirikina wakati mwingine vimetumika kama nguzo ya wanyonge ya kujitetea dhidi ya tabaka tawala. Hatuna ushahidi wa kufanikiwa kwake, lakini kuendelea kutumiwa kama nguzo na baadhi ya jamii ni dalili kuwa huenda kuna mafanikio.
Katika tamthiliya ya Lina Ubani tunaambiwa kuwa Talafa aliyekuwa msumbufu kwa wanakijiji walioktiwa wamelima fiwi badala ya pamba aligeuzwa shingo, uso umetazama mgongoni! Jambo hili ni la kutisha. Linaweza kubadilisha nia ya afisa yeyote mtendaji ambaye atakwenda kijijini hapo.
(ii) Elimu na Nafasi Yake
Tumetaja hapo awali kuwa Bibi alisifia elimu ya zamani. Lakini hakujadili mchango ama nafasi yake katikajamii.
Tamthiliya hii inaonyesha umuhimu wa elimu katika jamii na hasara zinazoweza kutokea kama elimu haithaminiwi. Kutothaminiwa kwa wasomi wetu kunaweza kuleta madhara makubwa.
Elimu ya jadi pia imedokezwa kwa namna fulani katika tamthiliya hii. Elimu hii inatolewa kwa kizazi kipya kupitia hadithi kama vile Bibi anavyofanya kwa Mota. Elimu zote zinaweza kuwa za manufaa katika jamii zikitumiwa vyema.
(iii) Nafasi ya Mwanamke katika Jamii
Mwanamke katika tamthiliya hii ana nafasi za msingi mbili: mwanamke mzazi na mwanamke mfanyakazi.
– Mwanamke Mzazi
Mwanamke katika kipengele hiki amejengwa akiwa na nafasi yake kama mama watoto. Hapa tunawaona akina mama wawili: Sara akiwa na mtoto wake Mota. Pili kuna Bibi ambaye ana watoto Daudi na Huila. Seti mbili za akina mama na watoto hao zinakamilishwa kwa dhana muhimu ya malezi. Mama, inakubalika na kueleweka kuwa ni mwalimu wa kwanza wa mtoto. Kwa hiyo nafasi yake kama mlezi ni muhimu sana katikajamii. Malezi mema huzaa chema. Malezi mabaya huzaa kibaya. Tumeonyeshwa katika tamthiliya hii mbinu na watu mbalimbali walio muhimu katika malezi, msingi wa kwanza akiwa ni mama.
– Mwanamke Mfanyakazi
Mwanamke huyu ni msomi. Hapa tuna mfano wa Sara na Lijino. Hakuna tatizo kubwa linalojitokeza kwa Sara, lakini tunaambiwa na Bibi juu ya mwanamke Lijino kuwa alikuwa mkatili, kama kwamba hakuzaa. Usemi huu unasisitiza ukatili wa Lijino.
Kutokana na hali hii, tunaweza kusema kuwa tabia haitegemei jinsi-nafsi. Mwanamke ana uwezo sawa tu na mwanaume kama akipewa nafasi inavyotakiwa.
(iv) Mjadala Kuhusu Ushairi
Suala la ushairi wa vina na mizani (kimapokeo) na ule wa masivina linaelekea kujitokeza katika tamthiliya hii. Mota katika tamthiliya hiyo anatunga “ngonjera” ambayo “haina” vina na mizani.
Katika ngonjera yake anawakashifu Madyamini ambao yeye anawaona wako hata sasa:…hapa hapa shuleni, kama yulefulani anakaa deski la mbele, kachukua machungwa ya wenzake… (uk. 55). Hapa dhana ya Madyamini imepanuliwa na kuwa wabaya wote.
(v) Ulevi na Ukweli wa Maisha
Mwanahego ni mtu aliyechorwa kuwa ni mlevi ambaye anaonekana kuwa na akili zake zenye ukweli mtupu. Maneno anayoyasema Mwanahego si ya mlevi, bali ni mtu ambaye ameamua kuserna ukweli, lakini baada ya kujifanya mlevi. Kwa upande mwingine, tukubaliane na hali hii ya ulevi, je, Mwanahego anaelewa juu ya suala la umoja? Anaelewa umuhimu wa fedha za kigeni? Kuna utata.
