FASIHI SIMULIZI: MUHADHARA WA TISA: METHALI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: FASIHI SIMULIZI: MUHADHARA WA TISA: METHALI (/showthread.php?tid=723) |
FASIHI SIMULIZI: MUHADHARA WA TISA: METHALI - MwlMaeda - 08-01-2021 MUHADHARA WA TISA: METHALI Methali ni tungo fupifupi zenye hekima na busara zitumiwazo kuonya,kuadibu na kuadilisha jamii.
Methali ni sehemu ya lugha inayoweza kufananishwa na kiungo cha lugha na kitoweo cha lugha. Hutumiwa kutafakari na kuyapima maisha,kujifunzia jumuiya na kutawalia jamii na mazingira ya binadamu.
Sifa za methali kwa mujibu wa M.M.Mulokozi:
– Methali huwa ni usemi mfupi na wenye urari wa maneno japo maneno hayo si mepesi nay a kawaida.
– Usemi huo ukubalike kwa watumiaji wa lugha husika.
– Usemi huo uwe unamleta msikilizaji katika kufikiri,kuchambua na kupatanisha ukweli ili ang’amue maana ya ndani ya usemi huo.
– Methali huwa na maana ya ndani na maana ya nje ambayo huelezwa kama mafumbo yanayohitaji ufafanuzi au ufumbuzi ili ziendane na mazingira halisi ya jamii.
MUUNDO WA METHALI
Methali nyingi huwa na muundo wa sehemu mbili. Sehemu ya kwanza huwa ni wazo/fumbo/swali na sehemu ya pili huwa ni jibu au ukamilifu wa wazo/fumbo.
USANII WA METHALI
Methali huwa na urari wa maneno yenye busara,mvuto wa lugha na tamathali mbalimbali za usemi.
Urari wa maneno
Mfano:
– Harakaharaka,haina Baraka
– Polepole ya kobe,humfikisha mbali
Tashibiha
Mfano:
– Utajiri ni kama umande
– Ujana ni kama moshi
– Ufalme ni kama maua
Sitiari
Mfano:
– Mapenzi ni majani,huota popote
– Kukopa harusi,kulipa matanga
– Ulimi ni upanga
Balagha/chuku
Mfano:
– Chovya chovya,humaliza buyu la asali
– Bandu bandu,humaliza gogo
Kejeli
Mfano:
– Mfinyanzi hulia gaeni
– Hindi ndiko kwenye nguo na wendapo uchi wako
– Wagombanao hupatana
– Ukienda kwa wenye chongo fumba lako jicho
– Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
DHIMA YA METHALI
(i) Ni kuwa ghala na kielelezo cha utamaduni wa mwafrika
(ii) Hutumika kuonya
(iii) Hutoa mausia
(iv) Hushauri
(v) Hufunza
(vi) Husuta
(vii) Hutia hamasa
(viii) Hushauri mtu kufanya maamuzi magumu
|