MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

HEKAYA ZA ABUNUWAS >>> KISA CHA SULTANI NA MVUVI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
HEKAYA ZA ABUNUWAS >>> KISA CHA SULTANI NA MVUVI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48)
+---- Thread: HEKAYA ZA ABUNUWAS >>> KISA CHA SULTANI NA MVUVI (/showthread.php?tid=939)

HEKAYA ZA ABUNUWAS >>> KISA CHA SULTANI NA MVUVI - MwlMaeda - 08-20-2021

HEKAYA ZA ABUNUWAS  >>> KISA CHA SULTANI NA MVUVI
ALIKUWAKO Sultani katika nchi ya Ajemi. Siku moja akaenda kutembea pwani pamoja na Waziri wake. Wakamkuta mvuvi anatengeneza mishipi yake tayari kwenda baharini. Na siku hiyo bahari imechafuka vikubwa, na upepo unavuma mtindo mmoja. Sultani akamwita mvuvi, ya mvuvi! Akaitikia, naam Maulana. Akanena palipo wanne, na wanne, hawakifu wanne? Mvuvi akajibu, hawakifu wanne, bwana. Sultani akamwuliza, unamtumikia mtu au unaitumikia nafsi? Mvuvi akajibu, naitumikia nafsi. Sultani akanena, ya mvuvi Halla! Halla! Mvuvi akasema, mimi mchokozi bwana, namjua pweza alipo.
Sultani na waziri wakashika njia kurudi mjini. Njiani Sultani akamwambia Waziri, umefahamu maneno yale niliyosema mimi na mvuvi? Akasema, la sikufahamu. Akamwambia, wewe Waziri mzima usifahamu maneno yale, akayafahamu mvuvi. Sharti unifahamishe. Akamshika Waziri hata asiwe na raha. Waziri akanona hana njia ila amtafute yule mvuvi amwulize. Akamwita kwake. Akamwambia nataka namaa ya maneno yale uliyosmea na Sultani pwani? Mvuvi akamwambia, sijui mana yake, mimi nimejisemea tu. Akamwambia, tafadhali niambie nitakupa reale miteen. Mvuvi akasema, sijui. Akamwambia, nitakupa reale hamsini mia. Mvuvi akasema, bwana wangu sijui fasiri yake. Akamwambia nitakupa shamba langu la mahali fulani. Akanena, bwana sijui. Hata mwisho akamwambia, nitakupa hii nyumba yangu ninayokaa. Mvuvi akamwambia, niandikie hati ya mkono wako bwana, akamwandikia.
Akamwambia, sasa nitakueleza. Sultani aliniambia, palipo wanne, na wanne, hawakifu wanne. Maana yake Sultani aliona ile dhoruba iliyokuwapo, akaona ajabu kuniona mimi natengeneza nyavu kwenda baharini. Ndipo akaniambia wewe katika mwaka kuna miezi, miezi minne ya kaskazi ndio wakati wa uvuvi wa samaki, kuna miezi minne ya maleleji ndio wakati wa bahari kuwa shwari. Basi miezi hii minne huwezi kupata samaki wa kutosha kuweka miezi hii minne ya kusi? Na mimi nikamwambia, akiba ya miezi minane haitoshi kuwa akiba ya miezi hii minne ya kusi.
Waziri alipopata fasiri hii akatoka akaenda kwa Sultani. Akamwambia, nimekwisha pata fasiri ya maneno yako na mvuvi. Akamwambia nieleze. Akamweleza kama vile alivyoambiwa na mvuvi. Sultani akamwambia, umefahamu mwenyewe? Akanena, naam. Sultani akafurahi, akampa zawadi. Baada ya siku si nyingi Sultani akapata habari kama mvuvi anakaa katika nyumba ya Waziri. Maneno haya yakaenea katika mji. Hata Sultani akataka kujua maana yake. Akamwita mvuvi, akamwuliza amepataje kuwamo katika nyumba ya Waziri. Akamwambia, nyumba ni yangu sasa si ya Waziri. Akamwuliza, imepataje kuwa yako? Akanena, bwana unafahamu siku ile pwani uliponiambia, Halla! Halla! Nalifahamu kuwa umeniambia, usimpe rahisi. Name nikakuambia, mimi mchokozi, namjua pweza alipo.
Maana yake, mimi maskini najua njia ya kupata pesa. Sitamwambia ila kwa kupata faida kubwa. Na sasa nimepata faida, nakaa nyumba ya Waziri. Sultani alipoona kama Waziri wake amedanganya alikasirika sana.
Akamwita, akamwambia, umenidanganya kuwa umetambua kwa akili zako, kumbe! Umeambiwa. Basi sasa hufai wewe kuwa Waziri, umekuwa mwongo na mjinga. Huyu mvuvi ndiye atakayekuwa Waziri wangu. Mvuvi akawa Waziri, akastarehe siku zake zote.