SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 30 - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 30 (/showthread.php?tid=925) |
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 30 - MwlMaeda - 08-19-2021 SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 30
Ni siku nyingine kabisa ikiwa ni nyumbani kwa mama Tito. Kwakweli mama Tito alibaki ni mtu wa kuwa na simanzi tu mda wowote kutokana na Tito kuhukumiwa kifungo cha miaka Kumi gerezani. Siku hiyo akiwa amekaa na Bite Walikuwa wana maongezi kidogo hivi.
Yaani Bite Mimi siamini kama Jeni alikuwa ni wakutufanyia hivi.
Ila mama Ndiyo maana wahenga walisema kikulacho ki nguoni mwake.
Ni Kweli Bite kikulacho hakiwezi kuwa nguoni mwa mwingine.Yaani Kabisaaaaaaa Jeni ni wakumfanya Tito Hivyo.
Ila mama sikiliza niwaambieni tu kitu.
Kitu gani na wewe Unataka useme tena hapa?.
Aaaaaa ni kwamba Unajua penye Ukweli haina haja kupawekea rangi nyeusi eti ili pasionekane Bali penye ukweli pawekwe tu rangi nyeupeeee peeeeee ili paonekane vizuri na kwa Haraka. Haina haja ya kupaka matope sehemu ambayo ni nyeupe pepeeeee.
Unajua Bite kama vile sikuelewi unachomaanisha kabisaaaaaaa.
Najua ni vigumu kunipata kwa Haraka.
Kwanini iwe vigumu?.
Aaaaaaa acha tu niongee kwa kiswahili cha kawaida.
Kwani hapo uliongea kwa kiswahili gani?.
Cha kifasihi zaidi.
Mmmmh embu ongea cha kawaida.
Ni kwamba. Mama chanzo cha haya Matatizo ni nyiye hapo.
Nyiye nani na nani?.
Wewe na Tito.
Kivipi Sasa.
Kivipi?.wakati mlikuwa mkimtesa Zamda wa watu.kumbe Zamda naye Ana shoga wake ambaye anayejua haki za binadamu kwa vile kasoma japokuwa siyo mpaka elimu ya juu.
Nani huyo?.
Jeni.
Ana nini Sasa?
Jeni Ana jamaa yake Yaani Mpenzi wake ambaye ni mwanasheria. Ndiyo maana unaona jambo hili limefanyika chapuchapu.
Kwahiyo ndiyo kafanyaje?.
Anajua ustawi wa Jamii ninini
Tuseme Mimi mama yako hayo Mambo siyajui?.
Unaweza ukawa Unajua kitu fulani Lakini usijue kazi yake.Sijui kama umenipata mama Yangu.
Kidogo Sana
Kwasababu ni kosa lenu. Kwa hapa haina haja ya Kulalamika kabisaaaaaaa.
Kwanini Sasa ?.
Sasa mama kama siku ile Zamda ndiyo amerudi kutoka huko Ngata akiwa na watoto wake wawili alafu nyiye mnaanza kumtishia kwamba arudi alikotoka.Yaani hadi huyo kabisaaaaaaa Tito anamtishia Zamda na kisu.
Sikaondoka bila kumuaga mume wake.
Kwani akikuaga wewe kama mama mkwe kuna tatizo?.
Nakwambia hajamuaga mume wake.
Tito hakuwa amemuoa Zamda.
Bali alikuwa amemfanyaje Zamda?.
Walikuwa Kwenye uchumba tu.
Unajua na wewe Bite usijifaye Unajua sana kuliko watu ambao tumeshaanza kupiga miswaki kwa miti. Wewe nimekuzaa juzi tu hapa hapa mjini unaanza kupiga mswaki ambao sio wa mti uyajulie wapi haya Mambo. Halafu kila kitu Unataka kujifanya Unajua sana mwanangu.
Si kwamba najifanya najua mama yangu.
Hapana. Wewe Mambo yasiyo kuhusu achana nayo kabisaaaaaaa. Wewe ng'ang'ania ya huyo mme wako wa kuitwa Mpundu Sijui. Jina kidogo nitukane hapa.