Ni vyema kuelewa kwamba mlevi mara nyingi hakumbuki anayosema. Mlevi ni tofauti na mnywaji. Tunafikiri Mwanahego ni kipaza sauti cha mwandishi ambaye amedhamiria kuihakiki jamii yake.
Mwisho, tunaweza kusema kuwa hizo ni baadhi tu ya dhamira za Lina Ubani. Wasomaji wana nafasi ya kufanya utafiti zaidi na kugundua dhamira zaidi.
IV Vipengele vya Fani
Fani na maudhui ni pande mbili za sarafu moja. Lazima vitu hivyo viangaliwe katika mchangamano. Lakini hapa tumetenganisha kwa ajili ya majadiliano tu. Majadiliano yatazingatia muundo na mtindo, ujenzi wa wahusika, mazingira au mandhari, na hatimaye matumizi ya lugha.
(a) Muundo na Mtimdo
Tamthiliya hii inatumia mbinu za aina mbili za kimuundo. Mbinu hizo ni za kifasihi simulizi na zile za kidrama ambazo ndizo wasanii wengi wa tamthiliya huzitumia hivi sasa.
Katika kuineemesha, mwandishi anatumia (viingizi vya) nyimbo na maombolezo, ambavyo au huletwa na watambaji wanaounda sehemu ya wahusika na wahusika wengine kama vile Bibi.
Kimtindo, tamthiliya hii inatumia masimulizi ya ngano katika kuelezea ukweli wa namna fulani wa kifasihi. Aidha, kuna mbinu za kisasa za kidrama pia. Hali hii huunda michezo miwili katika mmoja.
Wachezaji muhimu wa mchezo ule wa kifasihi simulizi ni Bibi na Mota, wakisaidiwa na watambaji. Wale wanaotumika katika mchezo wa kidrama ambao ni wa kisasa ni pamoja na Zoeni, Huila na wale watu wa mataifa ya kigeni.
Michezo yote miwili huenda sambamba na kuunganishwa na watambaji. Watambaji katika tamthiliya hii ni muhimu kwani wao wanasaidia kupambanua zaidi dhana muhimu ya ukale na usasa.
Maombolezo katika tamthiliya hii yanaletwa na Bibi (ambaye kwa kweli kwa namna fulani analeta kero). Maombolezo hayo ni mengi, na tunadiriki kusema kuwa hii ni tamthiliya ya kwanza ya aina yake. Haijawahi kutokea tamthiliya ya aina hii, na Profesa Muhando anastahili pongezi.
Suala la matumizi ya nyimbo na ngoma limejitokeza katika tamthiliya hiyo. Wasomaji hufurahia kuisoma lakini wakati huo huo kuwa makini katika kutoa uhakiki wake.
(b) Wahusika
Kama tulivyodokeza sehemu nyingine hapo awali, wahusika ni watu, wanyama, vitu na mahali. Vitu hivi pamoja na viumbe hai vinaweza kutumika katika kazi ya fasihi kwa pamoja, au vinaweza visitumike vyote kwa mara moja. Hapa tutachambua wahusika muhimu tu – wakiwemo Mtambaji, Bibi, Huila, Zoeni, Mota, Daudi, Mwanahego, Lijino, Dyamini na wengineo.
(i) Bibi
Miongoni mwa wahusika muhimu wa tamthiliya hii ni Bibi. Kupitia Bibi, mwandishi anatoa dhamira mbalimbali ambazo zinaihusu jamii nzima. Bibi mwenyewe aghalabu anaonyesha tabia za aina yake pia.
– Ni mlalamishi. Ana uchungu wa kufiwa na mtoto wake kipenzi Daudi.
