SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 33 - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 33 (/showthread.php?tid=928) |
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 33 - MwlMaeda - 08-19-2021 SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 33
Baada ya mazungumzo yake kuisha katika ghafla ile iliyokuwa imeandaliwa na waziri Kabuziri kwakuweza kumteua Zaidu Sudaysi Zaidu kuwa kama balozi wa vijana.Yaani Zaidu Ndiye atakayekuwa kama mshauri wa Vijana mbalimbali katika nchi ya Kinani.Basi waandishi wa habari wakawa wako naye pembeni wakawa wanamhoji maswali mbalimbali.
Kwa ujumla vijana wengi haswa haswa wenye elimu yaani waliosoma hadi vyuo vikuu hujikuta sana kutaka Au kuwa na mawazo ya kuajiriwa japokuwa ana kiasi fulani cha Fedha kitakachoweza hata kumfanya msomi huyo kuanzisha mradi wowote wa halali kwaajili ya kumuingizia Hela.
Lakini unakuta kijana huyo yeye anakuwa ni mtu wa kutembea na bahasha za Kijani na nguo zilizopigwa pasi Kweli Kweli na kuingia katika ofisi mbalimbali ili kuweza kuomba Kazi.
Ila tukumbuke akili na kisukumizi chochote kile kinaweza kufanya mtu kuweza kuyabadilisha maisha Yake kwa sekunde chache sana.
Mabadiliko Hayo yanaweza kuwa ni mabadiliko ya faida au mabadiliko ya hasara.
Ikiwa ni kama mwaka mmoja Hivi na miezi kadhaa imeshapita.Ambapo tayari kwa kipindi hicho Zamda na Zaidu wameshapata mtoto mwingine ambaye alikuwa ni wa kiume. Mtoto huyo Kwakweli Kwa sura yake alifanana na baba yake Sana. Kwa jina aliitwa Rubai.
Basi siku hiyo Zaidu akiwa nyumbani hapo wakiwa pamoja na Zamda na Siku hiyo Jeni alikuja kuwatembelea hapo.Lakini Jeni akawa anataka kujua ni kwa nini Zaidu ameamua kumuita mwanaye jina lile kwamba awe anaitwa Rubai.
Basi mda huo ikiwa ni mishale ya saa tatu asubuhi wakiwa wamekaa hapo kila mtu kwenye kochi.Kuna meza inaonekana ina chupa ya chai ikionesha dhahiri shahiri kwamba ndiyo wametoka kupata kifungua kinywa mda si mrefu.
Basi mda huo Ndipo Sasa Zaidu akawa anatoa sababu za Yeye kuweza kumuita mwanaye kwamba aitwe Rubai.
Mda huo Zaidu anaonekana amejifunga taulo nyekundu huku akiwa amevaa tisheti nyeusi. Maongezi Yale ambapo kwanza Jeni alimuuliza hivi.
"Jeni akiwa amevaa suruali fulani hivi ya rangi nyeusi na tisheti ya bluu.Alisema ".Hivi Zaidu hili jina ulilomuitwa mwanao ulilipatia wapi?.Kwasababu sidhani hata kama Kwenye Ukoo wenu kama lipo hili jina.
Aaaaaa Kwakweli kila mtu huwa na maana Yake anapoamua kufanya jambo Fulani Ambalo liko katika akili yake Au liko la kuona kabisaaaa.
Ndiyo maana Yake.
Kwahiyo kuhusiana na hili jina Kwakweli ni kama Stori ndefu sana ila nitatumia kuelezea kwa ufupi Kidogo.
Haina shida chamsingi tuielewe Mimi na Bibiye Zamda Hapa.Au siyo Zamda.
" Zamda akamjibu Jeni kwakusema " Ndiyo maana Yake.
Basi tupe ufumbuzi kidogo kwa hilo jina.
Sawasawa. Aaaaa jina hili nimelipata kutoka katika kitabu Fulani hivi.
"Jeni akamkatisha maongezi Zaidu kwakumuuliza hivi". Umepata kwenye kitabu tena!!?.
Ndiyo maana yake eeeeeee kwenye kitabu.
