MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 28 - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 28 - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48)
+---- Thread: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 28 (/showthread.php?tid=923)



SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 28 - MwlMaeda - 08-19-2021

SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
 
SEHEMU YA 28
Baada ya Zamda kusikia maneno Yale kutoka kwa Tito na Kweli Zamda akawa anajua kabisa huko kwa mama Tito na Tito mwenyewe kwa mda huo atakuwa anaonekana hafai kama vile Nguruwe kwa muislam dhahir.
Maneno Yale Kwakweli Kwa Zamda kama ni kumchoma yalimchoma sana Zamda na yakawa yamemuingia mwilini mwaka mithili ya dawa ya Mwarobaini. Ila ndiyo hivyo afanyeje.
Basi kwa mda uleule tayari Zamda akawa amempigia Jeni simu na kuanza kumueleza Hivi.
Sasa Jeni wewe unanipangaje?.
Zamda.
Jeni.
Kama nilivyokupanga.
Mbona Lakini Jeni naona kama vile Mambo hayatonyooka!?.
Nakwambia hivi Zamda ondoa wasiwasi kabisaaaaaaa. Mimi najua namna ya wewe kuja Kimbu na mpaka hapa nyumbani kabisaaaaaaa.
Nyumbani tena!!??.
Ndiyo.
Na wakati ananitishia kisu hivyo.
Sasa ndiyo nakwambia Zamda wewe njoo hiyo kesho Au Kesho kutwa nikutengenezee bonge la tukio hapa hadi huyu Tito na mama yake watajuta kunijua mimi.
Ukweli kabisaaaaaaa Jeni.
Kweliiiii. Niamini Mimi ndiye rafiki nitakayekuokoa katika janga hili.
Sawa Jeni.
Ndiyo Hivyo, jiandae kwa Safari ya Kesho.
Sawasawa Jeni ntajiandaa.
Mimi hawa najua namna ya kuwaweka katika Matatizo na milele watajutia.
Sawasawa.
Nakwambia kwako itakuwa ni CHOZI LA DHAHABU na kwao itakuwa ni CHOZI LA MOTO.
Duuuuuuuuuuuu hiyo Hatari Sasa.
Ndiyo maana Yake.iko hivi Zamda.
Ndiyo.
Kama mtu anakufindiliza kukufanyia Mambo mabaya Basi na wewe badilika fanya hayo Hayo mabaya.Sasa hapa wamechokoza nyuki Kwenye mzinga wao mpya kabisaaaaaaa.
Haya basi Mimi huku najiandaa.
Wewe Chakufanya ukitoka huko njoo hadi nyumbani Hapo Sasa ndipo movie itaanzia hapo kabisaaaaaaa. Na Mimi kwa mda huo ntakuwa nimeshajipanga kabisaaaaaaa.
Sawasawa Jeni nakutegemea.
Ndiyo Hivyo na Mimi nakutegemea usiniangushe.
Haya Jeni. Baadae Basi.
Sawasawa. Unijuze michakato inaendaje huko.
Sawasawa.
Kama kuna Jambo linakwama huko nitaarifu mapema sana Zamda.Usisite kuniambia Kabisa Zamda.
Sawasawa Jeni nitakutaarifu.
Sawasawa. Halafu Kesho tena panda gari la mapema Sana ....
Sana.
Haya.
      Ikiwa ni mishale ya saa saba mchana hivi mda huo Tito akiwa sebuleni na Jeni wakiwa wanaangalia Runinga,kwa upande wa nje hivi kuna wadogo zake Tito Walikuwa wakifua huko.Kwahiyo kwa Mda huo Tito akawa amepata tena nafasi ya kuongea na Jeni.
     Jeni akiwa amejifunga kanga moja tu nywele zake mashaallah kajaaliwa kwelikweli za rangi nyeusi zilizokuwa zimelala hadi mgongoni na lainiii kwelikweli. Ukichanganya na Weupe wake Kwakweli hapo ni mithili ya mzungu kabisaa.
      Tito akiwa amevaa kaptula ya rangi nyekundu hivi na shati la bluu.Mda huo Tito akawa anamwambia Jeni hivi.
Jeni
Nini.
Vipi leo unatoka?.
Kwanini umeniuliza swali hilo?.
Aaaa Nina maana yangu Ndiyo maana nimekuuliza swali hili.
Ukimaanisha Nini?.
Usiku wa leo kama hutoki tutakuwa wote basi hapo chumbani kwako.
Mmmmh!. Sidhani.
Kwanini hudhani?.
Nitatoka.
Aaaaaaa kweli.
Ndiyo Ukweli huo nakwambia.
Waenda wapi?.
Naenda kwenye arusi.
Arusi?.
