01-07-2022, 01:46 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFYUNI'
Neno *afyuni* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli:i-/i-]* yenye maana ya 'kileo chenye umbo la kidonge kunachotengenezwa kutokana na utomvu wa *mpopi*( *afyuni* ) , ambacho kwa kawaida hutumika kama tiba ya kutuliza maumivu, aghalabu hutumiwa kinyume cha sheria kama dawa ya kulevya.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *afyuni* (soma: *afyuunun/afyuunan/afyuunib افيون)* lina maana ya 'dutu inayotolewa kwenye mpopi (afyuni) ambayo inatia ganzi na hutumiwa kwa kutuliza maumivu na kuleta usingizi, pia hutumika vibaya kama dawa ya kulevya.
Kinachodhihiri ni kuwa neno *afyuni* ( *soma: afyuunun/afyuunan/afyuunin افيون*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *afyuni* halikubadili maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda