METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA (/showthread.php?tid=724) |
METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA - MwlMaeda - 08-01-2021 METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA
Methali hii inasisitiza juu ya tahadhari. Binadamu ni lazima awe na tahadhari sana katika kuenenda na maisha; ni lazima ajihadhari na kiumbe hiki binadamu. Kama vile binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kuhisi ndivyo pia alivyo na uwezo mkubwa wa kuathiri. Mtu ni mtu lakini si kila mtu ana utu. Utu ni ubinadamu na ubinadamu ni mwenendo mwema kwa binadamu wengine. Huo mwenendo mwema ni hiari na matakwa ya huyo mwenyewe. Hiari ni siri ya moyo. Kila mtu ana moyo wake. Kwa hiyo ana siri yake-hiyo aijuayo. Hiyo siri ya moyo wake yaweza kuwa njema au mbaya kwa mtu mwingine.Kwa hiyo kama vile ilivyo kweli kwamba adui yako aweza kuwa mwema wako ndivyo pia ilivyo kweli kwamba mwema wako aweza kuwa adui yako.
Hii ni methali nyingine ambayo yamtaka mwanadamu awe mwangalifu zaidi awe na tahadhali. Mti ni mti, na huumiza hasa umuangukiapo kiumbe kama binadamu. Kwa hiyo binadamu akiuelewa huo udaifu wake na kama anataka kuishi maisha marefu zaidi, anawajibika kusimama kando ili mti usimuangukie. Maana inayojitokeza hapa ni kwamba tusijitie katika mambo yasiyotuhusu au tusiyoyaweza. Ni lazima tuchunguze uhusiano na uwezo wetu kabla hatujaamua kujishirikisha katika mambo ya wenzetu. Kama tukibaini kwamba mambo hayo hayatuhusu, hatuyawezi au yanaweza yakatuletea madhara, basi tukae kando na tuwaachie wenyewe waendelee na mambo yao.
Methali hii inajulikana sana kwa matumizi yake ya kila siku. Ni wazi kuwa ukitaka kukinga moto ambao unakuja basi nawe yakubidi uwashe moto. Hii hutumika kwenye vijiji vilivyo karibu na mapori. Maana ya methali hii hasa ni kwamba ubaya dawa yake ni ubaya vilevile. Yaani akufanyiaye mabaya basin awe mfanyie mabaya.Hivyo ubaya huo ukikutana aidha kutatokea namna Fulani ya usuluhisho. Tafsiri nyingine ya methali hii ni kwamba jambo lolote tukiona laenda kombo basi twatakiwa kuwahi kulitibu kabla halijawa baya.
Methali hii inafanana na ile isemayo hamadi kibindoni. Huwezi kufanya jambo kwa kutegemea msaada kutoka sehemu nyingine (jirani). Jirani hawezi kutatua matatizo yako kama vile ambavyo wewe mwenyewe ungeyatatua. Jirani si wa kutegemea. Twahitajika kujitegemea wenyewe kuliko kutegemea wengine.
Ni kweli kwamba fimbo iliyo karibu ndiyo iwezayo kuua nyoka. Methali hii hutumiwa wakati unapoongelea jambo ambalo utatuzi wake watakikana haraka ama pengine bila kupata msaada sehemu nyingine. Msaada wowote, akiba yoyote ambayo ipo tayari kwa wakati unaotakiwa, ndio msaada pekee unaothaminiwa na kutambuliwa. Huwezi kutegemea kitu ambacho kiko mbali ama kukipata kwake kuna matatizo ikilinganishwa na kitu ambacho kipo tayari kihitajiwapo.
Methali hii hutumiwa kwa kusema kuwa kwa kweli kula ni kula. Hakuna chakula ambacho hakina umuhimu. Chakula ni chakula hata kikiwa kiporo.
Methali hii yatutahadharisha tusiwe wenye tamaa tama. Twaambiwa kuwa unapokuwa na haja ya jambo Fulani ukawa katika hali ya kutekeleza basi usirukie jambo jingine la aina ile ile maana waweza ukakosa huku na kule. Shika ulichoshika usifuate kile ambacho huna uhakika wa kukipata.
Hapa mshipi umetumiwa kama kielelezo tu. Maana hasa ya methali hii ni kwamba binadamu tunapotembea tusijione kuwa ni kitu sana. Yatupasa kufahamu kuwa kila tunapotembea kifo kinatuzunguka.
Haiwezekani mtu awe mjinga moja kwa moja. Kuna siku anaweza kufanya mambo mazuri watu wakashangaa.Watu wengine huamini kuwa hakuna ujinga ambao ndani yake hauna welevu. Hivyo tusije tukawadharau watu kuwa ni wajinga na tukaamini hivyo moja kwa moja.Tukifanya hivyo tutakuwa tunafanya makosa.
Ni wazi kwamba shoka linapokata daima hukata vitu ambavyo vyaweza kupotea. Kinachokatwa na mdomo aghlabu hakipotei, maanachaenda tumboni. Binadamu anapokata kitu kwa mdomo ni wazi kuwa baadaye hukila kitu hicho na kwamba kitamnufaisha katika kujenga, kulinda na kuhifadhi mwili. Methali hii yatushauli kuwa tufanye mambo yetu kwa dhamiri maana katika dhamiri kuna mafanikio. Tusifanye mambo juu juu tu ; bali kwa undani na dhati.
Si rahisi kufahamu kunguni wa kitanda usichokilalia wanauma kiasi gani. Hivyo anayelalia kitanda hicho ndiye anayefahamu kunguni wake.Kimatumizi methali hii inatueleza kuwa mtu hawezi kujua shida zinazompata mtu mwingine.Jambo lisilokuhusu ama kukupata huwezi kujua ubaya wake.
Methali hii inajieleza yenyewe. Ndugu wana tabia mbalimbali na nyingi ya tabia za ndugu ni kinyume cha vile ambavyo tungewatazamia wawe. Hivyo basi unapoamua kukaa na ndugu basi yakubidi uwe mvumilivu kwani vitendo vingine vyaweza kuwa vya kusikitisha na kutisha. Hivyo basi tunapoamua kukaa na ndugu lazima tuwe wavumilivu wa maovu yote ambayo watatufanyia.
Uwingi daima ni bora maana una nguvu. Macho mawili ni bora zaidi kuliko bora. Umoja na ushirikiano ni ngao imara kabisa katika maisha. Katika umoja kuna ushirikiano na katika ushirikiano kuna mafanikio.
Chura kwa kawaida huishi majini. Twategemea kwamba ayajua vema mazingira yake. Kama ndivyo, basi yumkini afahamu urefu na ufupi wa maji. Yafaa kwa muogeleaji kutafuta ushauri wa chura hata kabla ya kuyazama maji. Ili tuufahamu undani na ukweli wa jambo yatubidi daima tufanye uchunguzi utakiwao. Njia mojawapo ya kuchunguza ni kuwauliza na kutaka ushauri wa hao wahusikanao na jambo hilo. Kuuliza ni kufahamu.
Methali nyingine :
|