Sawasawa ila ndiyo hivyo Ukweli huo hapo ubaoni.Huyo mwanao huko atanyea ndoa huko jela mpaka Basi tu.
Kwahiyo unafurahia Tito Kuwa Jela mda huu?.
Lahashaaaaaa.
Bali ninini kama ni Lahashaa ?.
Sheria Ndiyo imeamua na wala siyo mimi. Kwahiyo ninune ,nicheke kitu ni kile kile hakuna kitakachobadilika
Wai embu toka zako hapa acha Mimi nikalale zangu naona kama ndiyo unazidi kunitia matope tu kichwani mwangu.
Basi kwa mda huo mama Tito alitoka zake pale ndani na kuingia chumbani kwake. Kwasababu aliona kwamba ni kama tu huyo Bite anamuongezea Hasira kweli kweli.
Tukumbuke hivi Kijana Zaidu Sudaysi Zaidu alipokuwa akiishi mkoani Kimbu hakuwa anaishi kwa Wazazi wake kabisa wakumzaa Bali alikuwa akiishi tu Kwa Mjomba wake.Mjomba wake alikuwa akimpenda sana Zaidu kutokana na Mambo yake ya kifikra Pevu aliyokuwa akiyafanya.
Kwahiyo tayari siku nazo zikiwa zimeenda kidogo.Siku ikiwa ni siku ya jumatano mishale ya saa Tano asubuhi. Wakiwa wanaonekana Jeni, Zamda na Zaidu na watoto wa Zamda wakiwa wanacheza hapo kitandani.Watu hao Walikuwa na maongezi ya kimikakati Kweli Kweli. Basi Zaidu alikuwa akisema Hivi.
Aaaaaaa Unajua Jamani kwasasa naona maisha yangu tayari yameshaanza kukaa katika mstari ambao nilikuwa nikiutaka.
"Zamda akiwa amekaa karibu na Zaidu.Zamda akasema Hivi".Hongera sana Zaidu.
Shukrani sana Zamda. Hivi Unajua wewe ndiyo Kama ulikuwa kichochezi kwenye kuandika hadithi kabisaaaaaaa kwenye haya mashindano.
Kivipi yaani?.
Ayaaaa huwezijua ila kwa Mimi ndiyo najua ilikuwaje.
Duuuuuuuuuuuu Sasa hiyo kali kabisaaaaaaa.
Ndiyo hivyo. Kwasababu kuna hadithi kati ya hadithi nlizoziandika za Ukweli ambazo Yaani ni maisha ya mtu kweli kweli. Hiyo hadithi inahusu maisha yako Yote japokuwa mbeleni kabisaaaaaaa kuna baadhi ya vitu nimeviongeza kidogo.
Kweli Zaidu Kabisa.
Ndiyo Ukweli huo.
Asante Sana.
Tulia tukifika huko nitakuonesha ndipo Sasa utajua zaidi.
" Jeni kwa mda akiwa amekaa kimya akaamua kuongea Jambo kidogo kwakusema Hivi ".Aaaaaaàaaa Unajua Zaidu, vipi kuhusiana na suala la wewe kuendelea katika masomo.
Aaaaa Shukrani sana Jeni kwa swali hilo zuri sana umeniuliza.
Sawasawa.
Aaaaaa. Niseme tu nitasoma five na six kwa mwaka mmoja.
Utaweza kweli Zaidu.
Nitaweza tu.Yaani itanibidi tu niweze. Kwasababu siwezekusema nipige miaka miwili wakati na mda nao ndiyo huo unaenda umri kuzidi kuruka tu na kuna Mambo mengi tu Natakiwa kuyafanya.
Sawasawa.
Kwasababu kwasasa ndiyo Kama Hivyo mimi naitwa Baba Kwasasa.Kwahiyo Lazimaaaaa niumize kichwa. Mimi sitaki Hawa watoto wateseke kabisaaaaaaa,sitaki Hawa watoto waishi kama waliokotwa. Hawa watoto nitawahudumia kama vile sijui nani tu.
Ni vizuri pia kwa mipangilio yako hiyo.
