SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” **SEHEMU YA 06* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” **SEHEMU YA 06* (/showthread.php?tid=950) |
SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO ” **SEHEMU YA 06* - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI : “MAPIGO YA MOYO “, **SEHEMU YA 06*
Gari dogo aina ya Noah linapaki nje ya uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere ,ni baada ya safari ndefu yenye foleni ya magari mengi sana lakini hakuna chochote ambacho kiliweza kuhalibika.
“Ok goodbye mr Rodgers!, wahi ndege yaaani dakika kumi tu zimebaki ndege iweze kuondoka, foleni ya Morogoro road kidogo itucheleweshe kabsaaa! sunajua Mbezi mpaka hapa kwa mida hii ya jioni lazima jasho likutoke ……”,mzee Jastin alimkabidhi begi kijana wake wa kazi, huku akilaumu foleni ya magari, foleni ambayo iliweza kuwachosha sana na ilikuwa imebaki kidogo tu waweze kukuta ndege imeondoka.
“Sawa bosi, nikifika kisauni Mombasa ……nitakupigia simu, ngoja niwahi ndege “,ilikua ni sauti ya Rodgers, akipokea begi lake kutoka kwa bosi wake na kisha kuelekea sehemu ya abiria waliokuwa wakisafiri, tayali kwa ajili ya kuondoka haraka sana Dar es salaam.
********
Jumba kubwa la kifahari, jumba ambalo lilikuwa limezungukwa na ukuta mrefu sana kiasi kwamba nyumba ilikuwa haionekani kutokana na kuzuiliwa na ukuta,lilikuwa kimya sana huku sauti pekee za mbwa ndizo zilikuwa zikichangamsha mji huu.Nyumba hii ilimilikiwa na mfanyabiashara maarufu sana, si mwingine bali mzee Jastin.
“Karibu nyumbani kipenzi changu “,Rose aliongea huku akinikalibisha ndani, nyumba ambayo ilikuwa mala yangu ya pili kuikanyaga, japokuwa siku zote sikuweza kumkuta mzee Jastin, mzee ambaye sijui angenifanya nini kama angenikuta ndani kwake.
“Asante mpenzi!, nimekalibia “,niliongea huku nikiketi na kuangaza kila kona ndani ya jumba lile, jumba ambalo sikuweza kuuzoea uzuri wake, hivyo ilikua ni jambo la kawaida kulishangaa.
“Rose naomba nikuulze kitu! Utanisamehe kama nitakuwa nimekosea kukuulza swali hili ……”,niliongea huku nikijiweka tayali kwa ajili ya kumuulza swali Rose, bila kutambua kuwa nilikuwa hatarini kwani mzee Jastin alikuwa njiani akija nyumbani kwake baada ya kutoka kumsindikiza Rodgers.
“Hivi ulikusudia kunigonga na gari! “,ilibidi niulize swali ambalo sikuzote lilizunguka kichwani kwangu, na kila nilipokuwa nikitaka kumuulza swali hili Rose, roho yangu ilisita kwani sikupenda kumchukiza Rose, msichana mrembo ambaye ilinigharimu sana kumpata!
“Sina budi kukwambia ukweli Robert ……! Nilikugonga na gari kwa makusudi ili nikuue kabisaa, awali nilikuwa sikupendi na nilikuchukia sana………lakini kwa msaada wa wananchi walioshuhudia tukio walitaka kunishambulia nilipotaka kutoweka, ikabidi nirudi kukuchukua na kukupeleka hospitali “,Rose aliongea kwa huzuni sana, huku akionekana kujutia kitendo alichonifanyia. Lakini kwa upande wangu mapenzi yalitoweka ghafla! mala tu baada ya kuniambia alitaka kuniua, niliona ilikuwa ni kweli kwani nilimfuatilia muda mrefu sana lakini sikuwa na bahati ya kupendwa, zaidi ya kuambulia mateso tu!