Mhhh duuuuuu hiyo hatari tena.
Wala kawaida tu.
Ok tuambie sasa vizuri.
Aaaaaa kitabu hicho ni kitabu ambacho nilikisoma mwanzoni sana nilipokuwa naanza kutambua kipaji changu cha uandishi wa hadithi mbalimbali. Kitabu hicho ambacho kilikuwa ni cha Riwaya Kwakweli ilikuwa ni ndefu yenye kurasa takribani elfu moja kamili za kusoma.Mwandishi wake ni Hausteni Malubu Bizarre. Mwandishi huyu alikuwa ni mwandishi mashuhuri sana kwa kipindi hicho katika riwaya na ushairi.
"Jeni akauliza kwa mshtuko.Alisema Hivi".duuuuuuuuuuuu kurasa elfu moja kabisaaaaaaa?.
Ndiyo maana Yake.
Naukamaliza kabisaaaaaaa!!??.
Ndiyo maana Yake.
Mmmmh tupe Sasa Stori. Aaaà katika riwaya hii kuna mhusika ambaye alikuwa akiitwa Rubai.Alikuwa ni wa kiume .Ni mtoto pekee katika familia yao ambaye alizaliwa Wakati baba na mama wakiwa tayari wameshafanikiwa kimaisha. Kwasababu watoto wengine ambao ni wakubwa zake Rubai Walikuwa kama wawili hivi walizaliwa Wakati Mama na baba wakiwa katika shida sana Tena sana.
Kwahiyo Rubai akawa ni Kijana Mwenye kuwa na mapenzi sana ya dhati na wakubwa zake na pia Ndugu zake.Kwasababu Stori hii alikuja kupewa na mama yake Ambapo Kipindi hicho anahadithiwa hadithi hii alikuwa ameshafikisha umri wa miaka Kumi na Tano.Kwahiyo kama ni kujielewa alikuwa kabisaaaaaa anajielewa vizuri kabiaaaaaa.
Kwakweli Rubai kwa siku hiyo alivyoelezewa hadithi hiyo Kwakweli alilia Sana tena sana.Yaani haamini kabisaaaaaaa maisha ambayo wazazi wake Walikuwa wakiishi na wakubwa zake huyo Rubai.Lakini naye Rubai akamuahidi mama yake kwamba kwakusema Hivi"Mama nitasimamia kidete katika kuweza kuendeleza maisha yetu kuwa mazuri. Milele hatutarudi tulipokuwa .Wakubwa zangu nitakuwa nao pamoja milele daima katika nyanja zote.Nitasimama wima na Ndugu zangu kama mlingoti wa Bendera ya Taifa."
Kwakweli maneno Yale yalimpa nguvu sana mama yake.Nakweli kijana yule alikuja kufanikiwa sana na mwisho wa siku kabisaaaaaaa alikuja kuingia katika Mambo ya siasa.kwa Mara ya kwanza Kabisaaaa aliteuliwa kuwa kama waziri mkuu wa Taifa hilo.
Kwasababu Rubai alijitahidi kusoma sana na hadi akawa amesoma hadi elimu ya juu yaani chuo kikuu.Huko huko chuo kikuu ndipo alipoanza kupata jina kwelikweli.Mwisho wa siku kijana wa busara na vitendo hadi akafanikiwa kuingia ikulu.
Pia kipindi cha kampeni kilipofika akaamua kugombea nafasi ya urais katika Taifa Lao.Basi na mungu si Athumani nakweli Rubai akafanikiwa kupata nafasi ya urais katika Taifa Hilo. Aliweza kuongoza kwa mihula miwili kama ilivyo katika katiba yao inavyosema.kwakweli Rubai aliliongoza Taifa Hilo katika nyanja zote vizuri sana. Hadi wananchi walitamani aendeelee kuongoza tu.
Pia baada ya kustaafu katika uongozi Kwakweli alikuja kupewa tunzo kubwa Sana iliyokuwa ikijulikana kama TARU.
"Jeni akamuuliza swali hivi".inamaanisha nini Hiyo!!?.
