MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'HALMASHAURI'

Neno *halmashauri* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kikundi cha watu waliochaguliwa au kuteuliwa kufanya kazi ya kuwa watawala, watunga sheria, washauri au kuelekeza jambo fulani.

2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* chombo cha kiutawala katika wilaya au mji.

2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kundi la watu waliochaguliwa au kuteuliwa kuelekeza utendaji wa shughuli fulani.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *halmashauri* ni naneno mawili ya Kiarabu yaliyowekwa pamoja; neno *ahlu* (soma: *ahlu/ahla/ahli اهل)* lenye maana ya *watu, -enye,* na neno *mashauri* (soma:*mashuuratun /mashuuratan/mashuuratin* *مشورة* ) pia *mash-wara* (soma: *mash-waratun/mash-waratan/mash-waratin مشورة)* lenye maana zifuatazo:

1. Kinachotolewa nasaha kwa rai au namna nyingine.

2. Ushauri.

3. Nasaha, muongozo.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno haya mawili *ahlu mashuurat/mash-warat*  yaliipoingia katika Kiswahili na kutoholewa,  neno jipya la Kiswahili *halmashauri* lilipatikana.

Katika lugha ya Kiarabu neno *shuuraa شورى* linatumika kwa kisawe cha maneno *mashuurat مشورة* na *mash-warat مشورة* na hupatikana misamiati *ahlu al-shuuraa* (soma: *ahlush shuraa اهل الشورى washauri)* na *majlis al-shuuraa* (soma: *majlisush shuraa مجلس الشورى baraza la ushauri; bunge).*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)