MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 10 - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 10 - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48)
+---- Thread: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 10 (/showthread.php?tid=906)



SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 10 - MwlMaeda - 08-19-2021

SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU           
 
SEHEMU YA 10
      Tito kwakweli maisha kwakwe yalizidi kuwa ni maisha ambayo ni kutamani tu awe kama mtu fulani Bali uwezo huo hana. kwa mama Tito hakuweza kuwa na msaada wowote kwa Tito. Yote hiyo ni kutokana na elimu aliyokuwa nayo ilikuwa ni ndogo Sana.
Lakini siku nazo zilivyozidi kwenda Tito hakukata  tamaa katika kutafuta kazi maalumu itakayoweza kumuingizia kipato vizuri japokuwa hakutaka kujiendeleza kikazi.Miezi michache hivi kupita Tito akawa amepata tena kazi Kwenye kampuni moja hivi ya ujenzi tena ujenzi wa miundombinu ambapo kampuni Hilo ndilo kampuni linalomiliki mabasi ya kampuni ya SAKAS.COM Tito nafasi ambayo aliipata pale katika kampuni lile siyo kama Nafasi ya cheo ambacho alikuwa nacho katika kampuni ya ujenzi ile ya kichina.Nalo kampuni hili lilikuwa ni la wajapani.Hivyo basi kampuni Hilo la wajapani ndilo lilikuwa na ushindani mkubwa sana na kampuni Hilo la kichina.
Basi Tito akawa ameanza kazi katika kampuni Hilo la ujenzi. Lakini Kwakweli Sasa hapo ndipo Safari za kikazi za kwenda nje ya mkoa zikawa zimezidi kwelikweli kwa kijana Tito kitu ambacho Kwakweli Zamda hakukipenda Sana.
Baada ya kupita miaka kama miwili hivi na miezi kadhaa tayari Tito akawa amempa Zamda mimba ili kuweza kutekeleza ahadi ya Zamda ambayo aliiahidi ya kipindi hicho kwamba Zamda anaishi na Tito ili aweze kumzalia Watoto tena wazuri Sana. Lakini baada ya Tito kumpa mimba Tito akawa tayari ameshapata Safari ya kikazi ya kwenda nje ya mkoa kwa mda wa mwaka mzima Kabisa. Sasa siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa moja asubuhi ndiyo mda ambao Tito alikuwa akimuuaga Zamda na hadi Zamda akawa haamini kweli Tito anaenda kikazi mwaka mzima Kabisa. Basi mda huo wakiwa wanaonekana wako mlangoni hivi Wakiwa pamoja na mwanao ambaye ni Glady kwa kipindi hicho tayari ameshakuwa na kuanza hata kuongea vizuri. Mda huo Mabegi ya Tito yakiwa yanaonekana yamewekwa hapo.Zamda naye ndiyo huyo anaongea kwa kuchatuka kweli kweli akiwa anasema Hivi .
"Mda huo Zamda Anaonekana kavaa dera tu nguo za kawaida tu ikimaanisha mtu huyo ndiyo Kama ametoka Kulala mda huo".Sasa Tito Jamani unaenda huko kikazi unasema mwaka mzima...mwaka mzima alafu hata hujaacha Hela kubwa ya matumizi. Tito nionee huruma miyeee mke wako.
" Tito akiwa anaonekana kavaa suruali yake ya JEANS na tisheti ya bluu" Hahahaha Zamda unasema pesa nilioacha siyo kubwa,kwani pesa ina umri?.Wewe vipi Zamda. Mimi naenda huko nikipata nitakutumia.
Yaani kweli sijui kama kweli utatuma Hela. Tito hata nionee huruma tu Jamani huoni hapa kwenu unavyoniacha mmmmh tena na mama wakati mimi na mama Ndiyo Hivyo hazipandi kabisaaaa.Sekunde twacheka na masaa twanuniana.Ntaishije miyeee hapa ?.Nionee huruma Mimi kwasasa ni kama mke wako tu Tito na wala siyo tena mpenzi wako.Nakuomba nisikilize.
Zamda na Mimi nakuomba nielewe Miyeeee.Nimekwambia ntakutumia Hiyo pesa.