Aaaaaaa, tunzo hii ilikuwa ni tunzo ya amani.Ambapo kirefu chake ni Tunzo ya Amani kwa Rubai.
Ahaaaaa, hapo nimekuelewa kabisaaaaaaa.
Sawasawa.Kwaujumla kuna tunzo nyingi sana alipewa ila hii Kwakweli ilikuwa ni tunzo ambayo ilimpa heshima kubwa Sana Tena katika Taifa lake na pia katika mataifa mengine.Kwasababu kwa kipindi cha uongozi wake nchi iliyokuwa ikiongozwa na Rais Rubai ilienda kwa amani sana Lakini mataifa mengine hayakuweza kumiliki amani kwa mda mrefu sana. Yaani kila siku ni machafuko tu kila kona.
" Jeni akauliza swali.Akisema'.Kwani tunzo hiyo nani Ndiye aliyempatia?.
Aaaaaa, kwa ujumla tunzo hiyo alipatiwa na Umoja wa Mataifa.
Ahaaaaa. Umoja wa Mataifa.
Daaaa Kwakweli ni pongezi kubwa Sana huyo mtu anatakiwa apewe.
"Zamda naye akasema hivi".Ni Kweli.
Kwasababu Kwanza katika uongozi wake ni uongozi ambao Kwakweli ulikuwa ni uongozi Kweli Kweli. Hadi wazungu huko Walikuwa wanamuita A Man of Action.
Kwahiyo Jamani ndiyo maana na Mimi nikaamua kumuita huyu mwanetu aitwe Rubai.
"Zamda akasema Hivi".Aaaaaaa kweli kwanza kwakweli mume wangu nikupe heko kubwa Sana ya kuweza kumkumbuka huyo mhusika katika riwaya Hiyo.
Shukrani sana mke wangu.
Kwasababu Kwakweli Natumai na mwanetu kuwa na jina kama hili aaaaaa kama ni kusadifu Kwakweli jina hili linasadifu yaliyomo haswaaaa. Rubai mtoto aliyezaliwa kutoka katika familia ambayo ilikuwa imetokea katika umaskini uliokisiri sana na baadae mungu si Athunani Mambo yanakuwa vizuri. Kwa ujumla umepatia sana kuweza kumuita Jina hili.
Sawasawa mke wangu.
" Jeni naye hakuwa nyuma katika kuweza kusema jambo naye la moyoni kuhusiana na Stori hiyo.Alisema Hivi ".Aaaaaaàaaa sawasawa ni vizuri kumuita Kweli hilo jina.
Sawa.Japokuwa nilipowaambia baba na mama kuhusiana na suala hili walileta kelele sana.
" Jeni akasema hivi".Ayaaaa .
Ndiyo hivyo. Hili si Jina kama la huko Asia hivi.
Ndiyo Ndiyo.
Lakini nikaamua kuongea nao vizuri sana na Hadi wakaja kunielewa vyema kabisaaaaaaa.
"Zamda akasema".Unajua mume Wangu jina la Babu kwamba ndiyo angeetwa huyu Kwakweli lisingenoga kabisaaaaaaa.
Ni Kweli mke wangu.Kwasababu hapa Mimi naitwa Zaidu Sudaysi Zaidu. Halafu tena mwanangu aitwe Zaidu Sudaysi Zaidu ndiyo maana nikasema hapa Sasa ni kama ndege kutua uwanja wa mpira kabisaaaaaaa.
Ni kweli mume wangu.
Ndiyo maana Yake.
" Jeni akasema Hivi ".ila daaaaaaa Zaidu nakupa hongera kubwa sana tena sana.
Shukrani sana haina shida Jeni.
Kwasababu Zamda kwakweli hapa umepata mume kabisaaaaaaa.
" Zamda akamjibu huku akiwa anacheka. Alisema hivi ".Haya Bana. ila ndiyo hivyo huyu ndiyo mume wangu Bwana Zaidu Sudaysi Zaidu. Namshukru sana Allah kwakuweza kukutana na mume kama huyu.
" Zaidu akasema Hivi ".Haya Bana.
