MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NDOTONI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: NDOTONI
#1
NDOTONI

Mgeniwo nimefika, naomba unipokee,
Ni kwema nilikotoka, wasiwasi uondoe,
Mno tumekukumbuka, twatamani urejee,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Sikutaka kuamini, punde niliposikia,
Umetoweka nyumbani, machoni sitokutia,
Nikawaza hivi nani?, pengo atakuzibia,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Sasa umeshazoea, kamba huna mguuni,
Naona wafurahia, tabasamu nabaini,
Nitaenda simulia, sitoacha abadani,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Kwa kweli wewe ni jembe, hakika nakwaminia,
Ulichukia uzembe, nani asiyelijua?
Ukatufanya tutambe, heshima kutupatia,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Kila nimachochunguza, naona yako alama,
Kiswahili ulikuza, hukutaka kiwe nyuma,
Vya kwetu kuvitukuza, takukumbuka daima,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Wanyonge ulitetea, kwa kuvitenda vitendo,
Furaha ikawajaa, wakazidisha upendo,
Tena ulipogombea, ukashinda kwa kishindo,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Taifa ulilijenga, uchumi kuimarisha,
Mipango uloipanga, hakika ilinikosha,
Nchi ukaipa mwanga, gizani kuiondosha,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Ilipozuka Korona, mashaka yalinijia,
Namna nilivyoona, wenzetu waangamia,
Ukasimama kunena, Mungu wa kutegemea,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Kwa kutumia utunzi, hatua nitachukua,
Kuhamasisha ujenzi, wa taifa Tanzania,
Kwa dhati nitayaenzi, mema ulotuachia,
Siku itakapofika, nasi tutakuwa huku.

Kwa heri baki salama, sasa narudi nyumbani,
Umefurahi mtima, kuyaona maskani,
Nikampe lipi mama? alihifadhi kichwani,
Ilikuwa njozi njema, sasa kumepambazuka.

Mtunzi: JOHN LUKAS JOHN (Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Lugha na     Utawala- Chuo Kikuu Mzumbe).

0788514751/0747225775.
 johnlucasjohn074@gmail.com
Reply
#2
Hongera sana John kwa shairi zuri
Mwl Maeda
Reply
#3
(09-01-2021, 11:26 AM)MwlMaeda Wrote: Kongole sana John kwa shairi zuri

Ahsante sana
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)