Jamani Tito hapa tumboni Nina Mtoto, kuna huyu Glady hapa wa kumlea tena Hapa. Hizo Hela Mimi nitatolea wapi Jamani. Nionee huruma Mimi mwana wa mwanamke mwenzako.
Zamda nahisi wewe hata darasani ulikuwa ni mgumu sana wa kuelewa.
Nilikuwa naelewa sana tu ni  kwa vile wewe ulinipaga mimba ndiyo ndoto zangu zikawa zimeishia hapo hapo.
Haya sawa kama unaelewa vizuri Basi elewa Hivyo Hivyo. Ni Kweli mimi natoka kikazi kwa mda wa mwaka mmoja na miezi kadhaa najua nitarudi na wewe uko na mama hapa nyumbani. Kwahiyo mbona Maisha yataenda vizuri tu.Ni wewe tu ndiyo unayeona mambo ni magumu Sana.wakati ni malaini kama mlenda wa kijijini.
"Tito kusema vile hadi zamda akashindwa kuvumilia na akajikuta anacheka.Kisha akasema hivi".Haya ila kumbuka ahadi yako uliyoniahidi itakuwa ni mfaraji mkubwa sana wa moyo wangu katika MAPENZI  yetu.Uendako nikumbuke sana kwamba uwe unajua umemuacha mke wako huku akiwa na Mtoto mmoja anayeitwa Glady na mwingine anayetarajiwa kuzaliwa baada ya miezi Tisa.Tito nakupenda sana wewe ni wangu wa milele Hivyo basi fanya penzi letu lizidi kunawiri na kuzidi kuleta harufu Nzuri kama ya ua la warudi.
Sawa Kwaheri.
"Kisha Zamda akamuaga Tito kwakumkumbatia huku akiwa anamchumu".
Basi waliagana hapo Lakini Kwakweli Zamda hakuridhika Kabisa  na huo msafara. Kwasababu anahisi kwamba hapo ndipo Tito ataanza tena kumsaliti na migogoro ndipo itakapozidi.Pia Zamda anajua Kabisa Tito hatoweza kutuma pesa yoyote kwa mda wote huo atakaokuwa huko.
Baada ya siku chache kupita Dada yake Tito alikuwa ameenda chuo Kwahiyo akawa analala huko huko.Hivyo  Basi baada ya Bite  kuondoka chumba alichokuwa akilala kikawa hakina mtu wa kulala.Baada ya mama Tito kuona hivyo ikabidi akubali mtu yeyote aje apangishe.Nakweli kuna mwanadada alikuwa anasoma Elimu ya watu wazima akawa amepangisha katika chumba alichokuwa akiishi  Bite.Basi siku Hiyo ikiwa ni siku ya jumapili Zamda akiwa anaonekana amekaa kwenye kochi akiwa na huyo shoga wake mpya aitwaye Jeni   wakiwa wanapashana habari kidogo hivi. Maongezi yao yalikuwa hivi.
"Jeni akiwa naye amekaa kwenye kochi huku akimhadithisha Zamda Hivi".Hivi shoga niko hapa kama miezi kadhaa Hivi na masiku  kidogo nakuona na mtoto wako huyu Glady Lakini  Baba Watoto simuoni Yaani Kwaujumla sijawahi kumuona.
"Zamda akiwa anaongea huku Tabasamu lake likiwa linaonekana kwa mbali".Ni Stori ndefu Sana Jeni.
Ndefu kivipi wanitisha Unajua au amefariki?!.
Hapana,yuko hai Kabisa
Mbona simuoni?.
Aaaa amesafiri Kikazi
Duuu amesafiri mda wote huo?
Aaaaa kawaida tu mbona.
Hadi lini Sasa ?.
Hadi mwaka uishe ndipo aje.
Duuuuuuuuuuuu Sasa siutamkumbuka sana?.
Lazima nimkumbuke.Lazima nimkumbuke mme wangu wa milele.Yaani nitakuwa nahamu shoga wangu sijui nikuelezaje tu Jeni.
Kwasababu gani?.
Mda huo Wote yaani nakwambia zitajaa mwilini Kwelikweli.