Siku zikiwa zinazidi Kuyoyoma Kweli Kweli. Basi Siku hiyo ikiwa ni mishale Ya saa Kumi jioni siku ya jumapili hivi. Siku hiyo Zaidu alienda kumtembelea Jeni ambaye ni rafiki yake kipenzi sana. Nyumba ambayo alikuwa akiishi Jeni ni kwamba ni Zaidu Ndiye aliyemnunulia Nyumba hiyo.Yote hiyo ni Kwasababu tu ya misaada mbalimbali ambayo Jeni alikuwa akimpatia tangu kipindi hicho kabisa.
Basi mda huo maongezi yao yalikuwa hivi.
" Jeni akiwa amekaa kwenye kochi amejifunga kanga yake kama kawaida yake. Huku Zaidu akiwa amevaa suruali ya jinsi hivi na tisheti nyekundu hivi. Jeni alikuwa akisema Hivi ".Mmmh Zaidu Nakumbuka juzi uliniambia utakuja weekend hii kwa mazungumzo maalumu.
Ndiyo ndiyo.
Sawa karibu sana.
Duuuuuuuuuuuu naona unazidi kupapamba tu hapa au sio?.
Wala ila kawaida tu.Hii ni kawaida ya mwanamke tu.
Ni Kweli.
Yaani kawaida ya mwanamke kama Mimi lazima kujiongeza sana .
Ni kweli. Kwasababu kwa namna tulivyokuwa tumeinunua hii nyumba siyo kama Sasa kabisaaaaaaa. Kuna vitu vimeongezewa hapa Kabisaaaaaaa.
Ndiyo ndiyo.
Aaaaaa ni vizuri sana kabisa.
Asante.
Kwa ujumla lengo la kuja hapa leo hii jumapili ni kwamba nataka tuongee kidogo kuhusiana na Maendeleo ya biashara ambayo unashughulika nayo?.
Aaaaa kwanza tu Zaidu niseme nizidi kukupa shukurani kubwa Sana mda wowote kabisaaaaaaa.
Sawasawa Jeni.
Aaaaaa kwa ujumla kazi kule inaenda vizuri. Kwasababu kuna mabadiliko mbalimbali nimeyafanikisha kuyaona Tangu nianze huu mradi.
Ni vyema sana nani jambo la kumshukuru Mungu.
Ni Kweli. Unajua Jeni jambo langu ni kama lako na lako ni kama la kwangu isipokuwa baadhi ya Mambo tu.
Ni Kweli.
Kwahiyo Ndiyo maana unaona nakuwa kama nakufuatilia hivi.
Aaaaaaa haina shida.
Sawasawa. Aaaaa vipi kuhusiana na suala la jamaa yako kule Kijijini?.
Aaaaa Kwakweli Zaidu yule jamaaaa Daaaaa hata sikuelewi kabisaaaaaaa.
Kwanini Tena.
Kwasababu anaaza kufikia mahali tena pakusema kwamba Mimi nirudi kule kijijini.
Kwanini Sasa.
Si kwa vile Mimi ni mchumba.
Aaaaa aaaahaaa.ndiyo maana Yake. Sasa ukienda huko kwakweli Jeni sidhani kama utarudi.
Hapana huko Mimi kama ni Kwenda huko hapana.
Aaaaa Unajua Jeni si kwamba nakulazimisha.
Hapana Zaidu sijakuwa na maana hiyo kabisaaaaaaa Yaani kabisaaaaaaa. Kwasababu Zaidu eti leo hii uniambie niende nyumbani huko alafu kitakachofuatia kwa Mimi na jamaa yangu yule ni suala la kuoana tu.
Ni kweli.
Unajua kwasasa Zaidu Ndiyo Kama hivi umenifungulia hiyo sehemu ya kuingiza vimiamia kidogo na Mimi pia nionekane niko mjini hapa.
Ni Kweli kabisaaaaaaa.
Kwahiyo nilisema kwenda kule Ndiyo hivyo na Yeye anafanya kazi kule kule. Alafu Ndiyo Kama hivi kazi yake ni ya upolisi.Kuhamishwa kirahisi tu ni kitu ambacho hakiwezekani kabisaaaaaaa.