Ndiyo mipangilio Yangu hiyo. Kwahiyo hadi mwaka kesho mwezi wa tano nitakuwa nimeshamaliza form six na Kuanza kusubiria Mambo ya matokeo Sasa.Kwahiyo ukiangalia kwa ratiba hii chamsingi ni kujitoa mhanga tu Basi.
Lakini Zaidu kwa Mimi sidhani kama nina kipaji cha kusoma tena.
Kwanini?.
Siunaona Mambo yanagoma tu.
Basi wewe ulikuwa unatakaje?.
Bora hata nikafanye biashara tu.
Haina shida tukienda huko nakokuambieni kila kitu kitanyooka.Kwasababu kule kwasasa mimi naishi kwenye Nyumba yangu Kabisaaaaaaa. Gari ndiyo Kama hiyo niliyopark hapo nje.
Basi sawa Mimi nakutegemea.
Haina shida kwasasa ni mda wa kunitegemea Mimi Kwasababu nilipokuwa America nilikuwa nakutegemea wewe sana.
Kwahiyo huko ulikuwa unamuwaza sana Zamda?.
Weeeeeeeeeeeeeeeeee nisimuwaze Zamda Kwanini Sasa.
"Zamda akiwa anacheka na kusema hivi".Lazimaa aniwaze Wewe. Mme wangu huyu.
" Zaidu akasema Hivi ".Yaani natamani hata ningeenda na Zamda.
" Jeni akasema Hivi "Kwanini.
Ayaaaa kule kila mtu Yaani unakuta yuko na mtu wake.Kwahiyo mtu akimuona mke wake pale kwanza moyoni anafarijika kweli kweli na kazi lazima afanye vizuri Sana.
Haya bana.
" Kisha akamwambia Zamda Hivi mda huo amemshika mkono wake kushoto akisema ".Zamda nakupenda sana.
Na Mimi pia mume wangu.
Asante sana kwa Majibu Hayo."Kisha Zaidu akamchumu Zamda.Akaendelea kuongea akisema Hivi".Sasa Jamani kwa ujumla tu kuanzia Sasa kufanya Maandilizi ya kuweza kuondoka.
" Wote wakajibu kwakusema Hivi ".Sawa.
"Zamda akamuuliza Zaidu hivi".Aaaaa Kwahiyo nyumbani kwetu Ngata tutaenda lini?.
Aaaaa tutaenda tu Zamda. Kwasababu Ngata ni karibu sana na Mkoa ule ninaoishi Basi Itakuwa vyema sana kama tutakwenda kule na pia tukapeleka na mizigo yote ili tukienda Ngata tusiwe na Mizigo mingi Sana.
Sawasawa haina shida.
" Pia Jeni akawa amesema hivi ".Ni vyema pia Kweli tukifanya hivyo.
Kwasababu Unajua Zamda hata Mimi natamani sana kuweza kwenda huko Nyumbani kwenu na kuweza kupajua.
Mbona pabaya tu.
Heeeeeeeeeeeeeeeeee maneno gani Hayo Zamda. Kwani mbona wewe mzuri hivyo?.
Haya Bana umenishinda Zaidu.
" Mda huo Jeni naye akasema Hivi ".Unajua Zaidu kwa nafasi hii uliyoipata Unajua ni nafasi nzuri sana katika Maisha yako na familia yako.
Ni Kweli Jeni jambo unalolizungumzia nakuunga Mkono kabisaaaaaaa. Yaani bila kipingamizi chochote kabisaaaaaaa. Kwasababu siamini kama miezi sita nyuma hivi nikikumbuka haki yangu ya kimaisha kwa namna ilivyokuwa Kwakweli kuna utofauti kabisaaaaaaa.
Ndiyo maana Zaidu. Hiyo ni Nafasi kubwa Sana.Hivi Unajua kwa wewe kwasasa ni mtu ambaye unajulikana na wasomi mbalimbali.Angalia majarida mbalimbali yameanza kutolewa kutokana na maisha yako ili tu kuweza kuwapa watu mbalimbali motisha ile.
