VITENDAWILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: VITENDAWILI (/showthread.php?tid=961) |
VITENDAWILI - MwlMaeda - 08-21-2021 Vitendawili ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi lisilo wazi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huulizia swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti, harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitajika kufikiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa la neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalum kulingana na jamii yake. Sifa za Vitendawili
Aina za Vitendawili a) Vitendawili sahili ni vifupi na huwa na na muundo mwepesi kueleweka. K.v. b) Vitendawili mkufu huwa na vipande vinavyofuatana na kila kipande huwa na uhusiano na kipande kilichotangulia. Mfano “ nikisimama anasimama, nikiketi anaketi, nikiondoka huondoka pia c) Vitendawili vya tanakali hutumia tanakali za sauti Mfano: Prrrrrrh mpaka ng'ambo “ buibui; huku ng'o na kule ng'o. d) Vitendawili sambamba huwa na maelezo marefu (kama hadithi fupi) halafu jibu lake huwa ni refu pia (kama mafumbo) Umuhimu wa vitendawili
|