SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 12* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 12* (/showthread.php?tid=944) |
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 12* - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU “ **SEHEMU YA 12*
Mwamutapa;
Ngesha baada ya kufika nyumbani kwao na kumkuta mama yake akiwa anamsubilia huku hofu kubwa ikimtawala kwani alikuwa na hofu kuhusu usalama wa mwanae. Mama yake hakuamini pale tu Ngesha aliporudi nyumbani akiwa mzima wa afya, na alipojaribu kumuulza alikuwa wapi?, Ngesha alimsimulia mama yake kila kitu bila kuficha chochote kile. Kiasi kwamba kifo cha mfalme hakikuwa siri tena, kwani tayali Ngesha na mama yake walikuwa tayali wameshafahamu.
Kutokana na usiku kuwa tayali umeingia ,Ngesha na mama yake walipata chakula na kuelekea vitandani kujipumzisha, huku mama yake Ngesha akikosa usingizi kabisa mpaka kunakucha siku ya jumatano, kwani alikuwa na mawazo mengi kuhusu kifo cha mfalme, jambo ambalo aliweza kuambiwa na mwanae Ngesha.
Mwamuyeshi;
Mji ukiwa umechangamka sana huku shughuli mbalimbali hasa biashara zikiendelea,kwani ndio ilikua shughuli kuu katika nchi hii tofauti na nchi jirani ya Mwamutapa,kwani Mwamutapa walitegemea sana kilimo. Mganga maarufu katika nchi hii akiwa amepanda farasi wake, alijaribu kupenya katikati ya soko ambalo lilikuwa na watu wengi sana mida ya asubuhi. Soko hili lilikuwa limepakana na ikulu ya mfalme Muyeshi, kiasi kwamba njia pekee ya mkato kuelekea ikulu kwa mfalme iliweza kufurika watu na kuziba njia hiyo. Bila kukata tamaa, mganga yule alizidi kupenya katika kundi lile la watu na hatimae aliweza kufanikiwa, kwani alionekana kuwa na haraka sana.
Ikulu kwa mfalme Muyeshi;
Pilika pilika za hapa na pale zikiwa zinaendelea katika jengo kubwa la mfalme Muyeshi, huku vijakazi wa mfalme wakisafisha mazingira ya ikulu, katika asubuhi nzuri ya siku ya jumatano.
Mfalme Muyeshi akiwa ameketi nje ya jengo lake, huku akiota jua zuri la asubuhi. Alishashangaa kumuona mganga wake aliyemtegemea akifika ikulu, huku akionekana kuwa na jambo muhimu sana ambalo liliweza kumleta ikulu, bila kuitwa na mfalme.
“Aiweeh mfalme wangu Muyeshi, nimekuja haraka sana kwako, kuna tatizo “,mganga yule alimsalimu mfalme Muyeshi, huku akishuka juu ya farasi wake na kisha kumfahamisha mfalme kuwa kulikuwa na tatizo ambalo liliweza kumleta.
“Aiweeeh mganga wangu kipenzi, tatizo gani limekuleta kwangu asubuhi yote hii “,mfalme aliweza kumjibu mganga wake na kumpatia swali mganga yule.
“Rafiki yako Mutapa, mfalme wa Mwamutapa alifariki jana, lakini kifo chake sio siri tena, watu wake wameanza kufahamu “,mganga aliongea maneno ambayo yaliweza kumshitua mfalme, kwani mfalme aliweza kuitambua hatari ambayo ingemkuta rafiki yake baada ya kifo chake kufahamika, kwani hata jeneza la ajabu lipatikane lisingeweza kusaidia chochote kile. Bali mfalme Mutapa angekufa bila kufufuka tena, na huo ndio ungekuwa mwisho wa utawala wake.
“Ondoka haraka sana, nenda kazuie hili jambo lisiweze kutokea, nenda katoe taarifa ikulu kwa mfalme Mutapa, ili wote wanao ifahamu siri hii waweze kuuawa haraka sana “,mfalme aliongea na kisha kutoa askari kumi wenye farasi ili waweze kumsindikiza mganga yule na kumpatia ulinzi wakati wote, na bila kupoteza muda, kundi la watu kumi na moja walianza safari kuelekea nchi jirani ya Mwamutapa haraka sana.
