SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 07* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 07* (/showthread.php?tid=956) |
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 07* - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU “ **SEHEMU YA 07*
Mwamutapa;
Mama yake Njoshi akiwa mwenye huzuni,
huku mawazo mengi kuhusu mwanae, yakishindwa kumtoka kichwani mwake. Anachukua jembe lake, pamoja na kikapu na kisha kuanza safari kuelekea shambani, lakini pia kitendo cha Ngesha kuondoka bila kumuaga na kushindwa kutambua mahali alipoelekea ghafla . Kilizidi kumwongezea maswali, kwani alihisi kuna jambo ambalo Ngesha alitaka amweleze Njoshi, jambo la muhimu sana, na ndio maana alishtuka baada ya mama yake Njoshi kumweleza kuhusu mahali ambapo Njoshi alielekea,kitendo kilichomshitua rafiki yake,na kisha kuondoka haraka sana bila hata kuaga. “Labda kaelekea
kwa mfalme kuangalia usalama wa rafiki yake,lahasha!,si angeniambia tu kuwa anaelekea huko,”mama yake Njoshi alizungumza peke yake,huku akiwa njiani kuelekea shambani,akiwaza na kuwazua kitendo cha rafiki yake mwanae ,kuondoka ghafla bila hata kumuaga. Msitu wa majini;
Njoshi akiwa na hofu,huku akitetemeka
mithili ya mtu aliyenyeshewa na mvua ya masika,mnvua inayoandamana na baridi kali.Alinyanyuka kutoka mahali alipokuwa amejificha,huku akiwa haamini,kama kweli kundi lile la askari hatari wa msituni walimpita bila hata kumwona ,na kisha kutokomea upande mwingine wa msitu,kwenda kumtafuta. “Hapa ngoja nipite
upande mwingine nielekee kwenye ngome ya malikia,lazma leo nifanikishe misheni yangu na kisha kesho nirudi nyumbani”,Njoshi aliongea peke yake kama kichaa,na kisha kushika panga lake,ambalo tayali alikuwa amelitelekeza chini bila kujitambua,kutokana na hofu aliyokuwa nayo kipindi akiwashuhudia askari wale wa msituni,wakipita mbele yake. “Eeeeh mizimu wa
mababu,niokoeni na balaa hili kijana wenu”,Njoshi aliomba mizimu huku akifumba macho yake kwa dakika chache,na kisha kutamka maneno ya kitamaduni bila kutoa sauti,na baada ya sala hiyo,Njoshi alitokomea kuingia ndani kabisa ya msitu,kwa kupitia upande mwingine tofauti kabisa na upande ambao jeshi lililokuwa likiongozwa na jini mweupe,waliweza kuelekea huko. “Miii……zi…mu
niokoeniii……na ku…faaa!!”, zilikua ni kelele za Njoshi ghafla,kwani sehemu aliyokuwa akipita,ni kama vile aliruka mkojo na kukanyaga mavi,kulikua na shimo ndefu sana kuelekea chini, likiwa limetegwa huku juu kukiwa kumefunikwa na fito nyembamba kama kuni,ambazo zingevunjika pale tu mtu atakapozikanyaga .Pia fito hizo zilifunikwa na majani makavu pamoja na udongo,kiasi kwamba mtu asingeweza kugundua kitu chochote,bali sehemu hiyo ilionekana kuwa kama njia nyingine,kwani kulikuwa hamna tofauti yoyote ile. Mtego huo kweli
ulifanikiwa kumnasa Njoshi,ujanja wote aliokuwa nao,pamoja na uhodari,uliweza kumwishia,na kumfanya kuwa mpole,tangu alipoikanyaga ardhi ya msitu wa majini.Alijilaumu sana kupita njia ile ,njia ambayo ilionekana kupaliliwa vizuri bila kutambua kuwa katika njia hiyo kulikuwa na mtego wa shimo uliotegwa na kisha kufunikwa na udongo. “Pwaaaaah…………”,ilikua
ni sauti ya maji mengi ikimpokea Njoshi,baada ya kusafiri umbali wa kama mita mia mbili kwenda chini,sawa na urefu wa viwanja viwili vya mpira wa miguu. “Duuuh kweli leo
nimepatikana,lakini mimi nishujaa,kwa vyovyote vile lazima niishinde vita hii”,Njoshi aliongea maneno ya kishujaa na kujipa moyo,huku akiziba pua yake kutokana na harufu kali ya maji yale yaliyoonekana kuwa machafu sana,maji yaliyomfika Njoshi kifuani mwake “Mungu wangu!,nini
tena hiki……yalaa……aaa”,.Njoshi alipigwa na butwaa,huku sauti kubwa ya hofu ikimtoka kinywani mwake,kwani alipojaribu kupapasa maji yale kwa kutumia mkono wake,alijikuta ameshika kichwa cha binadamu kilichokuwa kimeliwa na kuoza vibaya,kitendo kilichomfanya akitupe haraka sana na kisha kupiga kelele kutokana na hofu kubwa aliyokuwa nayo. Ikulu kwa mfalme;