– Kiungo muhimu katika dhamira ya ukale na usasa. Msisitizo wake wa kutaka mtoto wake achaguliwe mchumba wa kabila lake, kusifia kwa nyimbo za zamani, kutamba hadithi ni miongoni mwa vitu vinavyothibitisha dhana ya ukale na usasa.
– Amechanganyikiwa. Tabia zake katika hadithi ya tamthiliya hii inashindwa kueleweka. Je, ni nini hicho anachodai kiteremke toka, mawinguni? Kuna nyakati tunafikiri labda ni utawala/viongozi u(wa)lio juu na wanalazimishwa kuteremka. Aidha, kuna wakati inajionyesha tabiayawehu.
– Ni mtu asiye na shukrani.
Haridhiki kwa huduma anayopewa na mke wa Huila. Hampendi Sara – anamwita mchawi.
– Ili kuonyesha uzee wake, Bibi amepewa sifa zote za kizee.
– Mhakiki muhimu wa jamii, kwani anazungumzia matatizo ya kuhamia vijijini yaliyotokana na utekelezaji mbaya, matatizo ya ndoa za mseto wa makabila na kadhalika.
(ii) Zoeni
Huyu ni mwanasiasa ambaye kimsingi amepewa tabia nyingi zinazoudhi. Tabia hizo ni kama zifuatazo:
– Ana dharau na hajasoma elimu ya kisasa. Haambiliki.
– Ana kiburi. Yeye ni mhusika muhimu ambaye anakuwa nguzo ya mchezo katika tamthiliya hiyo yenye mbinu za kidrama.
– Mwanasiasa asiye makini. Hajali utaalamu wa wasomi kama vile Huila.
– Ni mpenda rushwa na hongo. Aidha, ni mzembe! Hali hii inajitokeza wakati anapokwenda mkutanoni kuiwakilisha nchi naye analala katika chumba cha mkutano.
– Ni mbadhirifu wa mali ya umma kwa shughuli zake za binafei.
– Hana adabu kwa wafanyakazi wengine. Anawatukana na kuwaaibisha mbelezawatu.
(iii) Huila
Tofauti na mhusika kama Zoeni, Huila ni msomi, ambaye ana tabia zifuatazo:
– Ni mtulivu namvumilivu mkubwa.
– Nimchapa kazi, na ana juhudi kubwa.
– Hakatitamaa upesi.
– Ni mtetezi wahakiza binadamu.
– Ana ushirikiano mkubwanawafanyakaziwenzake.
– Anajalifamilia yake wakati wote.
(iv) Mwanahego
Miongoni mwa wahusika airibao wamechprwa kuwa wazembe, lakini ni muhimu sanani Mwanahego.
– Ni msema ukweli
– Nimcheshi
– Anawahakiki viongozi wazembe katika J’amii.
(v) Sara
Ni mke wa Huila. Anamsaidia sana mume wake katikakumfariji anapokuwa namatatizo.
(vi) Mota
Huyu ni mtoto wa Huila na Sara. Anakuwa kiungo muhimu cha rtiaelezo kuhusu malezi ya kizazi kipya.
– Mota anatumika kuelezea migogoro kati ya ushairi wa mapokeo na masivina.
– Ni mwelezaji wa hali ya ubaya miongoni mwa watu: Kwamba kila mahali kuna wabaya (Madyamini).
– Ni msikivu. Ni mtulivu. Ana akili bora.
(vii) Daudi
Kakake Huila ambaye alifia vitani; wakati wa kumfukuza Dyamini.
(viii) Dyamini
– Mvamizi.
(ix) Watambaji
Wanaisimulia hadithi na kuiunga kati ya hadithi ya kingano na ile ya kisasa.
(x) Wahusika wengine
Lijino, Katibu Kata, Katibu Tarafa na wengine wanasiasa.
© Mazingira/Mandhari
Mazingira ya tamthiliya hii ni ya kitanzania. Ni mazingira ya baada ya Azimio la Arusha na vita ya kumwondoa Idi Amini. Japokuwa hadithi (sehemu kubwa) inasimuliwa kingano, hadithi hiyo inaihusu Tanzania.