Ni kweli Jeni. Pia nataka na wazazi wangu kwakule maeneo ya kijijini Kwakweli nipaweke vizuri harakaharaka kabla sijaanza Mambo ya masomo ya five na six.
Ndiyo maana Yake hivyo.
Kwasababu naweza kujikuta na kuwa na Mali kweli Kweli Lakini ukiangalia mazingira ya nyumbani kwetu Kwakweli hayafai.Kwahiyo itabidi niyarekebisha vizuri chapuchapu pamoja na kule nyumbani kwa akina mke wangu mtarajiwa Bibiye Zamda.
Ilipopita miezi kama sita hivi na Siku kazaa Hivi ambapo tayari hata Zaidu, Zamda na Jeni wako huko huko katika mji mkuu wa Nchi ya Kinani ujulikanao kwa jina la Damaresela. Ambapo Damaresela huko na Ndiyo makao makuu ya nchi ya Kinani,ndipo ikulu ya Kinani iliko huko. Kwahiyo katika jiji la Damaresela Mambo mengi hupatikana huko
Basi siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku ni mda wa Kusikiliza taarifa ya habari ya kutwa.Basi wakionekana Zamda na Zaidu wakiwa wanaangalia Runinga Hapo na Chaneli waliyokuwa wakiangalia ilikuwa ikiitwa SAKAS.COM TV .Wanaonekana sehemu waliyokaa ni kwenye sofa hivi.Jumba ni kubwa kwelikweli hapo ndani kuna maurembo ya kila aina yake.Zamda sura inayoonekana Kwakweli siyo kama alivyokuwa akiishi kule mkoani Kimbu. Unaweza kujiuliza Mara Mbili Mara tatu Ndiyo upate Majibu sahihi kwamba ni Yeye Au laaa. Mda huo tayari na muhtasari wa habari ulikuwa tayari umeshasomwa Sasa kinachofuatia ilikuwa ni taarifa yenyewe na uhakika wake.Basi mtangazaji huyo alikuwa akisema Hivi.
Habari Ndugu mtazamaji na msikilizaji wa SAKAS.COM TV .Baada ya kukusomea muhutasari kamili wa habari Basi tupate habari iliyokamili.Ni Mimi mtangazaji wako Sirati Kundi kinu.
Mfungwa mmoja alimekutwa amefariki kwa kujichoma na kisu katika gereza kuu la Mkoa wa Kimbu Wakati wakiwa katika shughuli za Shambani wakilima. Mfungwa huyo alikuwa ni nambaari M678 na kwa jina lake aliyekuwa akijulikana Kama Tito.Ambapo tukio Hilo limetokea katika gereza kuu la mkoa wa Kimbu.Kwa taarifa zaidi tumsikilize ripota wetu kutoka katika gereza kuu la Kimbu bwana Heriman Kaputi.Tumsikilize.
Basi ripota yule Alisema hivi.
Hapa ndiyo gereza kuu la mkoa wa Kinani. Nikiwa katika mashamba ya gereza hili ili kukupatia taarifa kamili. Ambapo mku wa Jela Bwana Rabit kabutu anasema kwamba "Ikiwa ni mishale ya saa saba mchana mfungwa wa gereza kuu la mkoa wa kimbi mfungwa nambari M678 .Amekutwa amejichoma na kisu katika eneo alilokuwa akifanyia kazi Yaani hapo Shambani. Inasadikiwa kwamba ni Mara nyingi sana mfungwa huyo alikuwa akijaribu sana kujiua Lakini anakutana na vikwazo vingi.Kwasababu mfungwa huyo alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka Kumi. Lakini hadi mauti yake yanamkuta tayari alikuwa amefikisha miezi sita na siku ishirini.Maamuzi Hayo Kwaujumla aliyafanya baada ya kuona ni mda mrefu sana atakaa jela hivyo Basi ni bora kutangulia mapema mbinguni.Kwasasa mwili wake umeenda kuhifadhiwa Katika hospitali ya Garisa ya mkoa wa Kimbu.kutoka gereza kuu la Mkoa wa Kimbu Ni Mimi Heriman Kaputi wa SAKAS.COM TV .
|