MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU'

Neno *kuntu* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Kihisishi:* Neno linaloonyesha ukubalifu wa moja kwa moja katika moyo wa mtu; sawasawa, barabara, hasa. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. *Kielezi:* Sawasawa, bila ya shida yoyote. (Chanzo: Kamusi ya Karne ya 21).

3. *Kielezi:* Kwa ufupi, kweli, hakika; hasa; kabisa; ndivyo. (Chanzo: Kamusi Teule ya Kiswahili).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *kuntu *(soma: kun + tu  كنت* ) ni kitenzi cha Kiarabu cha wakati uliopita *fiilu maadhwi فعل ماض* kwa nafsi ya kwanza, chenye maana ya:  nimekuwa/nilikuwa.

Kitenzi hiki kimenyumbulika kutokana na kitenzi cha Kiarabu *kaana كان* amekuwa/alikuwa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *kuntu كنت* lilipoingia katika  Kiswahili lilipewa kategori ya kihisishi/kielezi na kupewa maana mpya tofauti na maana yake ya awali katika lugha ya Kiarabu ya kuwa kitenzi chenye maana ya: nilikuwa/nimekuwa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)