(d) Matumizi ya Lugha
Lugha ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa jamii. Matumizi ya lugha hutofautisha kazi – kazi ya kisanaa na isiyo ya kisanaa.
Katika tamthiliya hiyo, mwandishi ametumia lugha vyema katika kuwajenga wahusika wake. Tuchambue matumizi yake.
(i) Lugha ya Kikabila
Mwandishi amemjenga mhusika muhimu sana, Bibi, kwa kutumia lugha za aina mbili: lugha ya Kiswahili fasaha na lugha ya kikabila – Kikaguru. Jambo hili limesaidia kwa namna moja katika kuumba hali halisi aliyokuwa nayo Bibi. Lakini pia, tahadhari ni kuwa baadhi ya mambo ambayo hayakutafsiriwa kwa Kiswahili yatashindwa kufikisha ujumbe ipasavyo.
(ii) Lugha za Kigeni
Yako matumizi ya lugha za kigeni, zikiwemo Kifaransa, Kiingereza, Kijerumani n.k. katika kuwajenga wahusika wanaohudhuria mkutano wa kimataifa. Hali hii inaweka mazingira ya tamthiliya iwe karibu na uhalisia wa mambo yanayozungumzwa.
(iii) Kiswahili Fasaha
Lugha hii imetumiwa na msanii pia. Pamoja na lugha hii, kuna pia matumizi ya lugha iliyo sanifu.
(iv) Matumizi yu Methali, Misemo na Nahau,
Mwandishi ametumia misemo na nahau, pamoja na methali pia katika kuimarisha kazi hii. Angalia kwa mfano;
– Penye wema(…) ubaya huzengea (uk. 36)
– La kuvunda lina ubani (uk. 58).
(v) Tamathali za usemi.
Mwandishi ametumia tamathali mbalimbali za usemi. Tamathali hizo ni pamoja na sitiari, tamathali ambayo hulinganisha mambo/vitu viwili au zaidi vyenye sifa tofauti, lakini haitumii maneno ya viungo kama tashbiha. Mfano wasifa tofauti ni huu ambao ni kilio cha Bibi.
Quote:
“Aliyeua Daudi (Kaua jembe langu)”
………
(Kaua kuni zangu)
………
(Kaua nguozangu) (uk.2)
Kwa upande wa tashibiha, hizo nazo zimetumiwa katika tamthiliya hii. Tunamsikia Bibi akisema:
Quote:
….Basi kupaka tu wacha iniwashe. Inachonyota kama upupu Kaja Talafa, Mkali kama pilipili
Tunaweza kupata picha ya sabuni hiyo inayosemekana inachonyota kama upupu. Lazitna iwe sabuni mbaya! Halafu tunamfikiria huyu Katibu Tarafa aliye mkali kama pilipili. Hapana shaka huyu ni mtu mkatili na hana utu wala ubinadamu.
Matumizi ya tamathali za tabaini yapo pia. Tabaini ni mtindo wa uneni wa fasaha ambao kwayo msemaji husisitiza kauli kwa kutumia maneno yenye ukinzani, aghalabu neno si. Tunamsikia Bibi akimlalamikia au kumsema mtoto wake aliyeamua kuolewa na Mchusa aliyemwelezea ukatili wake kuwa alikuwa, “Mbogo si mbogo, Kifaru si kifaru”. Matokeo yake? Inasemekana Melina “akakonda akawa mifupa mitupu”. Kwa mara nyingine tena tabaini hapa imeimarishwa na tamathali ya sitiari.
Kumekuwa na matumizi pia ya tamathali ya kiritifaa. Ritifaa ni mbinu ya aina ya semi ambazo kwazo (i) mtu aliyekufa huombolezwa na kuliliwa kama vile angali hai. (ii) vitu visivyokuwa ulimwenguni kwa sasa, husimuliwa au husifiwa kama viumbe katika hali ya maisha ya duniani. Katika tamthiliya ya Lina Ubani Bibi analia na kaomboleza mara kwa mara kuhusu mtoto wake Daudi. Tena pia tunamsikia akimlaumu Dyamini na kumkashifu kutokana na ubaya wake. Pamoja na tamathali hizo, kuna matumizi machache ya dhihaka na kejeli.