Ndiyo maana Yake.
Yanani?.
Ya rafiki yangu wa damu sana Yaani tena Sana.
Ahaaaaa basi Kesho kutwa hivi.
Kwa hapo Sawa.
Okay.Vipi utakuwa una nauli ya kwenda kwenye arusi?.
Mmmmh..
Wewe sema tu bana kama huna.
Haya Bana sina.
Sasa unaogopa nini?.
Naogopa tu.
Poa usihofu kwa hilo Natumai laki Tano na nusu inatosha ili ukawatunze vizuri hao Bwana na Bibi arusi.
"Hadi moyo wa Jeni ulishtuka baada ya Tito kutamka Hela ile kwa urahisi tu.kisha Jeni akasema Hivi".Ndiyo itatosha kabisaa.
OK tulia nikakuletee sasa hivi nisije nikatoka hapa alafu nikaja kupotea hadi baadae Usiku nasitokukuta.
Sawasawa nipatie tu.
Okay.
      Nakweli Tito akawa ameingi chumbani Kwake ili kuchukua Fedha ile na kumpatia Jeni.
   Lakini Kwakweli Tangu Tito aanze kumhonga Jeni hajawahi kukutana Kimapenzi na Jeni hata siku Moja .Kwasababu hapo kwa Jeni amekutana na kisiki ambacho Kwakweli ukijikwaa kwake ni Furaha tu na wewe unaenda kulilia Mbele kabisa.
      Basi Jeni akawa ameingia chumbani kwake na kisha akaanza kuongea peke yake akisema Hivi.
      Hivi huyu Tito anataka kunichukuliaje Mimi huyu.weeeee, Mimi siyo mlaini laini kama anavyoona wanawake wengine huko nje. Etii oooo nataka usiku wa leo tuwe wote.Nyoooooooooo nakwambia na hii laki Tano sijui hii ndiyo tunaanzishia maisha na Zamda Wangu hapo kati.
Hapa mjini watu wanaishi kwa mitego tu Mbona. Kwahiyo kama Ndiyo Hivyo kuna watu ambao wanategwa vizuri sana kama kina huyoooo Tito.
Wewe unafikiri watu tunapigwa style ya kifo cha mende kirahisi rahis tu.weeeeee. utaisoma namba hapa ndiyo umekutana na Toto la Lumbu hapa  limekuja mjini kusaka Hela kwa akili wakati wewee unasaka Hela kwa nguvu.utafilisika unajionea kabisaaaaaaa.
Nakwambia Zamda njoo hiyo kesho ujionee movie hapa inavyochezwa.Nakwambia kwaasa mbona Behind the scene ndiyo itakuwa inaoneshwa kwenye video.
Basi ikiwa ni mishale ya saa Mbili usiku ambapo tayari mda huo hata baba Zamda alikuwa tayari amesharudi kutoka msikitini kwa swala ya insha.Mda huo wakionekana wakiwa wamekaa kibarazani Hivi wakiwa mama Zamda, Baba Zamda, Zamda pamoja na wengine hapo.Walikuwa na maongezi kidogo kutokana na Safari ya siku inayofuatia. Baba Zamda alikuwa akisema Hivi.
Aaaaaa Zamda kwa awamu hii unaondoka hapa kwa amani Kabisaaaaaaa na siyo kama Kipindi kile.
Duuuuuuuuuuuu kweli. Kwasababu Kipindi kile ilikuwa ni Hatari.Yaani sijui mlijisahau kabisaaaaaaa kama Mimi ni mtoto wenu.
Hapana bana Zamda. Zile zilikuwa hasira tu Ndiyo maana nilikwambia mapema tu kwamba Hasira hasara.
Ni kweli ila haina shida. Sasa Jamani Mimi kesho ndiyo naenda Jamani Wazazi wangu.
"Wote walisema Hivi"Sawasawa.
" Mama akasema Hivi "Mimi nakutakia Safari njema mwanangu kwa hiyo Kesho.
Shukrani sana. Wazazi wangu kama nilivyowataarifu tangu mwazoni tu nilivyokuja kuhusiana na Maendeleo yangu huko kwa Tangu nimeenda huko na pia hata nikienda huko.
Ndiyo.
Kwahiyo nipende kusema tu Mambo yataenda vizuri siku si chache.Kwa mabadiliko niliyosema yanaweza kujitokeza basi yanawezekana kabisa.
Sawasawa mwanetu.
Kwakweli maongezi kwa siku ile yalikuwa ni marefu sana Yaani wakikaribia kukata usiku kabisa.