Ndiyo maana Yake Jeni. Kwasababu tukikumbuka na maisha yetu namna yalivyokuwaga Kwakweli duuuuuuuuuuuu inabidi tukaze sanaaaaaaaaa tena Sana.
Sawasawa Zaidu kwa hapo nakuunga Mkono.
Kwasababu Unajua Jeni maisha kubadilika ni sekunde chache sana tena sana. Leo hii Mimi siyo mtu wa kuanza kulia lia kwa ajili ya shilingi mia Bali ni mtu wa kuanza kufikiria nifunge kampuni ya nini Basi.
Ni kweli Zaidu. Kwahiyo kwa Mimi ninachosema tu kwamba nitapambana hapahapa mjini na hadi maisha yatazidi kukaa tu kwenye mstari maalumu.
Sawa Haina shida.
Aaaaaa, Na Mimi pia nilikuwa na mpango nianzishe salon hivi.
Ya kike au ya kiume?.
Zaidu.Naanzisha ya kike Bana.
Ahaaaaa. Sawa ni vyema pia.
Kwasababu Zaidu kuna location nimeipata naona iko vzuri Kweli Kweli.
Ni Jambo jema Sana.
Shukrani sana.
Aaaaaa hata Mimi kuna eneo nimelipata pia nataka kufungua sehemu ya kupikia chipsi waswahili tunaita vibanzi.
Ahaaaaa, alafu hiyo inauza kweli kweli kabisaaaaaaa.
Ndiyo maana Yake.Kwasababu kuna rafiki yangu hivi nimemuona kuanzisha mradi huu Kwakweli unamuingizia mtaji mkubwa Sana.
Ni vizuri sana Zaidu.
Sawasawa. Sasa Jeni kwasasa mimi nataka nitoke kidogo, nataka nielekee mahala fulani Hivi Ndiyo nitarudi nyumbani baadae Hivi.
Basi Sawa. Angalia epuka na Nyumba ya pili.
Hapana Jeni, milele Mimi siwezi fanya Hivyo. Weeeeeeeeeeeeeeeeee Yaani kabisaaa nimfanyie Zamda hivyo.Hapana weeee.
Haya bana.
Jeni aliinuka ili kuweza kumsindikiza Zaidu. Kisha baada ya kufika hapo nje na Zaidu akapanda gari na Kisha huyo akawa ameondoka.
Siku Hiyo ikiwa ni siku nyingine Kabisa. Siku Hiyo nyumbani kwa Zaidu alikuwa na ugeni mkubwa sana na tena mzuri Sana. Wageni hao Walikuwa ni mama na Baba Zaidu.Kwakweli siku hiyo ilikuwa ni Furaha sana kwa Zamda na Zaidu. Watoto wa Zaidu kwakweli siku hiyo Walikuwa nao wanafuraha sana Tena sana.Yite Hiyo ni Kutokana na kuja kwa bibi yao na babu ambaye ni mama na baba Zaidu.
Ikiwa ni Siku ya jumapili hivi. Kwa Siku hiyo Zamda alikuwa yuko akiendesha gari hivi.Lakini mda huo alikuwa akielekea maeneo ya supermarket hivi akiwa na watoto wake wote watatu pamoja wakiwa na mfanyakazi wao wa ndani.
Lakini alipokuwa anapaki gari lake kuna mtu kwa nje akaanza kumuita Zamda. Mtu huyo ni wa kike akiwa anauza matunda hivi.Mda huo Ndiyo Zamda alikuwa anapandisha kioo Lakini baada ya kusikia sauti ile ikabidi ashushe kwanza kioo na kumuangalia mtu yule akiwa anamuita Zamda na huku akimwambia rafiki yake hivi.
Zamda.
Zamda ni wewe."Zamda anafungua kioo "
"Mtu yule akaanza kusema hivi kwa mtu aliyekuwa naye karibu kwa mda huo. Alisema hivi".Hivi duuuuuuuuuuuu ni kweli macho yangu naona Au vipi?. Jamani huyu si Zamda kabisaaaaaaa.
|