Licha ya tamathali tulizozisema, mwandishi artietumia pia mbinu nyingine za kisanaa. Mbinu hizo kwa mfano ni takriri mbalimbali. Takriri ni mbinu ambayo husisitiza jambo kwa kulirudiarudia. Ziko takriri za aina mbalimbali: takriri-imundo, takriri-neno na kadhalika. Katika tamthiliya hii takriri zinazojitokeza mara nyingi ni zile za maneno. Angalia kWa mfano Mota anavyoyalalamikia Madyamini – ambayo anayaona kuwapo: “Madyamini shule, Madyantini vijijini, Madyamini mijini”. Neno Madyamini limerudiwa ili kusisitiza dhana anayoitaka msanii. Hakika mbinu hizi ni nyingi mno na zinasaidia sana kuimarisha kazi hii. Matumizi ya mdokezo yapo pia kwa wingi. Hii ni tobinu ambayo kwayo mwandishi husema na kukatiza maneno na kumwachia msomaji au msikilizaji ahisi yeye binafsi mwisho wa maneno hayo. Kwa mfano Huila anasikika kwenye simu: “Haloo… Oh! Dr. Matayo…eeee… ndiyo…mama…ee?Vipitena…?eeh? (uk. 57). Maneno hayo yanaonyesha hamu ya kujua nini kipo upande wa pili. Mbinu ya mjalizo imetumika pia. Mbinu hii huunga vifungu vya’maneno kwa kutumia mikato, kwa mfano, kama Huila anavyolalamika kuwa…. “Nimekwenda kote huko! Ugawaji, Usagishaji, Biashara” (uk. 36). Tashtiti, hali ya kuuliza na kushangaa mambo yanayofahamika imetumiwa vyema na mwandishi wa Lina Ubani. Mifano iko mingi. Pamoja na tashtiti kuna pia matumizi ya nidaa. Nidaa m aina au namna ya msemo wa msisimuo au sauti ya mshangao atoayo mtu kudhihirisha maono yake ya ndani au kilio cha moyo wakati apatwapo na mgutusho ghafla wa furaha, hasira, huzuni, chuki na kadhalika. Nidaa imetumiwa sana na mwandishi wa Lina Ubani. Sara, kwa mfano anapomwona Bibi analia na kuendelea kuwa mlalamishi anasema: “Ee Mungu wangu!” (Anatoka) (uk. 32). Msemo huu unaonyesha nidaa. Tamathali na mbinu za kisanaa zimesaidia katika kuijenga taswira pia.
Hizo ni baadhi tu ya mbinu za kisanaa katika tamthiliya hii ya Lina Ubani. Utafiti zaidi unaweza kuzifafanua nyingine.
V Mwisho
Profesa Penina Muhando anlefanya jaribio ambalo halijawahi kufanywa katika uandishi wa tamthiliya za Kiswahili. Jambo hili limefanya tamthiliya hii kuwa na hadhi ya aina yake rta ya kipekee kuliko zile alizopata kuziandika mwenyewe. Aidha, kwa rtsomaji wa kawaida anaweza kujikuta katika matatizo ya kushindwa kuufuatilia vema mchezo huu kutoka mwanzo hadi mwisho. Vinginevyo, hiini kazi bora, tunampongeza Profesa kwa kazi nzuri hii.
VI Maswali
1. Ni kwa vipi dhamira ya kisiasa imejitokeza katika Lina Ubani.
2. Eleza maana ya muundo na mtindo katika kazi ya fasihi. Je, Lina Ubani ina muundo na mtindo gani?
3. Chambua dhamira za Lina Ubani, kishajadili kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mwandishi.
4. Jadili wasifu wa wahusika Zoeni, Bibi, Sara na Huila.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)