Ikiwa yapata mida kama ya saa nne
asubuhi,Ngesha anafanikiwa kutoboa tundu,baada ya tofali moja kupasuka na kuachia nafasi katika ukuta uliozunguka ngome ya mfalme,nafasi hiyo iliweza kuonesha kila kitu kilichoendelea ndani ,kama mtu akiweza kuchungulia. Kijana Ngesha baada ya
kuangalia huku na kule,na kugundua kuwa hakuna mtu yeyote aliyekuwa akimtazama,tofauti na siku zote kwani walinzi wa mfalme walizunguka muda wote,kuhakikisha hakuna mtu yeyote aliweza kuusogelea ukuta huo. “Duuuh leo,pako
shwaliii,kulikoniii??,yaani hamna hata wale mbwa wanaojiita askariii “,Ngesha aliongea maneno ya kejeli huku yakiwa na mshangao ndani yake,na bila kupoteza muda aliweza kuchungulia ndani ya ngome ya mfalme,ngome ambayo ilijitenga mbali kidogo na makazi ya watu,huku msitu mdogo ukiizunguka ngome hiyo,na haikuruhusiwa mtu yeyote kuuvuka msitu,na kisha kuisogelea ngome hiyo bila sababu maalumu,ukikamatwa adhabu ilikuwa ni kifo tu na sio kitu kingine. Kutokana na sheria
hiyo,watu wengi waliogopa sana kuisogelea ngome ya mfalme,na ndio maana Ngesha alifanikiwa kutazama ndani bila kuonwa na mtu yeyote,baada ya kujidhihirisha kuwa askari hawakuepo eneo lile. “Aiweeeh……mizimu
wa mababu,mbona watu wanalia!!,mbona Njoshi simuoni,mmmh mfalme kafa???” maswali mengi yalimuandama Ngesha, mala tu baada ya kuchungulia ndani ya ngome ya mfalme,alishangaa kuona familia yote ya mfalme ikilia sana,wake kwa waume,wakubwa kwa wadogo.Lakini pia alipojaribu kuangaza vizuri kila kona,hakuweza kumuona Njoshi,hali iliyomfanya azidi kupigwa na butwaa. Lakini bila kutegemea, kuna jambo kubwa sana lilimshitua kuliko yote, alishangaa kumuona binti mfalme, na si mwingine, alikuwa ni msichana Grace, msichana ambaye rafiki yake Njoshi alimpenda sana, akilia kwa kwikwi huku akimtazama mfalme aliyeonekana kulala bila kumjibu chochote kile. Grace alitamka maneno ya kumtaka baba yake asife, na kumwacha akiwa hana baba, kitendo kilichomfanya Ngesha kushtuka, kwani hakuona sababu ya kumfanya mfalme afe haraka sana kiasi hicho. “Mmmmh au ndio
maana mfalme haonekani mtaani, na imepita mwezi sasa, manyanyaso yamepungua, lakini kwanini baba yake Njoshi kauawa?, sababu ilikuwa nini nini?, inawezekana kweli mfalme kafa, ngoja nielekee shambani kwa mama yake Njoshi nikampatie taarifa hii, ninaweza kutambua kitu fulani “,Ngesha aliahirisha kuchungulia ndani kwa mfalme, na kisha kufunga safari kuelekea shambani kwa kina Njoshi, huku maswali lukuki yakimsumbua bila kuwa na majibu yoyote ya maswali hayo. Shambani kwa kina
Njoshi; Mama yake Njoshi akiwa amejipumzisha
“Eeeeh mizimu yachini ya mti wa maembe, mti pekee uliopatikana shambani kwake, aliendelea kula chakula chake taratibu, huku akishushia na maji kwani tayali ilikua imeshafika saa sita, mida ambayo tayali jua lilikuwa limechanganya vilivyo na kuwa kali sanaa. mababu, muokoeni mwanangu “,ilikua ni sauti ya mama yake Njoshi akimuombea mwanae kwa mizimu, iweze kumpatia msaada, kwani kutokana na uwezo wa kitabiri pamoja na uganga ambao mumewe alimrithisha, aliweza kutambua kuwa mwanae yuko hatarini, tena hatari kubwaa, baada ya ndege aliyekuwa juu ya mti ule wa maembe, kumnyea na kisha kinyesi chake kudondoka katika matiti ya mama yake Njoshi. Mama yake alikitafakali kitendo kile, na kugundua kuwa ilikuwa ni kama ujumbe kwake, kuwa mtu aliyenyonya maziwa kutoka katika matiti yake, yuko kwenye shida na matatizo, huku kinyesi cha ndege yule kikisimama kwa niaba ya matatizo yanayomsibu mwanae. Utabiri ambao ulikuwa sahihi, kwani wakati huo Njoshi alikuwa ndani ya shimo kubwa msituni, huku akisubili kukamatwa na majini hatari wa msituni. |