Msitu wa majini;
Mapenzi bwana, ni kitu cha ajabu sana. Huwezi amini, malikia wa majini alishindwa kupata usingizi usiku uliyopita, alizunguka huku na kule katika ngome yake huku akimtazama Njoshi aliyekuwa amepoteza fahamu huku akiwa amefungwa kwenye mti wa mateso. Alitamani amuone Njoshi akifumbua macho, lakini Njoshi alizidi kuyafumba macho yake mithili ya mtu aliyefariki dunia. Lakini fikra za malikia zilikwenda mbali sana, kiasi kwamba alitamani kumtoa Njoshi katika mti ule, lakini moyo wake ulisita, lakini aliapa kumtoa katika mti ule asubuhi siku iliyofuata siku ya jtano.
“Lazima nimtoe hapa alipo, siko tayali kuumia wakati mwenye maamuzi ni mimi “,malikia aliongea huku akimalizia kuwatoa nge na siafu kwa kutumia kijiti katika mwili wa Njoshi, na kisha kuelekea chumbani kwake kupumzika.
Jua likichomoza vema na kuufanya msitu wa majini kuonekana vizuri sana, huku rangi ya kijani ya miti ikipendeza na kuvutia machoni kwa ndege pamoja na viumbe wote wa msituni. Malikia alikuwa wa kwanza kusikia sauti nzuri za ndege zikifurahia maua katika ngome yake, na jambo la kwanza aliweza kuamka na kwenda kumtazama Njoshi.
“Mhhh kaenda wapi tena?, au ametoroka “,ilikuwa ni sauti ya mshangao kutoka kwa malikia, msichana pekee katika msitu wa majini. Kwani majini wote wa kike waliweza kutoweka baada ya mfalme kushindwa kutimiza laana yake.kwani alimkamata malikia akifanya mapenzi na jini mwingine wa msituni tofauti na yeye, kutokana na hasira mfalme aliapa kumuua malikia huyo lakini hasira zilipopungua alishindwa kufanya hivyo kwani alimpenda sana japokuwa alimsariti, Kutokana na miiko ya majini hao wa msituni,kwani kiongozi wao anapotamka jambo lazima alitimize. Wanawake wote msituni pamoja na mfalme waliweza kutoweka ,na kumuacha malikia akiwa mwanamke pekee wa kijini msituni.
Hali hii ilipelekea malikia kumchagua jini yoyote wa kiume wa kulala naye, pale tu alipokuwa na hisia za kufanya mapenzi. Kwani tayali mume wake ambaye alikuwa ni mfalme wa msituni, alikuwa hayupo tena.
Kwa upande wa majini wa kiume, baada ya kutoweka kwa wake zao, walijikuta wakijaribu kumbaka malikia baada ya kushindwa kuzuia hisia zao na kuambulia kuuawa na malikia, kwani alikuwa na nguvu sana kuwashinda. Hivyo basi, kuchaguliwa na malikia kulala naye lilikuwa ni kama jambo la bahati kwa majini wa kiume, na wengi waliomba mizimu waweze kuipata bahati hiyo bila mafanikio.
“Wote poteeni muelekee msituni, adui katoroka “,malikia alitoa amli baada ya majini wote wa msituni kukusanyika. Huku yeye akiwa ametoka ndani kwake kukagua mali zake, kwani baada ya kukuta Njoshi hayupo katika mti wa mateso. Aliamua kuelekea ndani kukagua mali zake na kukuta fimbo ya kifalme ikiwa imeibiwa, lakini mkanda pamoja na panga vilikuwepo kwani vilifichwa sehemu ambayo haikuwa rahisi kuviona. Malikia aliamini Njoshi hatafika mbali ,kwani alikuwa na majeraha makubwa na pia hakuwa na siraha yoyote ya kumlinda.
Ngesha na mama yake, pamoja na mama yake Njoshi, watauawa?? Kwani ndio wanajua siri ya mfalme …
Njoshi kaelekea wapi?
Tukutane sehemu ya 13
|