SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 08 - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 08 (/showthread.php?tid=904) |
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 08 - MwlMaeda - 08-19-2021 SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 08
" Mama Zamda akawa ameamua kuchachama kweli kweli akimuuliza maswali Tito ".Hivi Tito Unataka kuniona Mimi Mtoto kabisaaaaaaa eeeeeeee.
Siyo kwamba ni Mtoto mama.Huamini Kwamba huyu ni mfanyakazi. Nitakuwa namlipa mimi kama wewe unaona jau.
Sawasawa haina shida. Ila Lakini mfanyakazi gani huyu umekuja naye,wewe siutakuwa umemuokota tu huko.Kwanza Chakushangaza Hana begi hata wewe mwenyewe hata wewe mwenyewe tu hauna begi sijui umelitupia wapi.
Hayo mambo ya begi mama tutayaongea vizuri ila si kwa mda huu.ila wewe jua kwamba huyu ni mfanyakazi nimemleta Hapa.
Haya huyo mfanyakazi wako atakuwa analala wapi.Kwasababu ndiyo Kama hivi unavyoona Dada yako kwasasa wamefunga chuo.Kwahiyo kwenye hicho chumba kuna mtu hapooo na Mimi sitaki Dada yako ajibane bane hapa na mtu ambaye hata hamjui.
Haina shida atakuwa analala kwenye kochi.
Eti mbona Yaani unaongea kiurahisi sana.Hivi wewe Tito umechanganyikiwa nini, mbona huko Ngata pamekuharibu hivyo?.
Sasa mama kwani jambo gani la kuongea kiugumu hapa ?.
Haya Sawa kama unaona namna gani sawa.Basi haya atakuwa analala hapa Kwenye kochi patamtosha.Hana hata cha shuka wala nini.
Nitampatia vyote tu hivyo.Iko siku utakuja kumkubali kwelikweli. Tatizo wewe humuamini amini hivi.
Ntamuaminije mtu wakati Ndiyo kwa mara ya kwanza tu tunaonana.
Haya Basi utamzoea tu.
Haya siku hizi na wewe una maamzi ya kuwa na mfanyakazi. Sawa atakuwa anafanya kazi zote Hapa. Kwanza itakuwa vizuri sana.
Haina shida atakuwa anafanya kazi zote wala usihofu.Malipo pia nitakuwa nampatia Mimi tutaelewana naye tu.
Atiiiiii mtafanyaje?!.
Tutaelewana tu kwani Shida gani?.
Ahaaaaaaaa haaaaaaa Tito una Matatizo wewe
Matatizo gani mama ?!.Mimi sina Matatizo yoyote, sidhani kabisaaaaaaa kama Nina Matatizo.
Haya Basi mkaribishe huyo mfanyakazi wako akae Kwenye kochi.Anaitwa nani kwanza.
Anaitwa Zamda.
Atiii nani ?!
Anaitwa Zamda.
Haya.
Zamda karibu ukae kwenye kochi.
"Mda huo Zamda alipokuwa amesimama amebaki anaangalia chini tu kisha akajibu hivi ". Asante.
Tito kuweza kuongea vile kwamba Zamda ni mfanyakazi ilikuwa ni kuweza tu kufunika kombe tu mwanaharamu apite.Yaani kwa mda ule angeanza kumueleza kwamba amempa mimba Zamda Kwakweli mama Tito asingeelewa kwa mda huo .Kwahiyo ndiyo maana Tito akaamua kutumia ujanja ule.
Lakini ikiwa ni mishale ya saa mbili kamili Usiku baba Zamda akiwa na mama Zamda wanapata chakula kwa Upande mwingine pia tunawaona Mpundu na wadogo zake wakiwa wanapata chakula.Mda huo baba Zamda anavyopata chakula ili Sasa baada ya chakula aweze kwenda msikitini vizuri kwa sala isha. Kwasababu ndiyo kawaida yake tu alivyo.
Kwa mda huo kuna redio ambayo ilikuwa imefunguliwa hapo ikiwa imewekwa karibu na Sehemu ambayo mama na baba Zamda waliko.Ilikuwa ndiyo mda mwafaka kwa taarifa ya habari.Taarifa ya habari ile ilikuwa kama ifuatavyo.
Uhali gani Mpenzi msikilizaji wa Ngata FM,Natumai u mzima wa afya Kabisa.Ni kipindi maalumu ambacho kimegawanyika katika sehemu Mbili.Tutaagalia taarifa za habari za kitaifa na kimataifa na Kwa upande wa pili pia tutakuja katika uchambuzi wa michezo.Tukianza na Taarifa mbalimbali za kitaifa ni Mimi mtangazaji wako Sokutwe Ngazijamu.
Ajali kubwa iliyotaarifiwa kuwa imeweza kupoteza maisha ya abiria takribani hamsini na kuwa na majeruhi ishirini na tano walipokuwa wakitoka mkoani Ngata kuelekea mkoani Kimbu.Ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana karibu na daraja la Kisisiri, chanzo cha ajali hiyo inaelezwa ni kwamba inasemekana kuna kitu kilikuwa kikionekana Mbele ya gari ndipo dereva huyo wa gari Hilo akawa ameshika breki na kujikuta gari limeshapoteza mwelekeo na kuanguka kisha likaanguka na baada ya mda likawa limelipuka.Ambapo miili ya marehem hao na majeruhi hao imepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Ngata.Basi kwa taarifa zaidi tumsikilize mwandishi wetu wa Ngata FM Uhuru kazi ambaye ameweza kufika kwenye tukio hilo.
Basi kwa mda huo Kwakweli taarifa hiyo ilivyotolewa mama Zamda moyo ulianza kumwenda mbio sana.Kwasababu anajua Kabisa kwamba hata Zamda na Tito watakuwa wamepanda gari Ambalo limepita Kwenye njia hiyo Hiyo. Mda huo akawa anamuuliza baba Zamda Hivi.
Mme wangu kweli hili janga halitakuwa limewakumba Hawa watu ?."mda huo anaonekana akiwa ameshika sahani ya chakula ambacho kilikuwa ni wali huku akiwa amekaa Kwenye kigoda. Naye baba Zamda Hivyo Hivyo akawa anasema Hivi".
Watu gani hao unawaongelea?.
Yaani kabisaaaaaaa hujui watu gani leo wamesafiri ?.
Alaaaaaaa mke wangu Yaani Unataka nijue kila abiria waliosafiri wa mkoa wote wa Ngata. Au Unamaanisha nini.
Namaanisha Zamda na Tito.
Ahaaaaaa,mungu atakuwa amewanusuru.
Yaani kirahisi tu Wakati hapa unaambiwa maiti ni nyingi kwelikweli.
Asaaaa, mke wangu Kwahiyo huu usiku wote Unataka ufanyaje?.Unataka uende huko Hospitali ya Rufaa.Kama wamefariki ndiyo hivyo mipango ya Mungu haina makosa. Tunasema tu inalillah waina illah Rajighun Basi haina haja ya kutoa machozi kweli kweli sijui kama nini.Ni sawa tu na mtu aliyeenda kununua sumu ya panya ili anywe tena huku anasubiria chenchi,Huyo atakuwa anajidanganya tu Hapo.
Haya.Tuachane na hiyo mada Kwasababu tunaweza kuzusha Mambo mengine kabisaaaaaaa hapa.
Lakini ilipofika mishale ya saa mbili na nusu usiku ni mda ambao wadogo zake Tito Walikuwa wameshamaliza kula kisha wakaamua kuelekea Kulala pia hata Dada yake Tito alienda Kulala. Kwahiyo hapo sebuleni wakawa wamebaki Tito, Zamda na mama Tito. Sasa ikawa ni mda mwafaka kwa Tito kuweza kuyaongea aliyoyaficha moyoni kuhusiana na ukweli wa kati yake na Zamda.Lakini ikabidi Tito atumie ujanja katika kuyatoa maelezo Yale.
Mama katika msafara wa leo Kwakweli tumekutana na majanga makubwa sana tena sana,Ndiyo maana mda ule ulivyouliza kuhusiana na mabegi yetu nikakwambia tutaongea mda mwingine.Kwaujumla kwanza sisi mungu anatupenda Sana.
Kwanini?.
Tumepata ajali mbaya sana leo.
Ajali?.
Ndiyo ajali Yaani ukisikia ajali ile kweli ni ajali.
Sehemu gani mmepatia hiyo ajali ?.
Pale Karibu na daraja la Kisisiri.
Chanzo cha ajali ni nini ?.
Dereva aliona tu mtu Mbele yake na kushika breki na gari lilikuwa liko Kwenye mwendo Kwelikweli likawa limepoteza njia kabisaaaaaaa na kujikuta tumeangukia huko
Kwanini mmepita huko Wakati mlikuwa na Gari la kazini.
"Tito akamjibu mama kwa ujasiri kwakusema Hivi" sijapanda gari la kazini.
Kwasababu gani.