Haaaaaaa weeeeee shoga wangu hapa mjini wewe.Yaani Mimi mwenyewe jamaa yangu nimemuacha huko vijijini Lakini suala Hilo la kusema nitakuwa na naniii nyingi sana mwilini haliwezekani.wanaume wamejaa Hivyo mtaani.
Duuuu Kwahiyo shoga wangu wanishaurije Sasa. Kwasababu huo mwaka mmoja si kitu cha utani utani.Unajua Mimi mwanamke wa kingata natakikana kweli nimfanyiye mwanamme Mambo yaliyonileta kwake na si kukaa tu.
Nikushauri nini Sasa ni wewe mwenyewe tu.
Alafu nimekumbuka
Umekumbuka nini tena wewe.
Aaaaaa kuna siku Hivi ulikuja na Kijana fulani cheupee kama mzungu vile na Ana mwili mdogo mdogo hivi.
Ahaaaa nampata ndiyo.Si yule ambaye aliondoka mishale ya saa mbili usiku hivi?.
Ndiyo huyo kabisa. Vipi ndiyo jamaa nini Yule Kwasababu anavyoonekana ni mtanashati Kwakweli hadi nikasema Kweli Jeni kapata hapa.
Wala yule rafiki yangu tu.
Acha kunidanganya Jeni mimi si mtoto bana.Sijazaliwa leo.Yule Mpenzi wako.
Kweli Mimi nakwambia hutaki kuamini?. Yule mkaka wa watu laiti ungejua anavyolia na mpenzi.Yaani kwasasa Hana Mpenzi kabisa. Kwasababu kuna kadada Fulani kalikuwa ni kazuri kwelikweli kakawa kamemuacha.Basi yule mkaka siku hiyo alichanganyikiwa ile mbaya. Yaani kwanza yule mkaka alikuwa anampenda ile mbaya.Kwanza yule mkaka hata hakuwa na Mambo ha michepuko na hata Sasa Hayo mambo Hana kabisaaaaaaa Kwa mda huu.Kwaujumla tangu aachwe na huyu mwanadada mrembo.
Daaaaaaa Sasa Jeni hako kasichana kalimuacha Kwanini?.
Yaaani sijui hata nikuelezaje tu.Ila Kwakweli huyo msichana alikuwa ni mzuri Sana.Kwahiyo yule mkaka hadi mda huu hana mpenzi yeyote. Kwasababu Mimi ananipaga stori mbalimbali tu kuhusiana na maisha yake.
Ahaaa haya.
Vipi ushamuelewa nini au
"Zamda akiwa anaongea huku anacheka akisema Hivi".Yuko vizuri Kweli. Ila usije ukaja kunidanganya ukasema siyo Mpenzi wako kumbe ni wako tukaja tunaanza kurushiana maneno baadae bureeeee shoga Wangu.
Hapana shoga wangu nakwambia Ukweli.
Haya  Basi mfuatilie namba zake Basi Au unipatie Sasa hivi tu.
Hapana tulia kwanza nikamwambie na nikishamwambia Ndiyo nijue amekubali Au laaa.Kwasababu kama nilivyokuambia bado Ana maumivu ya kuachwa.Kwahiyo kichwa chake Kwenye mambo ya mapenzi hakijakaa vizuri Hadi Sasa.
Haina shida Basi mwambie tu.Kwani jina lake anaitwa nani.
Anaitwa Zaidu.
Ayaaa bonge la Jina la kiislamu Jamani ndiyo angenipa mimba huyu ningefurahije Jamani.
Alafu angalia usije ukanogewa na Zaidu na ukampa yote na kumsahau jamaa yako.
Yaani waogopea mimba.
Ndiyo.
Ayaaaa kwa Hilo wala usiwaze jamaa ashaacha kijusi hapa tumboni Ndiyo akasafiri.
Duuuuuuuuuuuu Kweli mjanja huyo.Kwasababu anajua akikuacha Hivi Hivi tu lazima akirudi atakuta wapangaji wengine kwenye Nyumba yako.
Basi kesho ukienda huko school kwenu usijeukasahau kumwambia Zaidu tutagombana shoga wangu.
Usihofu Zamda ntamueleza tu.
Haya nakutegemea wewe.