01-18-2022, 05:14 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHERA/AKHERA'
Neno *ahera/akhera* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/-zi*] yenye maana ya:
1. Mahali panapoaminiwa kuwa ndiko roho za wafu zinakoenda.
2. Maskani ya roho za wanadamu baada ya mauti/kifo.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ahera/akhera*( *soma: aakhiratun/aakhiratan/,aakhiratin آخرة )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:
1. Kinyume cha Dunia. Kuna aya katika Qur'aan Tukufu isemayo: "Miongoni mwenu wapo wanaoitaka Dunia, na miongoni mwenu wapo wanaoitaka Akhera." (Qur'aan Tukufu, Sura ya 3 (Surat Aali Imraan, Aya ya 152).
2. Kinyume cha mwanzoni; mwishoni.
3. Maskani ya roho za wanadamu baada ya kifo.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *aakhira* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa limezoeleka kutamkwa *ahera* na *akhera* likibeba maana moja ya maskani ya roho za wanadamu baada ya kifo.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda