SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 27 - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 27 (/showthread.php?tid=922) |
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 27 - MwlMaeda - 08-19-2021 SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 27
Kweli kabisaaaaaaa Jeni uko Kwenye siku zako?.
Ndiyo.
Kwahiyo hadi lini Sasa?.
Mimi ntakuambia tu mda wake uko.
Basi usije ukanichenga bana.
Siwezi kukuchenga bana.Kwani huu si utamu tu tunapeana.
Ndiyo.
Kweli nisingekuwa Kwenye siku zangu kwa mda huu tusingekuwa tunaongea mada hii tena.
Haya bana.
Ndiyo hivyo.
Kwahiyo acha Mimi niende Hapo ndani Basi.
Niletee Basi Hiyo Hela mda huu Tito.
Sawa tulia nakuletea mda si mrefu.
Asante.
Mimi sipendi warembo kama nyiye hapa kuteseka kabisaaaaaaa.
Haya bana.
Kweli Yaani kama Wewe hautakiwi kujishughulisha na kazi yoyote Kabisa.
Kwanini?.
Mwanaume si yupo.
Kama Wewe hivi siyo?.
Ndiyo maana Yake.
Basi kaniletee hiyo Hela mda huu.
Sawasawa.
Nakweli kwa Mda ule ule Tito alitoka pale chumbani kwa Jeni na kuingia chumbani kwake kisha akaanza kumwaga mabegi yake ili kuweza kuangalia sehemu ambayo huwa anaficha hela zake ili Zamda asije kuziona.Alimwaga kweli kweli mabegi ya Nguo Nakweli akawa amekuta kuna shilingi laki nne Kwenye begi lake.Tito baada ya kupata ile hela kisha akasema Hivi.
"Kudadeki kumbe nilikuwa na laki nne wakati nimemuahidi laki mbili na nusu. Aaaaa tulia nikampatie laki tatu kamili ili ajue Kweli kuna watu tuna hela bali tunazichimbia tu.Alafu kumbe huyu demu mrahisi tu.Yaani hapa bila hicho kisingizio Yaani kwasasa ingekuwa tayari nishalowanisha utambi kitambo.
Yaani hapa wewe wa kuitwa Zamda baki huko huko ukija huku nakufukuzia mbali hukooo.Kuna chombo kipya hapa nimekipata.Yaani huyu namlia hapa hapa yaani hii haina Mambo ya guest hapa.
Nakweli Tito alitoka pale na kisha akaenda kumpatia Jeni fedha ile.
Baada ya Tito kumpatia Jeni fedha ile kisha Tito akawa ametoka nje na kwenda huko kijiweni kwake.Hapo ndani akawa amemuacha Jeni pekee yake.Jeni akiwa na ile shilingi laki tatu akawa anasema.
Daaaaa kumbe hiki kijamaa kina hela alafu kinakataa kumpa Zamda.Sasa hapa hii laki tatu inabidi niigawe ili nimpatie Zamda kwaajili ya nauli ya kurudi Huku. Yaani huyu Tito akajua Mimi ni mtu wa kiurahisi rahisi tu.weeeee Mimi siwezi kumsaliti Zamda. Weee Zamda Shoga Wangu wa karibu Sana Tena sana.
Yaani Zamda huko uliko samahani sana kwakumrubuni mchumba wako ila kwa faida yako.kumbe huyu mchumba wako ana hela ila Yeye zake ni za kuhongea tu.Sasa shoga Wangu mbona tutamla tu huyu na Hapa haonji chochote kutoka kwenye mwili wangu.
Yaani atabakia kuona mapaja yangu tu Basi..Yaani haonji kabisaaaaaaa. Kila siku ntakuwa nampa sababu tu kama akihitaji tusex.kama leo nimemwambia niko Kwenye siku zangu Sasa tulia hiyo inayokuja mbona atasaluti Amri kabisaaaaaaa. Weeeeee hapa rafiki yangu lazima apate nauli ya kutosha tena na hata chakula huko njiani akija huku.
Yaani huyu Tito anapenda kuhonga wanawake Kweli Kweli mwisho wa siku atakuja kuhonga hadi Jini Jamani.
Sasa Zamda huko uliko Mimi huyu mchumba wako nitamtumia vizuri kwelikweli ili tupate Hela tu hapa. Yaani hapa hamna kung'ang'aa macho tu.
Nimeshajua namna ya kupata hela kwake huyu ni kitu kidogo tu cha kufanya. Wewe Tito siunajifanya unamtesa Zamda. Sasa tulia nikuoneshe wanawake wa mjini walivyo kama miyee Jeni.
Nataka nimchezee bonge la move Yaani hadi hatoamini ni Kweli hicho kitu nimemfanyia Au vipi. Wewe tulia ajifanye pedeshee Mtoto. Sisi Ndiyo tunaowataka kama hao.
Kwahiyo kumbe Kwaujumla Jeni si Kwamba anataka kumsaliti Zamda Bali tu anataka kumlegeza Tito ili aweze kumpatia Fedha na waweze kugawana na Zamda. Kwasababu imeshaonekana kabisaaaaaaa kwamba Tito ni Mzee wa kuhonga wadada wa watu mwisho wa siku atahonga hadi Jini kama Jeni alivyosema.
Basi kwa mda ule Jeni akaamua kumpigia simu Zamda ili kuweza kumpa uhondo mbalimbali alioupata kwa siku ile.Basi maongezi yao yalikuwa hivi.
Nambie Zamda.
Safi.
Vipi shogaaaa huko Ngata Vipi?.
Safi tu huku .
Wanao vipi hao ?
Wako vizuri kabisaaaaaaa.
Ahaaaaa basi vizuri.
Vipi kuhusiana na wazee hapo?.
Nao wako vizuri.
Vipi kuhusiana na sikukuu huko.
Ni Kesho Ndiyo sikukuu.
Ahaaaaa basi itabidi Usichelewe huko baada ya Sikukuu huko.
Sawa.Ila tatizo nauli shida huku.Wazee Yaani hawana chochote mfukoni.
Haina shida. Kuna hela hivi nimeipata kiujanja janja tu Hapa.
Kweli Jeni.
Nakwambia Kweli kabisaaaaaaa. Vipi nikutumie kwa namba yako hii hii?.
Ndiyo.sawa nitumie kwa namba hii.
Basi poa tulia baada ya mda Hivi.Kwasababu hapa niko ndani Kwahiyo hadi niende mtaani.
Sawasawa Jeni.
Wala usihofu.
ila Jeni umeipatajepataje Hiyo Hela?.
Ayaaaa hapa mjini akili tu Mbona. Wewe ukija ntakuja kukupa Mkanda mzima Kabisaaaaaaa namna nilivyopata hii Hela.
Acha utani bana Jeni.
Ukweli nakwambia hapa mjini ni akili tu na mipangilio mizuri tu.
Daaaa haya bana Jeni Yaaani nakwambia hiyo idd ikiisha tu Lazimaaaaa nije huko.
Ndiyo maana Yake.
Vipi umemsikia Zaidu kachukua ile tunzo na Yeye ndiyo Kama vile mshindi wa Kwanza kidunia.
Eeeeeeeeeeeeeeeeeee yameshatiki tayari mbona.
Ndiyo maana Yake .
Kwahiyo wewe sikukuu ikiisha tu jiachie huko wewe njoo.
Haina shida Jeni.
Ntakutumia shilingi laki moja na nusu .
Heeeeeeeeeeeeeeeeee Jeni Yote hiyo!!!.??.
Ndiyo maana Yake .
Mbona nyingi sana?.
Kawaida tu Bana. Ndiyo maana nilikwambia hapa mjini akili tu bana.
Kweli.
Vipi wazee umewaambiaje kuhusiana na huyu Tito.
Mhhh?. Nimewaeleza vizuri Yaana kwa undani kabisaaaaaaa kuhusiana na uhusiano Wangu na Huyo Tito namna ulivyokuwa hadi mda huu.
Mmmhi ikawaje Tena Zamda?.
Nimewambia tu Ukweli Kabisaaaaaaa kuhusiana na uchafu anaoufanya huyo Tito.
Ahaaaaa vizuri sana kwa ulivyofanya hivyo.
Pia nikawa nimewaeleza bila kuficha chochote kuhusiana pia na uhusiano wangu wa Kimapenzi na Zaidu Sudaysi Zaidu.
Eeeeeeee!!! kweli kabisaaaaaaa?.
Ndiyo maana Yake.
Wakasemaje Sasa?.
Ayaaaa mbona wamekubali tu.Kwanza walivyosikia anaitwa Zaidu Sudaysi Zaidu Kwahiyo wakawa wanafurahi sana kwakuwa Zaidu ni muislam.
Daaaa afadhali.
Yaani ilibidi nijikaze kwenye ule mda wa kuwaambia hii Mada.
Daaa, Sasa Zamda Kwahiyo wewe jipange tu.Kwasababu huku Nyumbani ninavyopaona kila mtu Ana hasira na Wewe.
Duuuuuuuuuuuu yashakua Hayo.
Ndiyo maana yake Zamda.Kwahiyo Mimi nimeshaanza kuhamishia vitu bila wao kujua nini kinaendelea hapa kwangu.
Umehamishia wapi hivyo vitu?.
Nimevipeleka kule mjini.kuna sehemu hivi nimepata vyumba viwili hivi.
Daaaaa na umeshalipia kodi kabisaaaaaaa.
Ayaaaa.Bado ila Ndiyo tayari huyo mwenye Nyumba hana shida kabisaaaaaaa. Kodi ni ile ile tu kama ya hapa.
Basi sawa Jeni.
Sasa unapotoka huko jipange na Mimi na nitajua ni namna gani ya kujipanga huku ili kweli wakikukatalia kuingia hapa nyumbani kwao tujue kuna mahali pakwenda.
Nimekuelewa Jeni.
Basi poa wasalimie wazee huko.
Sawasawa Jeni.
Siku iliyofuatia Tito alimpiga simu Bibiye Zamda. Ikiwa ni asubuhi mishale ya saa mbili. Mda huo Tito alikuwa yuko chumbani kwake.Zamda alishangaa sana kwakuona Tito kampigia Simu. Zamda alipokea simu ile na kusema Hivi.
Halooo.
Vipi Wewe?.
Safi.
Kwahiyo ndiyo ukaamua kuondoka bila Mimi kuwepo siyo.
Sasa Jamani Tito wala hatujasalimiana vizuri tayari umeshaanza kuniwakia.
Lengo langu si kukusalimia.
Bali ninini?.
Kukuwakia.
Kwakosa lipi nililofanya?.
Umeondoka bila Mimi kukuruhusu.
Sasa Tito.
Sasa nini wewe. Siunajifanya umeota mapembe Sasa utayapunguza Mwenyewe.
Unamaanisha nini Sasa.mbona sikuelewi.
Hunielewi siyo?.
Sikuelewi.
Namaanisha sitaki urudi hapa nyumbani."Baada ya Tito kuongea vile kisha Zamda akawa amebonyeza simu yake sehemu ya kurekodia sauti ila awe na uhakika hata baadae Tito akija kugeuka.kisha Zamda akasema Hivi ".
Tito unasemaje?!.
Nasema hivi usije hapa nyumbani. Yaani ndiyo ukifindiliza kuja hapa nyumbani Wallah nakupiga kisu.
Kweli kabisaaaaaaa Tito unasema Hivyo?.
Kwani mimi Nasema uongo. Najua kama utani vile.Unajua siamini.
Sasa kama Wataka kuamini njoo ingia hapa getini kwetu nimeapa ntakuchoma na kisu. mimi sinaga utani na wanawake washenzi kama Wewe. Nakwambia iwe Ndiyo Mara ya kwanza na ya mwisho kabisaaaaaaa Kwa siku uliyoliona hili geti.
Tito.
Nini?.
Ukweli kabisaaaaaaa.
Ndiyo maana Yake.
Sawasawa.
Wewe unajifanya una maamzi kabisaaaaaaa ya kuondoka bila ruhusa yangu.
Sasa ruhusa yanini .
Yanini?.Hivi wewe ni kichaa siyo?.
Labda.naweza kuwa kichaa kabisaaaaaaa tena tahira.ila tutajuana tu Mbele ya Safari.
Wewe usinitishie nyau Mimi wewe.
Sawa basi acha nikutishie paka.
Wewe ropoka tu Hapa.
Haina shida.
Ndiyo tayari nimeshafikisha taarifa hivyo.
Sawa.
Nimesema nikiona sura yako hapa getini kwetuuu Wallah nakupiga kisu alafu Ndiyo kitaeleweka mbeleni huko.
Sawa Kwaheri.
Kwaheri yako hainisaidii chochote kabisaaaaaaa.
Kwa Hapo tayari Zamda ameshapata taarifa kamili kabisaa ukiachana na ile tu ambayo Jeni alimwambia kuhusiana na mama Tito na Tito mwenyewe namna gani wamepanga juu ya kumdhibiti Zamda asije pale nyumbani.
Tito anajua tayari ameshapata Mpenzi mpya ambaye ndiyo Jeni kumbe haelewi Jeni ndiyo bonge la kinyonga apatikanaye Katika maeneo ya msitu wa Amazon.
|