UTENZI: UMUGANURA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Historia ya makabila ya kibantu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=15) +--- Thread: UTENZI: UMUGANURA (/showthread.php?tid=782) |
UTENZI: UMUGANURA - MwlMaeda - 08-06-2021 [attachment=503] UMUGANURA ---------------- UMUGANURA ni siku, maarufu Rwanda ino. Maeneo yote huku, ni sherehe ya mavuno. ------- Ni Ijumaa ya kwanza, ya kulla wa nane mwezi. Sikukuu tunafanza,, kimila tukiuenzi. ------- UMUGANURA 'likuwa, desturi asilia. Wanajamii wakiwa, pamwe wanafurahia. --------- Nafaka pia maziwa, wahenga walichangia. Nazo nyama zililiwa, togwa na kangara pia. -------- Sikukuu ya mavuno, kwetu ndo UMUGANURA. Siku ya makongamano, kukumbuka ya kikwetu. -------- Twala mapishi ya jadi, na vinywaji kutumia. Tukipeana zawadi, umoja kuzingatia. ------- Mila za Waafurika, sana zakaribiana. Mshairi mshirika, n'kusaili muungwana. -------- Hini siku ya mavuno, tunayoienzi sana, jamii ya pande zino, kwenu inapatikana? ------- Utenzi natamatisha, wasanii n'kiwaomba, milazo kunijulisha, awabariki MUUMBA. ============= Rwaka rwa Kagarama (Mshairi Mnyarwanda), Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare, R W A N D A. |