SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 04** - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 04** (/showthread.php?tid=959) |
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 04** - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU “ **SEHEMU YA 04**
Nyumbani kwa kina
Njoshi; Jua likiwa tayali
linazama, huku sauti za ndege zikipungua na kuufanya mji wa Mwamutapa kuwa kimya.Ukimya huo unatokea pia katika nyumba ya kina Njoshi, ukimya unatawala tofauti na siku zote, kwani familia ilibakiwa na mtu mmoja tu,ambaye ni mama yake Njoshi huku mwanae akiwa hajarudi kutoka kwa mfalme. Akiwa ameketi barazani, nje ya kibanda chao cha udongo, kilichoezekwa kwa nyasi, aliendelea kupunga upepo huku akiwa na huzuni sana, “Siamini,hatimaye
leo hii nimebaki peke yangu, sina cha kufanya ndio tayali imeshatokea ……,eeeh mizimu ya babu zangu mlindeni mwanangu ” ,mama Njoshi aliongea peke yake kwa huzuni huku akinyanyuka sehemu aliyokuwa ameketi, na kisha kuelekea ndani kulala, hakuwa na njinsi kwani aliona kuketi pale nje kulizidi kumuongezea machungu. Ikulu kwa mfalme;
Giza likiwa tayali limeshaingia huku,
ukimya ukiwa umetawala katika ngome ya mfalme. Kijana Njoshi anamfuta machozi Grace, huku akiwa amemkumbatia, “Usijali Grace,
naamini nitarudi salama ndani ya siku tatu “,Njoshi alimtoa hofu binti mfalme, msichana aliyempenda sana, na aliamini atamuoa atakaporudi kutoka katika msitu hatari wa majini, msitu ambao aliambiwa na mama yake hana budi kwenda huko, kwani huko ndiko angeupata ufalme na ukombozi wa Mwamutapa. “Sawa Njoshi,
nakuamini wewe ni shujaa, nakuombea kwa mizimu yetu, urudi ukiwa mzima “,Grace aliongea kwa huzuni huku akitoka mikononi mwa Njoshi aliyekuwa amemkumbatia, na kumruhusu kuianza safari yake haraka sana, kwani alitakiwa kuondoka usiku huo. Na bila kupoteza muda, kijana shupavu na hodari, kijana pekee aliyeogopwa na askari pamoja na mfalme Mutapa kutokana na uhodari wake wa kupambana, anatoka katika ngome ya mfalme iliyojengwa kwa ukuta mrefu, huku wafanyakazi pamoja na familia nzima ya mfalme wakimtazama na kumtakia kila laheri katika safari hiyo, bila kutambua kuwa Njoshi alikuwa na malengo yaliyompeleka msituni huku swala la kuchukua jeneza la ajabu, likiwa la ziada tu. Mwamutapa
Kijana ambaye alikuwa ni rafiki yake
Njoshi, urafiki ambao ulitokana na kijana huyo kuokolewa katika kipigo kizito kutoka kwa askari wa mfalme, mara tu alipofanya kazi asubuhi mpaka jioni katika shamba la mfalme, na pale alipojaribu kudai haki yake, askari wale walimnyima pesa, jambo ambalo kijana yule alishindwa kulivumilia, alijikuta akilusha ngumi, na kuambulia kipigo kikali kwani asingeweza kuwashinda askari zaidi ya kumi, huku yeye akiwa mmoja tu, lakini bila kutegemea ghafla alishangaa, askari wale wakipigwa mateke ya haraka haraka na kutimua mbio. “mimi naitwa
Njoshi, na pole sana ndugu yangu, hawa ndio askari wetu, inatakiwa tuungane kuitafuta haki “,kijana yule aliikumbuka sauti ya mtu aliyemsaidia kutoka mikononi mwa askari wa mfalme, ikijitambulisha na kisha kumuomba waungane katika harakati za ukombozi wa Mwamutapa. Na huo ndio ukawa mwanzo wa urafiki wao, urafiki ambao umedumu kwa muda mrefu na wamekuwa kama ndugu sasa. “Inabidi kesho
niende kwao nikamuone rafiki yangu, tangu jana sijaonana naye “,rafiki yake Njoshi, aliyejulikana kwa jina la Ngesha, alizungumza peke yake huku akijifunika shuka lake na kisha kuuchapa usingizi, bila kutambua kuwa muda huo ambao yeye analala, rafiki yake yuko safarini bila kujali giza wala hatari yoyote usiku huo, akielekea katika msitu wa majini, msitu ambao ulipatikana umbali wa kilomita arobaini kutoka katika makazi ya watu wa Mwamutapa. Msitu wa majini;
Tangu asubuhi tetemeko lilipotokea, na
“Aiweeeh jinimalikia kutangaza hali ya hatari katika msitu, mitego ya kila aina iliweza kutegwa katika kila njia ya kuingilia msituni, huku jeshi la msituni likiwa tayali limeshika dhana mbalimbali za kivita ikiwemo mishale, na kuuzunguka msitu wote. mweupe, kiongozi wa askari wangu wa msituni, adui wetu yuko njiani anakuja, nakuomba jiandae kwa mapambano, uko huru kutumia nguvu za kichawi na kijini ulizonazo “,malikia alimpatia taarifa mkuu wa jeshi lake la ulinzi msituni, na haraka bila kupoteza muda alitoweka mbele ya uso wa malikia, kwenda kutekeleza amli aliyopewa ya kudumisha ulinzi kila kona ya msitu, na kujiandaa kwa ajili ya kulipiza kisasi. |