“Kwanini ulitaka kuniua?, nilikukosea nini ?”,niliongea huku nikiwa nina hasira, sikutaka kukaa tena mahali pale kwani niliona yote Rose aliyokuwa akinifanyia alikuwa kama anajilazimisha tu kunipenda, na pengine inawezekana alikuwa na lengo baya juu yangu.
“Nilipokuwa chuoni nilimpenda sana Peter ……,lakini Peter alikuwa akiniambia kuwa hawezi kuwa na mimi kwasababu alizani mimi na wewe ni wapenzi,hivyo siku zote nilikuchukia kwani nilikuona wewe ndiye chanzo cha mimi kumkosa Peter”Rose aliongea huku akipiga magoti, lakini sikujali! Niliona kama alikuwa akiniigizia tu.
“Vipi kuhusu Jacob! ” ,niliendelea kumswalisha Rose, na bila shaka aliweza kutambua kuwa nilikuwa nimechukia. Sikuwa na hofu, kwani ningeweza kuondoka sehemu yoyote na kuishi kwani nilikuwa nimepatiwa pesa nyingi sana na mheshimiwa raisi.
“Kuhusu Jacob, sikumpenda!, nililazimishwa tu na baba! .Nisamehe Rose lakini sasa hivi nakupenda kwa dhati, umevumilia mengi sana lakini hukusita kunipenda! Ndio maana najutaaa makosa yangu”,Rose aliongea mpaka nikaanza kumuonea huruma, kusema ukweli nilimpenda sana msichana huyu. Hivyo kitendo cha kumuona akianza kulia, ikabidi nipunguze hasira na maswali ambayo nilikuwa nazidi kumuuliza Rose.
********
Vyombo vya habari vinatangaza juu ya kutafutwa kwa muhusika aliyehusika na mauaji ya Jacob, televisheni ziliweza kuonesha picha za muuaji lakini stesheni za radio nazo hazikupitwa na taarifa hii, zilielezea muonekano wa muuaji vizuri sana kiasi kwamba hakuna mtu yoyote ambaye angeshindwa kumtambua muuaji kama angekutana naye uso kwa uso.
Mzee Jastin akiwa amekamatilia uskani wa gari yake, aliona kama gari halikimbii. Kwani alikuwa na haraka sana baada ya kusikia taarifa ya habari kupitia radio yake, alikuwa anawahi nyumbani kwake eneo la Temeke kwa ajili ya kufanya jambo fulani ili kumuokoa Rodgers asiweze kukamatwa mala atakapofika Mombasa.Kwani alitambua kuwa Rodgers kafanikiwa kutoka Dar es salaam salama, kwani kipindi anaondoka na ndege, taarifa ya habari ilikuwa bado haijatangazwa.
“Inatakiwa nimtarifu haraka sana Okumu, aweze kutuma vijana uwanja wa ndege wakampokee, lakini simu imezima chaji!,sina jinsi zaidi ya kuwahi nyumbani ……”,Jastin aliongea huku akiikanyaga mafuta gari yake, na kila taa nyekundu zilipowaka muda mwingine hakuweza kusimama kwani aliona kama Rodgers alikuwa muhimu sana kuliko faini atakayolipa kama trafiki wakimtia mikononi.
********
Japokuwa taarifa ya habari haikuweza kuwafikia abiria waliokuwa ndani ya ndege, huku simu zao zikiwa zimezimwa. Lakini Rodgers machale yaliweza kumcheza, alihisi jambo baada ya kumuona askari mmoja akikagua abiria mmoja baada ya mwingine. Hivyo ilibidi Rodgers atumie akili za kuzaliwa ili kukwepa kukamatwa na polisi yule aliyekuwa amevalia jezi zake huku picha ya Rodgers akiwa ameishika mkononi, alitazama sura ya abiria na kisha kutazama sura ya Rodgers.Bila shaka! alionekana kuwa na asilimia mia moja kuwa mtuhumiwa aliweza kuwemo ndani ya ndege ile.
Je Rose anampenda kweli Robert?
Rodgers atakamatwa ?
|