Basi asubuhi na mapema Zamda aliinuka na Kuanza kujiandaa vizuri ili msafara kuweza Kuanza. Ilipofika mishale ya saa Kumi na Mbili kamili tayari alikuwa ameshawasili katika stendi kuu ya Ngata ili kupanda gari na kuweza kuelekea huko Kimbu.Kwakweli msafara wa kutoka Ngata kuelekea Kimbu ulikuwa si msafara wa utani Kwakweli Kwa umbali wake namna ulivyo.
Ilipofika mishale ya saa Kumi na mbili za jioni tayari gari walilokuwa wamesafiria lilikuwa limeshashika breki kubwa katika stendi kuu ya Kimbu. Breki hiyo iliyofanya watu wakiwemo vijeba na wahuni wengine waliopo pale kuanza kupuliza Miluzi kweli kweli.
Basi Zamda akawa ameshuka kutoka  gari na kisha akawa amechukua mizigo yake na msafara ukaanza kuelekea huko mtaa wa Loronjo.
 Baada ya mda kidogo tayari geti linasikika linagongwa huko nje.Anayegonga geti hilo ni Zamda ndiye anayeonekana akigonga geti huku akiwa amesimama na watoto wake.Mmoja amembeba na huyo Glady akiwa amesimama pembeni hapo huku mzigo wa begi likiwa linaonekana. Zamda akawa anasema Hivi.
Hodiiiiiiii."Kimya kimetawala".
Hodiiiiiiii "Kimya Kidogo Kisha ikasikika sauti ya Mama Tito ikisema Hivi".
Nyiye kuna mtu anagonga geti huko nje.
" Ngongooooooooo".
Mda huo kumbe tayari Jeni akawa anajua kitu kinachoendelea kwa mda huo kabisa. Kwahiyo Jeni akawa anajipanga Kabisa kwa lolote ambalo linaweza kutokea mda si mrefu Hapo.
Mdogo wake Tito ndiye aliyeenda kufungua geti.Baada ya kufungua geti tu na mdogo wake Tito kwakumuona tu Zamda akaanza kufurahi kwelikweli na Kuanza kusema hivi.
Jamani wifiiiiii.
ile tu Tito alivyosikia neno "Wifi" tayari akawa ameinuka Kutoka Kwenye kochi na kuelekea huko mlangoni.Hapo mlangoni anakutana na Zamda akiwa ana Mzigo. Jeni naye akawa anaangalia Mambo yanayotaka kuendelea. Jeni kwa mda huo alikuwa Ana simu yake hapo akiwa ameishikilia mkononi. Tito Alianza kumtukana Zamda matusi makali kweli Kweli na maneno mengine kemukemu.Mda huo tayari Jeni naye akaamua kubonyeza simu yake sehemu ya kurekodi na Kuanza kurekodi tukio zima linaloendelea Hapo.Mda huo naye mama Tito akawa ameinuka.Tito alikuwa akisema Hivi.
Wewe mwanamke usiyekuwa na taadabu,mwanakulaaniwa wewe tena sheitwani rajimu wewe Yaani unakuja kufanya nini hapa wewe mshenzi?.
Si Nyumbani.
Nyumbaiiiii??.
Ndiyo.
Nyumbai hapa kwenu.Wewe mjinga nini.Toka nje kule.
Sasa nitoke nje niende wapi mda huu.
Uende wapi?.Wewe mjinga nini tena mpumbavu sana tokaaa nenda ulikotokea huko.
Sasa .
Sasa nini wewe tahira. Kwanza nilikuambia nini Kuhusiana na kuja huku Wewe.
Nisije.
Mpumbavu kweli wewe Yaani unajibu kirahisi kabisaaaaaaa eti nisije,Nyokoooo weweeee mwanamke usiye na adabu.Toka nje.
Sitoki.
Nasema toka nje Zamda. Ntakuchoma na kisu Sasa hivi. Ohooooo sifanyi utani hapa.Mimi sifugi mapaka shume Hapa.
"Mama Tito akawa amedakia mada na kusema hivi".Kwani wewe Zamda siku ile sinilikuambia kuhusiana na kwamba unaondoka bila kumuaga Tito. Lakini wewe ukanijibu kirahisi tu Yaaani kishwaini tu Hapa. Sasa Mimi hata sina la kuongea kuhusiana na wewe kilichobaki pambana na Tito wako.
Sasa mama mda huu Mimi niende wapi.
Heeeeeeeeeeeeeeeeee uende wapi.Wewe ulishajuzwa kitambo usije hapa Kwasababu umetoka bila ruhusa.
Jamaani.
" Tito kweli mda huo kaenda kuchukua kisu na anaanza kumtishia Zamda.Mda huo watoto wanalia Kweli. Tito anasema Hivi ".Zamda toka nje ntakuchoma na kisu.Yaani wewe thubutu kuingia hapa mlangoni.