Kuna tatizo lilijitokeza kidogo Kwahiyo nikawaomba waende tu kwamba Mimi nitasafiri kwa bus tu.
Tatizo gani Hilo Tito ambalo kweli limekufanya usije na Gari la kazini hadi ukakutana na janga Hilo?.
"Kwakweli hapo Sasa ikawa Sasa ni kazi kubwa Sana kwa Tito kuweza kumjibu mama Au kumpatia mama Majibu yaliyo kamili kwa wakati ule.Lakini ikambidi tu aongee Kwasababu afadhali hata kwa mda huo mama Zamda hakuwa na hasira sana kama mda huo walipofika tu.Tito akaamua kuongea ukweli kama ifuatavyo". Nimempa mimba Zamda."Kabla hajamaliza maelezo tu tayari mama Zamda akawa amemkatisha Tito kwakusema Hivi".
Atiiiiii unasema nini wewe Tito ?!!!.Embu rudia
Nimempa mimba Zamda Kwahiyo wazazi wake wameng'ang'ania nije naye hawataki mada nyingine Kabisa.
Yaani Unajua wewe Tito unachekesha Kabisa. Yaani umeenda Ngata miezi yote kama mitatu hivi kwa maamzi yako ya kishenzi kabisaaaaaaa ukaamua kumpatia mtoto wa watu mimba na kufanya ndiyo Kama zawadi kwangu.Alafu ulivyomnafiki mwanzoni unaniambia kwamba etiii umeniletea mfanyakazi wa ndani. Hivi wewe unajielewa kweli,Yaani unaamua kunidanganya kabisaaaaaaa.
Mama ndiyo Ukweli huo.
Ukweli wapi wakati mwanzoni ulisema kwamba umeniletea mfanyakazi wa ndani ambaye ndiyo huyu Hapa. Hivi wewe unaniona mimi mtoto sana Au sio?."Mama Tito akamgeukia Sasa Zamda kwakumuuliza Zamda Hivi ".wewe Zamda huyu nani Wako?.
" Zamda akiwa anajibu kwa kujing'antang'ata akisema Hivi ". Mchumba wangu.
Atiiiiii nani wako?!.
Mchumba wangu
Mbona mwanzoni alivyosema kwamba wewe ni mfanyakazi wa ndani,Mbona haukuongea chochote?.
Nilikuwa naogopa.
Ulikuwa Unaogopa??!. ...unaogopa nini Sasa. Yaani unakubali kuitwa mfanyakazi wa ndani kabisa na mtu ambaye ni mchumba wako Kabisaaaaaaa. Halafu hivi wewe Tito hadi maamzi Hayo uliyoyafikia ya kusema umeamua kumpa Dada wa watu mimba Sasa inaonesha dhahiri shahiri kwamba unajiweza Kiuchumi, Yaani unaweza kummiliki kabisa huyo mchumba wako.
Siyo Hivyo mama.
Bali ni Vipi. Yaaani nakwambia hii inadhihirisha kabisaaaaaaa kwamba wewe uko tayari kupokea familia katika mazingira yoyote Yale.Kwahiyo Sasa Tito ni mda wa wewe kwenda kupangisha huko utakapopaona panakufaa,hapa kwangu kwasasa utakuwa unapaona ni kama vile kwa jirani Hivi.
Sasa mama nikapangishe,nikapangishe wapi,nianzie wapi sasa?.
Nasema Tito sitaki maelezo mengine toka nje na huyu mchumba wako.Usinichefue usiku wote huu.wewe umeshakuwa tayari ndiyo maana hadi umeweza kumpatia Mtoto wa watu mimba. Nenda kule.
Mama.
Sitaki masuala ya mama...mama Hapa, Toka nje sitaki kukuona Hapa ndani kwangu,toka Sasa Hivi."Mama anaongea anaonekana Ana Hasira kweli kweli hadi kasimama".wewe Zamda toka nje na huyu mchumba wako tokaaaaa Haraka."Tito akasema Hivi "
Sasa mama tutoke tuende wapi usiku huu eeeeee.
Wewe Mimi sitaki maswali ya kizushi hapa toka nje na huyu mchumba wako.Yaani unaenda Ngata kikazi unarudi na msichana umempa mimba alafu bado unaishi nyumbani kwenu unakula ugali wa shikamo. Tokaaaaaa.
Mama Jamani mama tuende wapi sasa.?."Zamda anaonekana kachanganyikiwa kwelikweli hajielewi ni wapi pa kuelekea ".
Nasema tokaaa nje mtajuana huko huko nje mkalale stendi Au laaa.
|